Mjadala: Muziki sio Haramu. Inategemea na uimbaji wake

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,882
MUZIKI SIO HARAMU; INATEGEMEA NA UIMBAJI WAKE

Anaandika Robert Heriel.

Ipo kasumba Kwa baadhi ya watu wenye Elimu ndogo ya Kidini na kiroho isemayo muziki mi haramu. Dhana hii ni potofu na upotofu wake unatokana na ufinyu wa elimu zote mbili yaani elimu Dunia na elimu Akhera.

Muziki sio haramu. Muziki ni Sanaa inayotumia ALA/vyombo vya muziki pamoja na sauti ya mwanadamu au kiumbe yeyote.
Muziki Kama Sanaa unalenga kuonyesha uzuri na ustadi wa mchanganyiko wa sauti zenye ladha zinazoburudisha. Muziki husisimua, hutia simanzi, huamsha Raha moyoni. Hata hivyo muziki ukiingiziwa nyimbo, au tenzi, au tendi au aina yoyote ya vipera vya ushairi huwa na dhima kadhaa WA kadha, mathalani; kuburudisha, kuelimisha, kukosoa, kuonya, kufunza, kuhamasisha, kutunza Mila na desturi miongoni mwa dhima zingine.

Muziki haujaanza Jana wala leo, tangu kale na kale na mpaka milele Daima muziki utakuwepo. Matumizi ya Ngoma, zeze, santuri, gitaa, filimbi, kinanda, marimba miongoni mwa ALA zingine za Muziki yatadumu milele zote. Ukuaji wa Teknolojia hukuza muziki na kuubadilisha katika viwango vingine vikuu.

Zipo Aina nyingi za Muziki, miongoni mwazo ni Muziki wa Kidini(muziki wa injili na muziki wa Qaswida Kwa waislam), BongoFleva, RnB, Rumba, Amapiano, Hip hop, Pop miongoni mwa Aina zingine.

Kila muziki Una Aina yake ya uwasilishwaji. Hata hivyo muziki yote lengo lake ni kuijenga jamii.

Muziki ni KAZI Kama KAZI zingine.
Ni KAZI halali na inayopaswa kuheshimiwa.
Na hapa nazungumzia Muziki wa kidunia kuacha hii muziki ya Dini(injili na Qaswida).

Muziki wa kidunia ni Halali ikiwa utatumika Kama ulivyokusudiwa.
Ikiwa wanamuziki watalenga kuweka maudhui yanayojenga jamii katika muziki wao.

Hatuwezi kumtaja Mungu kwenye kila Jambo. Kumtaja Mungu kwenye kila Jambo ni matumizi mabovu ya Uelewa. Mungu mwenyewe katika amri zake keshakataza jina lake lisitajwe bure ikiwa hakuna ulazima wa kufanya hivyo.

Yesu alikuwa anamsemo usemao; Ya Kaisari mpe Kaisari na Yamungu Mpe Mungu.

Kutojua kutenganisha mambo ni Dalili ya ujinga Kama sio upumbavu.

Lazima ujue kutofautisha vitu vilivyowekwa wakfu na vitu vya kawaida. Hiyo ndio Dalili ya werevu.

Muziki ni haramu Kama utashawishi watu kufanya maovu. Muziki ni haramu Kama utahamasisha watu kumuasi Mungu. Muziki ni haramu ikiwa wanamuziki wataimba matusi, watavaa mavazi ya kishetani katika Mazingira yasiyo wataka kufanya hivyo.

Muziki ni Kama ualimu, Udaktari, uhasibu, Uaskari, Uanasheria miongoni mwa KAZI zingine.
Ualimu ni haramu ikiwa mwalimu atafundisha mambo yasiyofaa, mambo yanayoharibu jamii
Udaktari halikadhalika na kazi zingine.

Uharamu ni kitendo cha kufanya Jambo kinyume na inavyotakiwa, kufanya Jambo linalodhuru na kuharibu jamii. Huo ndio uharamu.

Muziki wa kidunia unaokatazwa na Mungu ni ule unapojaribu maadili ya jamii, unaofunza watu roho mbaya, unaodhalilisha utu WA binadamu, unaodhalilisha kazi za uumbaji wa Mungu, huo ndio muziki unaokatazwa.

Watu wa dini wasipotoshe na kuiharibu jamii kuwa watu wasiimbe nyimbo za kidunia kuwa ni dhambi, isipokuwa wawafundishe watu maadili ili wasiimbe mambo yanayoharibu jamii.

Tumezaliwa Duniani, Sisi ni wadunia, Duniani ndio kwetu, kwa nini tusiiimbe nyimbo za kikwetu(kidunia), hatuwezi kuwa na mtazamo Hasi Kwa kila kitu kwenye dunia hii.

Dunia ndio Mama yetu, Baba yetu ni MUNGU. Sio kosa kuimba za kidunia ikiwa hatutukani, hatudhalilishi yeyote, hatuvunji sheria za nchi na maadili yetu kulingana na tamaduni zetu.

