Mjadala: Magari ya viongozi wetu na dhana ya kubana matumizi

Braza ni aidha unajitoa ufahamu ama uwezo wako wa kuelewa ni mdogo. Mimi sijasema hizo Passat zitumike off road. Ebu usome na kuelewa basi mzee.
Kifupi viongozi wetu wakiingia madarakani wao wanasahau wako pale kama wito, kusaidia jamii, kurekebisha hali mbaya ya umaskini na shida kwa raia, sasa wao ndio kama wamepewa visa ya kufanya mastarehe na kusahau huku chini kabisa, yale mambo ya kusimamishana barabarani kwa masaa, wala hawajali, kwanini wasitumie helikopta?! Kwao raia sababu yuko chini basi aendelee kukandamizwa tu, siku ya kura/kula utawaona wakijifananisha nasi! Hata ukusanye kodi kiasi gani, au uwe na maliasili kiasi gani, bila kubana matumizi hasa serikalini nchi kama yetu haiwezi endelea kabisa, nchi tajiri kuliko sisi zabana matumizi itakuwa sisi, wabunge wangapi umewaona wakiacha mashangingi wakipanda mwendo kasi achilia daladala?! Maana mpaka wafanye hivyo ndio wataelewa kututumikia, otherwise yatakuwa yale yale, sijaona sehemu yoyote ya maana waliobana matumizi, wangeanza na hapa kwenye haya mambo ya usafiri na matumizi yake..
Wakumbuke sie tunaolalamika sio kwamba hatuwapendi, lahasha, twataka waendelee kutuongoza kwa kufanya haya kwanza, wakuta mtaa wenu barabara mbaya mno, cha kushangaza hata watu wa tanroads na ujenzi wapo, ila hakuna initiative wala nini, nao wanapita kwenye mahandaki kama nyinyi bila aibu wala aiba! Tubadilike, watusikie raia tuombalo..
 
Salaam,

Kama kichwa kinavyojieleza. Kumekuwa na mjadala wa miaka mingi juu ya aina ya magari ambayo viongozi wetu wa kiserikali wanayatumia kwa shughuli zao za kila siku.

Binafsi, nimekuwa nikisema mara kwa mara kwamba viongozi wetu wanaishi kama mastaa wa Hollywood kupitia migongo yetu walipa kodi.

Sasa baada ya kuona namna Rais mpya wa Ufaransa alivyo walk the talk, nikaona ni vyema tuendeleze huu mjadala. Angalia picha nilizoambatanisha hapa. Na pengine tuzidi kuishauri serikali ya Magufuli, ambayo inasisitiza katika dhana ya kubana matumizi.

View attachment 512594

Sina takwimu halisi ya namna gani magari ya viongozi yanaligharimu taifa, ila kwa kutumia uzoefu na common sense, ni rahisi kusema magari hayo yanaligharimu taifa pesa nyingi bila sababu za msingi.

Kuna ulazima gani wa Rais kutumia magari ya kifahari ya aina ya BMW? Katika msafara wake kuna BMW 7 series na BMW X5.
Kuna ulazima gani kwa VP kutumia Mercedes Benz GL Class? Kuna ulazima gani kwa PM na Spika kutumia Mercedes Benz S Class? Kuna ulazima gani kwa mawaziri, manaibu waziri, wakurugenzi, wakuu wa vyuo vya umma, wakuu wa polisi wa wilaya na mikoa, RCs, DC n.k. kutumia Land Cruisers 200 aidha VX au GX?

Hizi gari pamoja na bei ya kununua kuwa aghali, vilevile matunzo yake na utumiaji wa mafuta unaligharimu taifa fedha nyingi.

Kuna kipindi PM Pinda alitoa mwongozo juu ya aina ya magari kwa viongozi. Nakumbuka hadi Waziri Lukuvi akasema viongozi wataanza kutumia Suzuki Grand Vitara ama Toyota Rav4. Vilevile huyu bwana mkubwa wa sasa kwenye kampeni aliongelea juu ya haya magari ya viongozi. Ila bado mambo ni yale yale.

Kwanini inawawia vigumu kwa hawa viongozi kuamua kufanya angalau kama walivyojaribu Kenya kwa mawaziri kuanza kutumia VW Passat? Ingawa sijui kama utaratibu huo bado upo sasa. Hivi Rais akiendeshwa kwenye VW Passat kuna shida gani? Licha ya kujisifu kwamba serikali ya CCM imejenga mabarabara kila kona ya nchi, kwanini bado Land Cruisers zinatumika?

