Mjadala: Magari ya viongozi wetu na dhana ya kubana matumizi

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
47,244
2,000
Kinacholeta shida wanasema wale siyo watumishi wa umma, lakini mbona wanatumia magari ya umma?
 
  • Thanks
Reactions: SDG

Konsciouz

JF-Expert Member
Aug 12, 2015
4,864
2,000
Serikali za kiafrika ni extravagant.
Wanaingia unnecessary expenses.
Mleta mada nakuunga mkono asilimia mia.
Kuna gari comfortable na AWD ambazo zina pita popote pale.
Njia mbaya isiwe kisingizio kwa hawa mabwana kutumia magari ya gharama kiasi hiki.
Na kupita sehemu mbaya ni uwezo wa dereva.
Barabara yaweza kua mbaya lakini mtu mwenye vitz akapita na yule mwenye shangingi akakwama.
 

okyoma

JF-Expert Member
Dec 17, 2013
268
250
Hizi Mkuu zinaweza kukatwa kinyemela kisha Wabunge wa MACCM kupenyezewa pembeni ili waendelee kulifanya Bunge kama kitengo cha MACCM. Kumbuka rushwa ya milioni 10 kwa kila mbunge wa MACCM mwezi October 2016.
Aliyezoea vya kunyonga vyakuchinja hawaviwezi, hawa ndugu zetu wengi wao ni wafanya biashara, kwa hiyo hawakwenda pale kutetea masilahi ya wananchi walienda mjengoni ili kufanikisha mipango yao ya biashara haramu, mfano hivi mbunge wa morogoro mjini alifuata nini bungeni, mchungaji lwakatale anatafuta nini bungeni kama tu muumini maskini ambaye hajui atakula nini kesho aliyetoka mbagara charambe au bunju analazimishwa kutoa kiwango cha chini elfu kumi ili aombewe aende mbinguni huku mama wa watu anamiliki mashule tanzania nzima, ana mahekalu mbezi beach na vingine.
Angalau naona wabunge wa upinzani angalau wanawakumbuka wananchi wao angalau kwa kupiga kelele.
 

Kimweri

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
3,999
2,000
Unasema Waziri/mbunge/kiongozi atumie gari lake kufanya kazi za umma? Toka lini au nchi gani viongozi wanatumia pesa zao kufanya kazi za umma. Kumpa mtu dhamana ya uongozi ni pamoja na kumpa vitendea kazi katika kufanikisha kazi zake ikiwa ni pamoja na gari, mwisho utasema na rais atumie gari lake kufanya kazi zake za kiraisi.

Kuna kitu unachanganya naona; kwa sasa kuna ulazima wakutumia magari kama lc200 sababu ya miundombinu ila hiyo haimaanishi miundombinu haiboreshwi. Barabara bado zinajengwa hasa highways ila wilayani na vijijini ndani bado barabara ni mbaya. Hata wakiacha kutumia hayo magari ili kukazia barabara zijengwa hazitajengwa ndani ya mwaka mmoja au miwili nchi nzima, na pesa za magari zenyewe ni peanuts kwa pesa zinazohitajika kujenga miundombinu. Nevertheless, reli(STG), barabara na infrastructure zingine bado zina boreshwa, until then haya magari yataendelea kutumika.

Kujiweka kimasikini sio kipimo cha uongozi bora.

Haujaambiwa atumie pesa yake. ila asifuje pesa zisizo zake.
Upuuzi ni kutumia mali za umma kama hakuna kesho. wakati unaowatawala ni maskini wa kutupwa.
Mifano mliyopewa ya viongozi wanaotumia magari ya gharama nafuu relative to uchumi wao iwe chachu ya nyie kujitazama mlipo. sio mnataka kutimiza ndoto zenu za utotoni wakati mko vijijini kwa kutumia fedha za umma.

Kuhusu kutokutumia magari kwenda ofisini hilo sio tatizo, zipo nchi viongozi wanatumia baiskeli kwenda makazini, na uchumi wao uko juu kuliko wa kwetu.