Huwezi muimbia mchumba wako nyimbo na muziki mzuri alafu ukaiita hiyo ni yadini utakuwa umechanganyikiwa,
Hata Suleiman katika wimbo uliobora anatupa mfano Bora wa namna nyimbo za kidunia zinavyopaswa kuwa. Kwa maana wimbo ulio bora sio wimbo wa dini isipokuwa ni wimbo wa kidunia ambao Suleiman alikuwa akimuimbia Mpenzi wake.

Wito Kwa Wasanii wa muziki;
Jitahidini muimbe nyimbo zenu Kwa kufuata maadili ya utamaduni wa jamii yetu ili kuondoa hii Dhana potofu kuwa muziki ni haramu, Kwa maana Kama mtaimba nyimbo zinazohamasisha mambo haramu basi mnaufanya muziki wenu uitwe haramu.
Na hii itawafanya msiheshimike.

Baadhi ya wanamuziki ndio mnafanya kazi ya muziki idharauliwe na ninyi pia mdharaulike.
Sio ajabu kijana mwanamuziki akakosa mchumba kwenye familia inayojielewa Kwa sababu ya kuimba upumbavu.

Mwanamuziki unaweza kuwa na mafanikio makubwa ya kiuchumi na kufahamika Kwa watu lakini kutokana na nyimbo zenu mkadharaulika tuu.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
If God says this is wrong....YOUR OPINION DOESNT MATTER

Hata wanaosema muziki ni haramu ni maoni Yao.

Ukisoma Biblia au Quran lazima ujue kutofautisha maoni ya mwandishi (mtume au Nabii) na neno la Mungu.

Usidhani kila kilichoandikwa kwenye Biblia au Quran ni maneno kutoka Kwa MUNGU.
Mengine ni maoni ya Waandishi huitwa MAPOKEO
 
MUZIKI SIO HARAMU; INATEGEMEA NA UIMBAJI WAKE.

Hata Suleiman katika wimbo uliobora anatupa mfano Bora wa namna nyimbo za kidunia zinavyopaswa kuwa. Kwa maana wimbo uliobora sio wimbo wa dini isipokuwa ni wimbo wa kidunia ambao Suleiman alikuwa akimuimbia Mpenzi wake.

Wito Kwa Wasanii wa muziki;
Jitahidini muimbe nyimbo zenu Kwa kufuata maadili ya utamaduni wa jamii yetu ili kuondoa hii Dhana potofu kuwa muziki ni haramu, Kwa maana Kama mtaimba nyimbo zinazohamasisha mambo haramu basi mnaufanya muziki wenu uitwe haramu.
Na hii itawafanya msiheshimike.

Baadhi ya wanamuziki ndio mnafanya kazi ya muziki idharauliwe na ninyi pia mdharaulike.
Sio ajabu kijana mwanamuziki akakosa mchumba kwenye familia inayojielewa Kwa sababu ya kuimba upumbavu.

Mwanamuziki unaweza kuwa na mafanikio makubwa ya kiuchumi na kufahamika Kwa watu lakini kutokana na nyimbo zenu mkadharaulika tuu.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Nina maswali kadhaa nataka nikuulize.

1. Ni upi msingi wa kujua lipi halali na lipi haramu ?

2. Je faida ya mziki ni kubwa kuliko hasara ama hali ikoje ?

3. Hujatuonyesha kutokuelewa kwa watu au sisi tunaosema muziki ni haramu kwa kurejea mafundisho yetu ya dini na kutuelewesha mafundisho yetu yamemaanisha nini ?

Mfano kwetu sisi Waislamu kuna hii Hadithi ya Mtume inasema hivi :

Amehadithia Abuu ‘Aamir au Abuu Maalik kwamba kamsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Watakuweko watu katika Ummah wangu watakaojaribu kuhalilisha zinaa, uvaaji wa hariri, pombe na muziki. Baadhi ya watu watakuwa pembeni mwa mlima na mchungaji wao atawajia jioni na kuwaomba haja [fulani]. Watasema: "Rudi kesho". Allaah Atawaangamiza usiku, Atawaangushia milima kisha Atawabadilisha waliobakia wawe nyani na nguruwe na watabakia hivyo hadi siku ya Qiyaamah)) [Al-Bukhaariy]

Huo ni mfano katika nukuu nyingi za toka katika Dini yetu zizi Waislamu.

Lakini kingine ni kiwa laiti kama Muziki ungekuwa na faida basi wangetumia Mitume na manabii kuwaonya watu.

Shukrani.
 
Mbona wapo manabii waliotumia muziki akina Daudi na Suleiman.

Muziki ni sehemu ya burudani Kwa wanadamu.

Sasa kwenye sherehe za usiku ulitaka watu waweke Waswida au Injili Pale.

Kuna muziki wa misikitini, kanisani, misibani, HARUSINI, kilabuni, shambani n.k.

