Mjadala wa Umoja wa Upinzani StarTV Dec 5, 2010

Ahsante Yahya,
Hapa Tanzania kumekuwa na hali ya kutoaminiana baina viongozi wa kisiasa kama ifuatavyo:-
  • VIONGOZI WA KISIASA HAWADUMU KATIKA NAFASI ZAO NDANI YA VYAMA KWA MATAKWA YA WANACHAMA, WANAODUMU HUWA NI KWA HALI MITHILI YA UDIKTETA NDIO HUDUMU.
  • VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA HAWANA UUNGWANA, IWAPO WATABADILIKA NA KUWA WAUNGWANA...BASI ITAKUWA RAHISI KWAO KUUNGANA.
  • VIONGOZI WENGI WA VYAMA VYA SIASA SI WASAFI NA HUIBUKA KWA MISIMU TU, BALI WOTE HUVUTIA KWAO NA SI KATIKA MASLAHI YA KITAIFA.
  • VIONGOZI WA SIASA HAWAKO TAYARI KUONA MWENZAKE YU JUU (mwenyekiti wa umoja wa vyama vya siasa nchini) NA BADALA YAKE HUJIPENDELEA KWA UBINAFSI NA KUJISAHAU DHAMIRA ILIYO MBELE YAO NA KATIKA JAMII.
  • VIONGOZI WA SIASA WANAPASWA KUWA neutral ILI KUUNGANA, KUEPUSHA UKABILA, KUEPUSHA UDINI, KUEPUSHA ENEO WANALOTOKA...ILIMRADI TU MASLAHI YA TAIFA YAWE NDIO AZMA YAO.
  • NJIA YA MUUNDO IWALAZIMU VIONGOZI WA KISIASA KUWA NA MAELEWANO NA SI MISIMAMO MIKALI, IWAPO WATADUMISHA KWA KUEPUSHA TOFAUTI ZAO NA WASIWE NA TAMAA ZA MADARAKA...BASI UMOJA UTADUMU.
Ni hayo ndg yangu Yahya Mohamed, ila ningeomba namba ya simu hapo mapema ili nitoe mchango hiyo kesho. Mada yenu ya leo haikuwa moto na muelezeni Benard James achangamke awapo kwenye kipindi.
 
Wise men talk because they have something to say; fools, because they have to say something. Am afraid most of irresponsible politicians are of this phrase from Plato. Beleive me majority Tanzanians are still in total blackout. These forums are a step ahead if not done mariciously.
Thanks for strong argument

Thanks Yahya, Together we can Build this Nation. I want to be party of it just because i cant see my future generation suffering because we didint take any action at this right moment. Please post the number here.

Thanks again
 
Umeyasoma mawazo ya Malunde pia?

Nimeyasoma lakini nikabonyea kwa sababu sijaelewa definition yake ya falsafa na namna inavyotofautiana na definition ya kauli mbiu. Pia ametumia utofauti wa hizo kauli mbiu zao kuthibitisha kwamba hawataweza kuungana. Nadhani fikra zake hazikuvuka mto, kwamba ziko one sided. Je, hizo kaulimbiu tofauti siyo mtaji wa kuunganisha nguvu za pamoja (sina maana kuunganisha vyama vyote)
 
Nimeyasoma lakini nikabonyea kwa sababu sijaelewa definition yake ya falsafa na namna inavyotofautiana na definition ya kauli mbiu. Pia ametumia utofauti wa hizo kauli mbiu zao kuthibitisha kwamba hawataweza kuungana. Nadhani fikra zake hazikuvuka mto, kwamba ziko one sided. Je, hizo kaulimbiu tofauti siyo mtaji wa kuunganisha nguvu za pamoja (sina maana kuunganisha vyama vyote)