Narudia tena, ni USHAMBA tu ndio unawageuza viongozi kuwa Pimps in the middle of poverty.
 

enhe

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
2,084
2,000
Kikubwa na kinachosikitisha ni kwamba haya Mahari ni kama vile wanajinunulia wao..sababu yanapoharibika vitu vidogo tu huwa hayatengenezwi na yakitengenezwa basi ni kwa gharama kubwa sana kupitia michakato mirefu na yenye utatanishi...kubwa zaidi magari haya huuzwa bei ya chini sana kwa wao kwa wao eti kwa kisingizio kuwa yamekufa!
 

Kimweri

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
3,999
2,000
Unakumbuka kuna waziri alikataa kusafiri kwa ndege economy class akidai haina hadhi yake katika awamu ya nne na huyohuyo alisikika akisafiri kwa daraja hilohilo katika awamu ya tano

Anyway, shida iliyopo ni ubinafsi, mengi ya magari uliyosema yanatumika jijini ambako hata hizo VW zinapita bila shida

Ulimbukeni uliopitiliza.
Unajua siku zote maskini akipata huwa ni patashika. Mtu anataka miaka 30-40 ya kupigika kwenye umasikini aimalizie hasira zote kwenye miaka 5-10 ya uongozi wa umma.

huwezi justify kununua gari la milioni 200 wakati nchi masikini ya kutupwa na kuna wajawazito wanalala chini. fix your problems first then start the grandiose.
 

Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
6,500
2,000
Haujaambiwa atumie pesa yake. ila asifuje pesa zisizo zake.
Upuuzi ni kutumia mali za umma kama hakuna kesho. wakati unaowatawala ni maskini wa kutupwa.
Mifano mliyopewa ya viongozi wanaotumia magari ya gharama nafuu relative to uchumi wao iwe chachu ya nyie kujitazama mlipo. sio mnataka kutimiza ndoto zenu za utotoni wakati mko vijijini kwa kutumia fedha za umma.

Kuhusu kutokutumia magari kwenda ofisini hilo sio tatizo, zipo nchi viongozi wanatumia baiskeli kwenda makazini, na uchumi wao uko juu kuliko wa kwetu.

Narudia tena, ni USHAMBA tu ndio unawageuza viongozi kuwa Pimps in the middle of poverty.
Bado huzingatii Hali ya miundombinu ya TZ iliyopo. Wote tunatamani ingekua hivyo ila uhalisia unakataa. Nje wanatumia baiskeli kwenda kazini kama PM wa Netherlands sababu miundombinu inaruhusu wakati TZ bado. Matumizi ya haya magari haimaanishi jitihada za kuboresha miundombinu zimesimama, until then haya magari yataendelea kutumika.
 
  • Thanks
Reactions: SDG

Kimweri

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
3,999
2,000
Bado huzingatii Hali ya miundombinu ya TZ iliyopo. Wote tunatamani ingekua hivyo ila uhalisia unakataa. Nje wanatumia baiskeli kwenda kazini kama PM wa Netherlands sababu miundombinu inaruhusu wakati TZ bado. Matumizi ya haya magari haimaanishi jitihada za kuboresha miundombinu zimesimama, until then haya magari yataendelea kutumika.
Kinachomshinda waziri kutoka masaki hadi posta kwa baiskeli ni kitu gani? acha kuandika pumba.
 

Kimweri

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
3,999
2,000
Mkuu Umesahau na MAGOROFA aka MABUGANDO

Haswaa.., wewe unawajua haswa hawa ndugu zetu. kila sehemu tanzania ina udhaifu wake, tulichagua wa pwani tuliona udhaifu wake, huyu wa sasa naye ndio udhaifu wake huu.
 