Kila muziki uimbwe kwenye muktadha wake.

Hata huo muziki wa Qaswida au injili ukiimbwa kilabuni ni haramu Kwa sababu umeimbwa sehemu isiyosahihi.
 
Hata wanaosema muziki ni haramu ni maoni Yao.

Ukisoma Biblia au Quran lazima ujue kutofautisha maoni ya mwandishi (mtume au Nabii) na neno la Mungu.

Usidhani kila kilichoandikwa kwenye Biblia au Quran ni maneno kutoka Kwa MUNGU.
Mengine ni maoni ya Waandishi huitwa MAPOKEO
Mkuu ONDOA QURAN hapo, hakuna neno la MTUME MUHAMMAD (S.A.W) Mule ndani, wala hakuna story za yeye alizaliwa wapi na maisha yake.
 
Mbona wapo manabii waliotumia muziki akina Daudi na Suleiman.
Unao ushahidi wa hili ? Naomba utuwekee ushahidi kaka.
Muziki ni sehemu ya burudani Kwa wanadamu.

Sasa kwenye sherehe za usiku ulitaka watu waweke Waswida au Injili Pale.

Kuna muziki wa misikitini, kanisani, misibani, HARUSINI, kilabuni, shambani n.k.

Kila muziki uimbwe kwenye muktadha wake.

Hata huo muziki wa Qaswida au injili ukiimbwa kilabuni ni haramu Kwa sababu umeimbwa sehemu isiyosahihi.
Mpaka najiukiza kwanini hujibu maswali niliyo kuuliza.
 
Nina maswali kadhaa nataka nikuulize.

1. Ni upi msingi wa kujua lipi halali na lipi haramu ?

2. Je faida ya mziki ni kubwa kuliko hasara ama hali ikoje ?

3. Hujatuonyesha kutokuelewa kwa watu au sisi tunaosema muziki ni haramu kwa kurejea mafundisho yetu ya dini na kutuelewesha mafundisho yetu yamemaanisha nini ?

Mfano kwetu sisi Waislamu kuna hii Hadithi ya Mtume inasema hivi :

Amehadithia Abuu ‘Aamir au Abuu Maalik kwamba kamsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Watakuweko watu katika Ummah wangu watakaojaribu kuhalilisha zinaa, uvaaji wa hariri, pombe na muziki. Baadhi ya watu watakuwa pembeni mwa mlima na mchungaji wao atawajia jioni na kuwaomba haja [fulani]. Watasema: "Rudi kesho". Allaah Atawaangamiza usiku, Atawaangushia milima kisha Atawabadilisha waliobakia wawe nyani na nguruwe na watabakia hivyo hadi siku ya Qiyaamah)) [Al-Bukhaariy]

Huo ni mfano katika nukuu nyingi za toka katika Dini yetu zizi Waislamu.

Lakini kingine ni kiwa laiti kama Muziki ungekuwa na faida basi wangetumia Mitume na manabii kuwaonya watu.

Shukrani.
Sio kila kitu walichofanya mitume nawewe ukifanye ndio kuonyesha kwamba ni halali, au vile ambavyo hawajafanya mitume basi ni dhambi kuvifanya

Mbona mitume haikutumia vipaza sauti na maspeaker kwenye mahubiri, kwa hiyo na hiyo ni dhambi?

Utahitaji kutafuta andiko lililoruhusu matumizi ya speakers na vipaza sauti kwenye mahubiri ili ujue ni halali au haramu?
 
ma miziki ya ovyo ovyo na yaliyo jaaa mitusi kama ya diamond au mitaarabu ya mzee Yusuf siyo haram kwelii???
 
Waimbaji ndio wanaoimba muziki Haramu Ila muziki sio haramu.

Mfano, Askari wanaofanya dhuluma na unyanyasaji ndio wafanye Uaskari uitwe Haramu??

KAZI yoyote ukifanya kinyume na utaratibu hugeuka kuwa haramu. Sijui Kama unanielewa
 
Sio kila kitu walichofanya mitume nawewe ukifanye ndio kuonyesha kwamba ni halali, au vile ambavyo hawajafanya mitume basi ni dhambi kuvifanya
Unajua unacho kiandika na unarejea kwenye nini ?
Mbona mitume haikutumia vipaza sauti na maspeaker kwenye mahubiri, kwa hiyo na hiyo ni dhambi?
Kwami vipasa sauti ni sharti la kukubaliwa ibada ya mtu ?

Nakuuliza tena unakijua unachokijadili ?
 
Umesema ndani ya QURAN yapo maoni ya MTUME ndio maana nimesema kwenye hiko kitabu kitoe maana hakuna maoni ya Mtu Muhammad (S.A.W). Maoni yake utayakuta kwenye Hadithi na sio kwenye QURAN.

Ndio maana nikasema huko kwenye Quran kuna Aya inasema muziki ni haramu??
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom