Ubumuntu
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 14,340
- 10,866
Salaam,
Kama kichwa kinavyojieleza. Kumekuwa na mjadala wa miaka mingi juu ya aina ya magari ambayo viongozi wetu wa kiserikali wanayatumia kwa shughuli zao za kila siku.
Binafsi, nimekuwa nikisema mara kwa mara kwamba viongozi wetu wanaishi kama mastaa wa Hollywood kupitia migongo yetu walipa kodi.
Sasa baada ya kuona namna Rais mpya wa Ufaransa alivyo walk the talk, nikaona ni vyema tuendeleze huu mjadala. Angalia picha nilizoambatanisha hapa. Na pengine tuzidi kuishauri serikali ya Magufuli, ambayo inasisitiza katika dhana ya kubana matumizi.
Sina takwimu halisi ya namna gani magari ya viongozi yanaligharimu taifa, ila kwa kutumia uzoefu na common sense, ni rahisi kusema magari hayo yanaligharimu taifa pesa nyingi bila sababu za msingi.
Kuna ulazima gani wa Rais kutumia magari ya kifahari ya aina ya BMW? Katika msafara wake kuna BMW 7 series na BMW X5.
Kuna ulazima gani kwa VP kutumia Mercedes Benz GL Class? Kuna ulazima gani kwa PM na Spika kutumia Mercedes Benz S Class? Kuna ulazima gani kwa mawaziri, manaibu waziri, wakurugenzi, wakuu wa vyuo vya umma, wakuu wa polisi wa wilaya na mikoa, RCs, DC n.k. kutumia Land Cruisers 200 aidha VX au GX?
Hizi gari pamoja na bei ya kununua kuwa aghali, vilevile matunzo yake na utumiaji wa mafuta unaligharimu taifa fedha nyingi.
Kuna kipindi PM Pinda alitoa mwongozo juu ya aina ya magari kwa viongozi. Nakumbuka hadi Waziri Lukuvi akasema viongozi wataanza kutumia Suzuki Grand Vitara ama Toyota Rav4. Vilevile huyu bwana mkubwa wa sasa kwenye kampeni aliongelea juu ya haya magari ya viongozi. Ila bado mambo ni yale yale.
Kwanini inawawia vigumu kwa hawa viongozi kuamua kufanya angalau kama walivyojaribu Kenya kwa mawaziri kuanza kutumia VW Passat? Ingawa sijui kama utaratibu huo bado upo sasa. Hivi Rais akiendeshwa kwenye VW Passat kuna shida gani? Licha ya kujisifu kwamba serikali ya CCM imejenga mabarabara kila kona ya nchi, kwanini bado Land Cruisers zinatumika?
Kwa upana zaidi: hivi kuna ulazima wa viongozi wa serikali (pengine ukitoa wakuu wa mihimili ya dola) kupewa magari ya kutumia 24/7?
Ni hayo tu.