  • Thanks
Reactions: Nzi

Nzi

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,027
2,000
Bado huzingatii Hali ya miundombinu ya TZ iliyopo. Wote tunatamani ingekua hivyo ila uhalisia unakataa. Nje wanatumia baiskeli kwenda kazini kama PM wa Netherlands sababu miundombinu inaruhusu wakati TZ bado. Matumizi ya haya magari haimaanishi jitihada za kuboresha miundombinu zimesimama, until then haya magari yataendelea kutumika.

Nipe justification ya Spika kutumia S class 500 ku-commute kati ya Uzunguni-Bungeni-Uzunguni. Au PM kutumia S class 500 au LC 200 ku-commute kati ya home and office. Ama VP kutumia GL class ya mwaka 2015 ku-commute home and office.

Kwani wakitumia VW Passat kuna shida gani kwa hizi home and office commuting?
 
  • Thanks
Reactions: SDG

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
12,155
2,000
Salaam,

Kama kichwa kinavyojieleza. Kumekuwa na mjadala wa miaka mingi juu ya aina ya magari ambayo viongozi wetu wa kiserikali wanayatumia kwa shughuli zao za kila siku.

Binafsi, nimekuwa nikisema mara kwa mara kwamba viongozi wetu wanaishi kama mastaa wa Hollywood kupitia migongo yetu walipa kodi.

Sasa baada ya kuona namna Rais mpya wa Ufaransa alivyo walk the talk, nikaona ni vyema tuendeleze huu mjadala. Angalia picha nilizoambatanisha hapa. Na pengine tuzidi kuishauri serikali ya Magufuli, ambayo inasisitiza katika dhana ya kubana matumizi.

View attachment 512594

Sina takwimu halisi ya namna gani magari ya viongozi yanaligharimu taifa, ila kwa kutumia uzoefu na common sense, ni rahisi kusema magari hayo yanaligharimu taifa pesa nyingi bila sababu za msingi.

Kuna ulazima gani wa Rais kutumia magari ya kifahari ya aina ya BMW? Katika msafara wake kuna BMW 7 series na BMW X5.
Kuna ulazima gani kwa VP kutumia Mercedes Benz GL Class? Kuna ulazima gani kwa PM na Spika kutumia Mercedes Benz S Class? Kuna ulazima gani kwa mawaziri, manaibu waziri, wakurugenzi, wakuu wa vyuo vya umma, wakuu wa polisi wa wilaya na mikoa, RCs, DC n.k. kutumia Land Cruisers 200 aidha VX au GX?

Hizi gari pamoja na bei ya kununua kuwa aghali, vilevile matunzo yake na utumiaji wa mafuta unaligharimu taifa fedha nyingi.

Kuna kipindi PM Pinda alitoa mwongozo juu ya aina ya magari kwa viongozi. Nakumbuka hadi Waziri Lukuvi akasema viongozi wataanza kutumia Suzuki Grand Vitara ama Toyota Rav4. Vilevile huyu bwana mkubwa wa sasa kwenye kampeni aliongelea juu ya haya magari ya viongozi. Ila bado mambo ni yale yale.

Kwanini inawawia vigumu kwa hawa viongozi kuamua kufanya angalau kama walivyojaribu Kenya kwa mawaziri kuanza kutumia VW Passat? Ingawa sijui kama utaratibu huo bado upo sasa. Hivi Rais akiendeshwa kwenye VW Passat kuna shida gani? Licha ya kujisifu kwamba serikali ya CCM imejenga mabarabara kila kona ya nchi, kwanini bado Land Cruisers zinatumika?

View attachment 512595

Kwa upana zaidi: hivi kuna ulazima wa viongozi wa serikali (pengine ukitoa wakuu wa mihimili ya dola) kupewa magari ya kutumia 24/7?

Ni hayo tu.
Umeshawahi kutafakari,ukiwa na Suzuki grande au hiyo RAV 4 unayoizungumzia,unaweza kwenda vijiji vingapi ambavyo barabara zake asilimia 80 ni rough roads,na mara ngapi ili hiyo gari angalau iweze kuishi miaka 5?Hizo gari kama Landcruiser V8 kiuhalisia ni gari ngumu sana,kwa hali ya barabara za vijijini ukipeleka gari kama Rav4,Suzuki,Xtrail,Klugger na gari za mtindo huo maisha yake yatakuwa mafupi sana.
 