View attachment 512595

Kwa upana zaidi: hivi kuna ulazima wa viongozi wa serikali (pengine ukitoa wakuu wa mihimili ya dola) kupewa magari ya kutumia 24/7?

Ni hayo tu.

Magari ya gharama hununuliwa hasa hizo prado kutokana na hali ya barabara za Tanzania viongozi huwa ni wenye kusafiri mikoa mingi na yenye barabara mbovu.......Hawawezi nunua gari ndogo...
 
Magari ya gharama hununuliwa hasa hizo prado kutokana na hali ya barabara za Tanzania viongozi huwa ni wenye kusafiri mikoa mingi na yenye barabara mbovu.......Hawawezi nunua gari ndogo...
Kwa kununua hayo magari ya bei hizo, kwa akili zao au zako ndio waona solution ya kubana matumizi?!
Kuna mtu kasema hapa, sio lazima kila kiongozi awe na VX/GX, kwanini hawaazimani?! Maana yote ni ya serikali, kwanini kila mtu awe na lake? Uko Dar Es Salaam mjini, masaki to posta, wahitaji VX ya nini? Kwanza hawa kila mtu analo gari lake, kwanini serikali iwanunulie hayo ya bei kubwa?! Swala hatujuwi matumizi, hata tuwe na Phd au Masters, twapenda kuponda hela za mlipa kodi kama hatuna akili sawa, hatumjali maskini wala yule wa kijijini, kwanza sie wale baadaye, hata wasome kivipi hawa viongozi kubadilika ili wamtumikie raia sio rahisi, wana akili ya kupe kabisa, wanyonye mpaka basi, hata wakivimbiwa na kutapika bado wamo tu kunyonya damu!
 
wewe kweli akili huna...waazimane kwahiyo mmoja akiwa safari mwingine akipata safari ya ghafla inakuwaje...
hayo magari ni haki yao...ngoja tukiwa na barabara nzuri nchi nzima ndio wataweza nunua gari za bei nafuu..

ingekuwa ni gari za bei ghali wangenunua vogue..ila kwa kuwa ni VX sio ghali bali wewe ndio unaona ghali..

google expensive cars uone ni zipi ndipo useme...
 
Na mbaya zaidi wanatumia hayohayo magari yakuwabebea wakurugenzi au maafisa utumishi kuchukulia wake za watu au mademu za watu,inauma.
Kuna waziri mmoja kitambo kidogo alikua anaenda kumchukua binti anaitwa Shundi Malombo na jiVX jeusi huko chuo kikuu Dar. Gari namba za serikali. Na binti inadaiwa alikuja kuzaa nae na akagaiwa nyumba za serikali jirani na hicho chuo. Mlio Dar hayo ni kweli?
 
...hawa wezi wa kwenye utawala wa tz hawawezi kujifunza maana wamejawa na roho za kimaskini....wao lengo lao kuwa madarakani ni kutuibia...hivyo kuwapa mifano hii ni kama kumpigia mbuzi gitaa..,kama ni kujifunza wangeshajifunza miaka mingi....
 
wewe kweli akili huna...waazimane kwahiyo mmoja akiwa safari mwingine akipata safari ya ghafla inakuwaje...hayo magari ni haki yao...ngoja tukiwa na barabara nzuri nchi nzima ndio wataweza nunua gari za bei nafuu..ingekuwa ni gari za bei ghali wangenunua vogue..ila kwa kuwa ni VX sio ghali bali wewe ndio unaona ghali..google expensive cars uone ni zipi ndipo useme...
Wewe ndio nakuona zuzu kabisa unaetetea ununuzi wa haya magari, na ndio maana hata Kagame alinunua tofauti na haya, watetea nini kama sio mfaidika? Mjinga kabisa, gari moja jipya pale waweza jenga madarasa mangapi? Ukapata madawati mangapi? Ambulance ndogo ngapi? Mashine na vitanda hosptilani vingapi? Madawa nakadhalika, na kama hujafikiria haya basi kweli wewe huishi hapa TZ, na kama upo basi ndio yale yale mavyeti feki au kusoma kwa kukariri..
 
Salaam,

Kama kichwa kinavyojieleza. Kumekuwa na mjadala wa miaka mingi juu ya aina ya magari ambayo viongozi wetu wa kiserikali wanayatumia kwa shughuli zao za kila siku.

