jebs2002
JF-Expert Member
- Sep 3, 2008
- 8,835
- 7,600
Wenzako wala hawajali hiki, ndio kwanza wanafikiria kuongeza ndege nyingine ya kifahari! Kazi ipo sana, sana sana..Nilishawahi sema, nimeshuhudia hayo magari ya kifahari, VX6-VX8 yanapowashwa tangu asubuhi hayazimwi mpaka wakati dereva anapolala! Yaani hata kama gari imepaki ofisi au kwenye shughuli za mheshimiwa hakuna kuzimwa, kisa eti gari liwe na baridi ndani! Yaani jamaa wanaponda hela za mlipa kodi kama hawana akili nzuri..Sasa fikiria nimeona kama 2 au 3, je yako mangapi serikalini yanafanya hivi? Si mchezo hela zinavyochomwa moto..Salaam,Ni hayo tu.