Gurudumu
Thanks for response
 
Hiyo mada kwa sasa nadhan ingefika mwisho kwa maana ya kwamba tuliyoyasikia ndio hayo hayo tutakayoyasikia kesho.Kumleta Hamad na kushindwa kumleta Mbowe itakuwa ni kumpa Hamad uwanja wa kutamba atakavyo.Niliona siku ile katika ITV,Hamad alikuwa tayari amepandwa na jazba.Kusema hukutaka kufanya duplicate hilo si sahihi.Binafsi nimekuwa nikiwafuatilia sana nyie Star Tv.Kwa kweli awezaye kuendesha mijadala ya kisiasa hasa ni Dotto Bulendu pekee,nyie wengine mnaegemea upande mmoja.(Baruan na wewe).Kama Mbowe haji basi amueni hata Hamad asije.Kafulila tulishamwona kipindi kilichopita na Benson Bana.Nadhan NCCR mleteni Mbatia.
Maoni yangu ni kuwa kuunganisha upinzani kwa sasa hilo haliwezekani hasa kutokana na unafiki uliojitokeza hivi sasa.Wengi wa wapinzani wanakipinga chama cha Chadema na si CCM.

Ushauri kwa Star Tv:line zenu za simu ni mbaya hazikiki vizuri wakati mtu anapokuwa naongea.Mikwaruzo ni mingi sana.Jaribuni kutafuata mafundi competent wa kucontrol hili.
 
Yahya,nahisi hii mada badala ya kuwa constructive itageuka kuwa nani zaidi(kutunishiana misuri)hence divisive,wtz hatuhitaji upinzani ulioungana,tunahitaji upinzani wa kweli na imara hata kama ni wa watu 2(wawili)kuliko wingi usio na malengo kila m2 na lwake,kila chama kimeenda pekee kwa wananchi kikavuna kilivyovuna,kuungania bungeni ni kudhoofishana.NAWASILISHA
 
Hiyo mada kwa sasa nadhan ingefika mwisho kwa maana ya kwamba tuliyoyasikia ndio hayo hayo tutakayoyasikia kesho.Kumleta Hamad na kushindwa kumleta Mbowe itakuwa ni kumpa Hamad uwanja wa kutamba atakavyo.Niliona siku ile katika ITV,Hamad alikuwa tayari amepandwa na jazba.Kusema hukutaka kufanya duplicate hilo si sahihi.Binafsi nimekuwa nikiwafuatilia sana nyie Star Tv.Kwa kweli awezaye kuendesha mijadala ya kisiasa hasa ni Dotto Bulendu pekee,nyie wengine mnaegemea upande mmoja.(Baruan na wewe).Kama Mbowe haji basi amueni hata Hamad asije.Kafulila tulishamwona kipindi kilichopita na Benson Bana.Nadhan NCCR mleteni Mbatia.
Maoni yangu ni kuwa kuunganisha upinzani kwa sasa hilo haliwezekani hasa kutokana na unafiki uliojitokeza hivi sasa.Wengi wa wapinzani wanakipinga chama cha Chadema na si CCM.

Ushauri kwa Star Tv:line zenu za simu ni mbaya hazikiki vizuri wakati mtu anapokuwa naongea.Mikwaruzo ni mingi sana.Jaribuni kutafuata mafundi competent wa kucontrol hili.

Usitabiri shiriki katika mjadala na utatambua kuwa kila wakati siasa haina mwisho. Inaelekea hujashiriki mijadala hapa JF kwa muda. Utaendelea kulaumu mpaka lini. Toa Hoja. Hatukatai kukosolewa ila usiwe wimbo sasa be a critical thinker
 
Safari kuelekea umoja wa vyama vya siasa vya upinzani kwa masilahi ya umma bado ni ndefu. Nini mtazamo wenu wanaJF na umuhimu wa ushirikiano wa pamoja kwa vyama vya upinzani nchini.
Natanguliza shukrani zangu kwa ushiriki mzuri sana wiki iliyopita.

Mungu si mwanadamu.

Baada ya uchaguzi mkuu 2015, tumeshuhudia namna ambavyo kuna baadhi ya vyama ni washirika wa CCM, na kwa hivyo si busara kuviita vyama vya upinzani.

Maoni yangu:
Safari ni fupi. Wenye nia thabiti. Wenye moyo safi. Waungane na Chadema. Ndiyo chama pekee ambacho kama watawaondoa walafi na wachonganishi, basi siku si nyingi tutaikomboa nchi yetu.
 