Eminentia

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
2,468
2,000
ni hivi hizi gari mazingira zinapita mfano kuna jamaa angu huwa anapeleka watu wa serikalini vijijin huko kigoma sehemu ina matope gar yenye four wheel peke yake haipiti kwa hiyo haya ma rav4 hayawezi kwenda huko litakufa siku moja imagine cruiser 200 mkonge inapigwa gia arusha kigoma siku moja kesho yake ni matope tu barabara mbovu hatar hapo ndani ina watu saba hata 109 ikakwama sembuse rav4?? acheni tu watumie hizo gari
 

Lord Sauron

JF-Expert Member
May 4, 2017
224
250
Ni dhana nzima ya 'Ruling by Intimidation' Kwa dhana hii, kiongozi(soma mtawala kikwetu) lazima azungukwe na vitu vya ghali zaidi kuliko watawaliwa ndipo mtawala huyo aweze kuheshimiwa.
Kwa mfano, mkuu wa mkoa atawezaje kumtiisha raia kama gari ya ofisi yake ni Grand Vitara wakati ya huyo raia ni V 8?
Kwa hiyo magari ya gharama, makao ya kifahari, mavazi ya bei mbaya, wanawake warembo n.k ni nyenzo muhimu kwa watawala!
 

Kisu Cha Ngariba

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
22,152
2,000
Hap mkuu sio suala la kununua tu. Ukichukulia mfano ufaransa kila Rais ambaye amekuwepo amekuwa na choice ya gari gani (BRAND)atatumia kulinga na upenzi au ushabiki wakehapo ghalama haihusiki. KWa Rais lazima atumie gari secured mkuu bila kujali Ghalama. Maisha yake yanathamani kuliko Chombo anachotembelea kwa sababu anawakilisha watu zaidi ya mi 50.

Pia. Wapinzani ambao ndio Kipaumbele chao wangekuwa wa kwanza Kuweka pembeni maVX ili kuonyesha wanamaanisha wanachokisema. Mtu anamiliki HAMMER, au Mtu anasema akiingia madarakani atauza Mashangingi wakati hata tunavyoongea nyumbani kwake amepaki hayo hayo mashangingi mtu huyo inatia shaka kumwamini.

Ni kweli Hao wabunge na watumishi wengi wa serikali wanatumia magari ya anasa saana. Kabla ya kukimbilia kuayauza waangalie ni mbadala gani ambao ni cost effective bila kucompromise Usalama in case kuna ajali, Ubora,Uwezo wake kwenye barabara zisizorafiki etc. Unakumbuka CASE ya NAPE NAUYE Kama ingekuwa ni NADIA au NOAH asingetoka mule.

Kwahiyo hili suala linatakiwa kijadiliwa na upinzani?
 
  • Thanks
Reactions: SDG

ki2c

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
2,969
2,000
Mkuu hicho kichwa cha habari kimenikumbusha dereva wa mkurugenzi anayelala na gari la serikali tabata aamke nalo asubuhi kumchukua boss bunju ili ampeleke kazini posta.

Kwetu kuna mambo huwa sijui kwanini hayaingizwi kwenye vitabu vya Guiness.
Na mbaya zaidi wanatumia hayohayo magari yakuwabebea wakurugenzi au maafisa utumishi kuchukulia wake za watu au mademu za watu,inauma.
 
  • Thanks
Reactions: SDG

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,208
2,000
Kwahiyo hili suala linatakiwa kijadiliwa na upinzani?
Wapinzani wanajukumu la kuonyesha vile watakavyoishi ikitokea wametawala leo.
Sasa umesimama kwenye vx unawaambia watu nikiwa madarakani nitauza haya mavx yote watoto wapate mikopo ya Shule. Hili ni kuwadharau na kuwaona hamnazo wanaokusikiliza...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom