Mjadala: Magari ya viongozi wetu na dhana ya kubana matumizi

kama kweli wanatutumikia


Wanatutumikia kivipi, wanatununulia maziwa ya watoto?

Wanazitumikia familia zao na matumbo yao, kama mbavyo mimi ninavyoamka asubuhi nakwenda kazini kutafuta mshahara, nalitumikia tumbo langu na familia yangu!

Mbona mimi bosi wangu hajui na hataki kujua nafika fikaje kazini? Kwa nini mimi ufanyakazi wangu hauna thamani, mimi paka?

Au mimi ni illegal immigrant hapa Tanzania kama Wa-Mexico na waruka Visa wa Marekani wanaolipwa chini ya meza hawana haki zozote kazini?

Kwa nini tunakuwa brainwashed kuwasujudia viongozi namna hii?
 
Wanatutumikia kivipi, wanatununulia maziwa ya watoto? Wanazitumikia familia zao na matumbo yao, kama mbavyo mimi ninavyoamka asubuhi nakwenda kazini kutafuta mshahara, nalitumikia tumbo langu na familia yangu! Mbona mimi bosi wangu hajui na hataki kujua nafika fikaje kazini? Kwa nini mimi ufanyakazi wangu hauna thamani, mimi paka? Au mimi ni illegal immigrant hapa Tanzania kama Wa-Mexico na waruka Visa wa Marekani wanaolipwa chini ya meza hawana haki zozote kazini? Kwa nini tunakuwa brainwashed kuwasujudia viongozi namna hii?
Cha kushangaza hawa wanalilia magari na nyumba za serikali angali wanazo za kutosha, majumba kila kona, magari mpaka parking haitoshi! Anyway tunachoomba, magari yanayotumika mijini yawe economically, yale ya kutembelea vijijini wawe wanaazimana, maana wote wameajiriwa serikalini anyway, sio kila siku wanaenda vijijini anyway..maana kama wangekuwa wanakwenda huko, basi miundo mbinu vijijini ingebadilika maana huwezi kwenda kila mara kule halafu usifanye lolote, zile sio barabara, sio vichochoro hazina jina maalum..
 
Sikiliza wewe "nyau".Ngoja ifike mwaka 2020,gombea wewe urais,ukishinda tumia Toyo kwenye serikali yako.
Go @Magufuri go,ulipo tupo!!
 
Hap mkuu sio suala la kununua tu. Ukichukulia mfano ufaransa kila Rais ambaye amekuwepo amekuwa na choice ya gari gani (BRAND)atatumia kulinga na upenzi au ushabiki wakehapo ghalama haihusiki. KWa Rais lazima atumie gari secured mkuu bila kujali Ghalama. Maisha yake yanathamani kuliko Chombo anachotembelea kwa sababu anawakilisha watu zaidi ya mi 50.

Pia. Wapinzani ambao ndio Kipaumbele chao wangekuwa wa kwanza Kuweka pembeni maVX ili kuonyesha wanamaanisha wanachokisema. Mtu anamiliki HAMMER, au Mtu anasema akiingia madarakani atauza Mashangingi wakati hata tunavyoongea nyumbani kwake amepaki hayo hayo mashangingi mtu huyo inatia shaka kumwamini.

Ni kweli Hao wabunge na watumishi wengi wa serikali wanatumia magari ya anasa saana. Kabla ya kukimbilia kuayauza waangalie ni mbadala gani ambao ni cost effective bila kucompromise Usalama in case kuna ajali, Ubora,Uwezo wake kwenye barabara zisizorafiki etc. Unakumbuka CASE ya NAPE NAUYE Kama ingekuwa ni NADIA au NOAH asingetoka mule.
Kwanini unaingiza uchama hapa, mleta hoja anazungumzia matumizi ya magari ya kifahari kwa viongozi wa serikali na kisiasa na wala hakusema viongozi wa CCM. Nakushangaa unapoingiza suala la viongozi wa vyama vya upinzani, kwani hii ni sera ambayo mleta hoja anaonelea ibadilishwa viongozi na watendaji wa serikali watumia magari ya bei rahisi na nafuu kwa gharama za uendeshaji.
Hatuwezi kufika popote kama kila jambo tukiliangalia kwa mtazamao wa kisiasa - tuyaangalie mambo kizalendo. Haijalishi ni nani akivurunda tunaoumia ni watanzania wote.
 
Haujaambiwa atumie pesa yake. ila asifuje pesa zisizo zake.
Upuuzi ni kutumia mali za umma kama hakuna kesho. wakati unaowatawala ni maskini wa kutupwa.
Mifano mliyopewa ya viongozi wanaotumia magari ya gharama nafuu relative to uchumi wao iwe chachu ya nyie kujitazama mlipo. sio mnataka kutimiza ndoto zenu za utotoni wakati mko vijijini kwa kutumia fedha za umma.

Kuhusu kutokutumia magari kwenda ofisini hilo sio tatizo, zipo nchi viongozi wanatumia baiskeli kwenda makazini, na uchumi wao uko juu kuliko wa kwetu.

Narudia tena, ni USHAMBA tu ndio unawageuza viongozi kuwa Pimps in the middle of poverty.
Huu hata siyo ushamba ndugu, ni umaskini wa akili au tunaita umaskini wa fikra.
 
Sikiliza wewe "nyau".Ngoja ifike mwaka 2020,gombea wewe urais,ukishinda tumia Toyo kwenye serikali yako. Go @Magufuri go,ulipo tupo!!
Badala ya kuwa positive ndio kwanza mnaponda, ili mtumie mashangingi toka masaki mpaka mjini?! Ulimbukeni gani huo? Uzuzu kabisa, wewe badala ya kufikiria kubana matumizi ndio kwanza wafikiri kutumia Limousine ?!
 
Badala ya kuwa positive ndio kwanza mnaponda, ili mtumie mashangingi toka masaki mpaka mjini?! Ulimbukeni gani huo? Uzuzu kabisa, wewe badala ya kufikiria kubana matumizi ndio kwanza wafikiri kutumia Limousine ?!
Wakati najificha kwenye vyoo vya kwenye train kutoka mwanza mpaka moro kisha kudandia magari ya magazeti from moro mpaka iringa,kisha kupiga mguu from iringa town to Tosamaganga jee ulinisaidia kwa lolote?acha ushamba boya wewe!!!
 
Back
Top Bottom