Binafsi, nimekuwa nikisema mara kwa mara kwamba viongozi wetu wanaishi kama mastaa wa Hollywood kupitia migongo yetu walipa kodi.

Sasa baada ya kuona namna Rais mpya wa Ufaransa alivyo walk the talk, nikaona ni vyema tuendeleze huu mjadala. Angalia picha nilizoambatanisha hapa. Na pengine tuzidi kuishauri serikali ya Magufuli, ambayo inasisitiza katika dhana ya kubana matumizi.

View attachment 512594

Sina takwimu halisi ya namna gani magari ya viongozi yanaligharimu taifa, ila kwa kutumia uzoefu na common sense, ni rahisi kusema magari hayo yanaligharimu taifa pesa nyingi bila sababu za msingi.

Kuna ulazima gani wa Rais kutumia magari ya kifahari ya aina ya BMW? Katika msafara wake kuna BMW 7 series na BMW X5.
Kuna ulazima gani kwa VP kutumia Mercedes Benz GL Class? Kuna ulazima gani kwa PM na Spika kutumia Mercedes Benz S Class? Kuna ulazima gani kwa mawaziri, manaibu waziri, wakurugenzi, wakuu wa vyuo vya umma, wakuu wa polisi wa wilaya na mikoa, RCs, DC n.k. kutumia Land Cruisers 200 aidha VX au GX?

Hizi gari pamoja na bei ya kununua kuwa aghali, vilevile matunzo yake na utumiaji wa mafuta unaligharimu taifa fedha nyingi.

Kuna kipindi PM Pinda alitoa mwongozo juu ya aina ya magari kwa viongozi. Nakumbuka hadi Waziri Lukuvi akasema viongozi wataanza kutumia Suzuki Grand Vitara ama Toyota Rav4. Vilevile huyu bwana mkubwa wa sasa kwenye kampeni aliongelea juu ya haya magari ya viongozi. Ila bado mambo ni yale yale.

Kwanini inawawia vigumu kwa hawa viongozi kuamua kufanya angalau kama walivyojaribu Kenya kwa mawaziri kuanza kutumia VW Passat? Ingawa sijui kama utaratibu huo bado upo sasa. Hivi Rais akiendeshwa kwenye VW Passat kuna shida gani? Licha ya kujisifu kwamba serikali ya CCM imejenga mabarabara kila kona ya nchi, kwanini bado Land Cruisers zinatumika?

View attachment 512595

Kwa upana zaidi: hivi kuna ulazima wa viongozi wa serikali (pengine ukitoa wakuu wa mihimili ya dola) kupewa magari ya kutumia 24/7?

Ni hayo tu.
unathaminisha watu kwa kuwaangalia...unadhani wote ni wajuzi wa magari
 
Bado huzingatii Hali ya miundombinu ya TZ iliyopo. Wote tunatamani ingekua hivyo ila uhalisia unakataa. Nje wanatumia baiskeli kwenda kazini kama PM wa Netherlands sababu miundombinu inaruhusu wakati TZ bado. Matumizi ya haya magari haimaanishi jitihada za kuboresha miundombinu zimesimama, until then haya magari yataendelea kutumika.

Kwa logic yako, unamaanisha ikitokea nyumbani kwako kuna tatizo la choo, wewe kama baba utajinunulia "portable toilet" na wengine waliobaki watumie vichaka?
 
Kwa logic yako, unamaanisha ikitokea nyumbani kwako kuna tatizo la choo, wewe kama baba utajinunulia "portable toilet" na wengine waliobaki watumie vichaka?
Hawa jamaa wanafikiri TZ bado kuna mazuzu, makazi ya mawaziri ni karibu na mjini kabisa, sioni sababu ya kutumia yale madude kwa safari fupi namna ile, yako mengi mno bila sababu, kusafiri kwenda mikoani sio sababu, mbona yakiweka yote kwenye pool moja yatatosheleza usafiri wao wa mikoani kama alivyoshauri mdau fulani humu?! Kuna haja kweli ya kuendelea kuyanunua haya?! Tunawashauri watu wenye phd na masters, lakini kwao ni kung'ang'ania kuyatumia haya matia hasara tu..kunani?! Vyeti feki au kukariri?!
 
Magari ya gharama hununuliwa hasa hizo prado kutokana na hali ya barabara za Tanzania viongozi huwa ni wenye kusafiri mikoa mingi na yenye barabara mbovu.......Hawawezi nunua gari ndogo...
Kwa hiyo BMW 7 series, Mercedes Benz S class na Mercedes Benz GL class yananunuliwa ili yatumike kwenye barabara mbovu?

BTW, I thoght CCM inajisifia mara milioni kwamba imejenga barabara nchi nzima. Kumbe ni fiksi za mchana kweupe?
 
Kwa hiyo BMW 7 series, Mercedes Benz S class na Mercedes Benz GL class yananunuliwa ili yatumike kwenye barabara mbovu? BTW, I thoght CCM inajisifia mara milioni kwamba imejenga barabara nchi nzima. Kumbe ni fiksi za mchana kweupe?
Hapo ndipo utawaelewa kwanini walipata shida uchaguzi uliopita, sababu bado hawataki kusikiliza raia wao wanataka nini toka kwao, sasa unakuja tena 2020, wakiendelea na dhana hizi kuwa watashinda tu hata iweje wamepotea, muda ni huu kuwasikiliza raia, wabane matumizi, wapunguze starehe za magari ya kifahari, nyumba zao, ndege zao na maposho yao, walete hela mitaani zifanye kazi, haka kamvua tu kametutoa nishai ya kufa mtu, solution yao nini? Kununua VX/GX/BMW?!
 
Unasema Waziri/mbunge/kiongozi atumie gari lake kufanya kazi za umma? Toka lini au nchi gani viongozi wanatumia pesa zao kufanya kazi za umma.
Kufanya kazi ya umma maana yake nini, anafanya bure?

Basi kila mwajiriwa wa umma apewe gari, mafuta na dereva bure! Au wengine hawafanyi "kazi ya umma"?

Kiongozi yeyote yule ni mwajiriwa kama watu wengine, analipwa mshahara, na anatakiwa afike kazini kila asubuhi kwa jinsi anavyojua.

Wewe unapoenda kazini, public or private sector, mwajiri anakupa gari, mafuta na dereva bure?
 
Dah! Thanks a million mkuu kwa this thoughtful post. Yaani watanzania ni watu wa aina ya pekee duniani. Licha ya kuteseka na umaskini, lakini mtu bado anatetea hizo undeserving privileges ambazo viongozi ujipatia.

Sielewi kwanini wataalamu wa masuala ya akili hawajafahamu kwamba wanaweza kupata groundbreaking findings kwa kufanya tafiti juu ya akili za watanzania.
 
Dah! Thanks a million mkuu kwa this thoughtful post. Yaani watanzania ni watu wa aina ya pekee duniani. Licha ya kuteseka na umaskini, lakini mtu bado anatetea hizo undeserving privileges ambazo viongozi ujipatia. Sielewi kwanini wataalamu wa masuala ya akili hawajafahamu kwamba wanaweza kupata groundbreaking findings kwa kufanya tafiti juu ya akili za watanzania.
Kazi ipo aise, sasa kama zile nyumba wanasema wawajengee viongozi, kweli kuna haja?! Maana 110% ya wote wana majumba, kama kweli wanatutumikia kuna ubaya gani wakae kwao, yaani hakuna uchungu, sababu tu hela mlipa kodi ipo pale basi wanailekeza kule, yale mambo yaliyo machoni pao hasa kipindi hiki cha mvua wala?! Nawashangaa sana aise..
 
proxy

Zungumzia tanzania.
Barabara tunazojisifia zinakidhi mahitaji kwa asilimia chini ya 50.
asilimia kubwa ya sehemu muhimu leo haziendeki hadi kiangazi kianze.
KUJITAPA ubora wa barabara KULNGINISHA NA wakati uliopita sio KUlinganisha na LONDON mkuu
111332.jpg

HAPO VITS LABDA UIBEBE. Suggest right altenative mkuu. Hakuna anependa kuyaona haya magari ya gharama kama yana mbadala wenye kukidhi mahitaji
Inatakiwa waende na vitz ili wajue changamoto, a raia wao

Mkuu hicho kichwa cha habari kimenikumbusha dereva wa mkurugenzi anayelala na gari la serikali tabata aamke nalo asubuhi kumchukua boss bunju ili ampeleke kazini posta.

Kwetu kuna mambo huwa sijui kwanini hayaingizwi kwenye vitabu vya Guiness.
Nimependa sana hii kitu. only in Africa,upuuzi upuuzi kila kona.
 
Back
Top Bottom