Hakuona hoja ya falsafa maana amejifungia ndani ya box, akitoka ataona, nenda USA utaona falsafa ya democrat ma republican hawawezi kuungana maana wanatofautiana falsafa ambazo mwisho wa siku wanaziishi, inategema falsafa ipi ni muafaka kwa wakati kadhaa,
hatujafika maana uelewa mdogo na hili ni somo gumu najua mkuu hajui somo hili. People power si tamko ni falsafa inayowaunganisha wote wanaoamini ktk hilo, kudumisha mapinduzi ni falsafa ya mwl ili baada ya uhuru asije tokea msaliti wa mapinduzi, ndio maana nikasema kwa welewa hii sio issue maana hatuna threat ya kutawaliwa tena, bali tuna threat ya umaskini kushamiri. Muda utafika watu watakuwa na makundi mawili yanayokinzana na kila kundi lina haki sawa kuendeleza falsafa yake kwa ustawi wa jamii. Naamini soon tutafika huko, tutazika vyama vingine vyote, vitabaki viwili vyenye kupingana kwa hoja na vinavyotifautina kifalsafa na utekelezaji wa malengo ya jamii kila wakati kwa wakati. Kuna watu conservative (wanaamini maendeleo ni taratibu hamna haraka kama CCM ilivyo)na radical(wanaamini maendeleo kasi na utekelezaji kama chadema), wengine sijajua wako wapi ila itategemea uko kundi gani so itajidefine, ila mfano analysis zangu sera za ccm na cuf zinashaihia na huenda falsafa yao iko karibia sawa. Katiba inatakiwa ibebe makundi yote haya, iyalinde na yawe makundi ambayo yanasukuma mbele maendeleo. Katiba ya sasa haikidhi haja, ni gharama sana kuendelea nayo. Vyama vyote viungane kutengeneza katiba mpya ili tusonge mbele. Vyama havifai, havitakiwi, na si sawa kuungana kwa vyovyote. Waache wafu wawazike wafu wenzao, wazima waendelee na shughuli kama kawaida
 
Usitabiri shiriki katika mjadala na utatambua kuwa kila wakati siasa haina mwisho. Inaelekea hujashiriki mijadala hapa JF kwa muda. Utaendelea kulaumu mpaka lini. Toa Hoja. Hatukatai kukosolewa ila usiwe wimbo sasa be a critical thinker
<br />
<br />
Na nyinyi huwa mnaiuzi kwa ushabiki wa ccm hata kama bosi wenu ni ccm pls kuweni waandishi makini sio kukusanya watu kwa faida ya chama cha mapinduzi, mnajidhadhalilisha
 
Yahya,
Samahani sana. Shida ya kuunganisha vyama bungeni inatokea wapi? Hapa ndipo inabidi tutafakali na kujiuliza.Huu ni mkakati wa CCm kutupotezea muda wa kuongelea mambo ya muhimu kuliko hili. Katiba ndio issue kubwa sasa yenye haja ya kujadiliwa na si muungano wa vyama bungeni.

Kuna ukweli kwamba nyie waandishi wa habari ndio mmelifanya jambo hili kuwa kubwa kiasi hiki kwa sababu ushirikiano katika vyama haujawahi kuwapo na kama ungetakiwa kuwepo ulitakiwa uwepo hata kabla ya uchaguzi ili wakati wa uchaguzi vyama vya upinzani viingie kwenye uchaguzi vikiwa katika ushirika. Ni ajabu Bwana Yahya hamkulishikia bango kiasi hiki ingawa sie wengine tulihisi ni jambo la lazima. Kila chama kiliamua kuingia katika uchaguzi kikiwa pekee yake. Tena kila kimoja kikiomba kura na ridhaa ya wananchi peke yake.

Wakati huo hatukusikia CUF ikionea huruma vyama vidogo kama PPT maendeleo kwa kuvishawishi viingie ushirikiano nacho ili uchaguzi uongeze nguvu katika upinzani, bali kila mmoja alijinadi peke yake na kunadi sera zake, huku kikiomba ridhaa ya wananchi peke yake na tumeshuhudia wananchi waliweka wapi nguvu ya imani yao. Wengi walikiamini Chadema huku wakijua CUF na vyana vingine vingi tu vipo. Waliamini ni vyama visivyoweza kuleta mbadiliko. Walivinyima kura. Sasa kwa nini leo kuna mashinikizo kwamba lazima kuwepo ushirikiano?

Najiuliza na naomba uwaulize hao mliochagua kuwa katika mdahalo, kwa nini wanadhani leo ushirikiano unawezekana bungeni kama wakati wa uchaguzi haukuwezekana?. Tulitegemea kama kweli vyama vya upinzani vilitaka muungano basi walitakiwa kupata muungano huo nje ya bunge kwanza, lakini muungano ndani ya bunge hauwezekani kwa sababu zile zile zilizofanya wasiungane nje ya bunge. Tusiwaonee wananchi waliotoa ridhaa zao kwa kuwapa Chadema kura zao wakijua wazi kuwa watawawakilisha vema bila msaada wa hivi vyama vingine.

Lingine ni suala la katiba maana katiba ni suala la lazima na si la hiari kama CUF wanavyotaka kutuambia. Hivi tujiulize suali dogo kwamba je kama CUF wangekubalika kuongoza Zanzibar badala ya CCM je ingelikuwaje? je wao bado wangeendelea kuwa upinzani katika bunge la muungano? je CCM kama wangelikuwa kambi ya upinzani Zanzibar huku kwenye bunge la muungano wangelihesabika wapinzani au watawala?
Je leo CUF katika baraza la wawakilishi ni wapinzani? haya ni mapungufu makubwa ya kikatiba na hii inatakiwa kuwa hoja kubwa ya kuzungumziwa katika vyombo vya habari na sio hili la kuunganisha upinzani maana hawa wapinzani wote wanajitambua kuwa ni wapinzani. asiyetambua hili yeye ni sehemu ya serikali na abaki jinsi alivyo.

Yahya mijadala yenu isilengwe katika muungano wa vyama bungeni bali ilengwe katika kujadili mstakabli wa katiba ya nchi hii ambayo leo watawala wetu wameanza kusema hawaoni sababu ya kuijadili. Tusipoteze muda kujadili mambo yasiyo na faida huku tukiacha mambo yenye faida kwa wakati huu. Kuungana wapinzani bungeni hakusaidii kitu kama hawana muungano toka nje. Asante
 
Yahya kipindi chenu kizuri lakini ni kifupi sana hasa kwa simu za wasikilizaji mmetoa muda mfupi sana. Wengi wanapenda kuchangia lakini muda ni mfupi na si rahisi sana hata waalikwa kujibu kwa ufasaha kwenye mahitimisho kwani tayari wanakuwa na time limit. Kama kuna uwezekano filia namna ya ku solve shida hii.
 
Siungi mkono huu mdahalo una skewed motives kutokana na loss of credibility ya TBC
 
Gurudumu
Kama mada inavyosomeka nilitegemea uaanze kuonyesha njia sasa kwa kujenga hoja ambazo zitasaidia kutoa dira na si kupuuza mawazo mema ya waliotangulia hapo juu.
Lete hoja sasa ya msingi...kama mada inavyosomeka.
Thanks
Ndugu yangu Yahya! Kiukweli bado watu tumetawaliwa na siasa za upinzani za kishabiki ambazo hazina tija, hivyo basi badala ya kufaidika na mijadala hiyo mara zote itaendelea kuwa sehemu ya malumbani kwani watanzania wengi hatujijui tuko wapi na tunataka kwenda wapi!?

La Msingi, waulize kwa niaba yangu "Je kipindi hiki watakachokuwa madarakani watawafanyia nini watanzania?" haijalishi chama kina diwani mmoja ama mbunge. tunachohitaji kujua ni mchango wao kwa Wa-Tanzania. au nao watatuambia hawawezi kufanya lolote kwa sababu hawakupata u-rais? :embarrassed:
 
Back
Top Bottom