Mjadala: Magari ya viongozi wetu na dhana ya kubana matumizi

Salaam,Ni hayo tu.
Wenzako wala hawajali hiki, ndio kwanza wanafikiria kuongeza ndege nyingine ya kifahari! Kazi ipo sana, sana sana..Nilishawahi sema, nimeshuhudia hayo magari ya kifahari, VX6-VX8 yanapowashwa tangu asubuhi hayazimwi mpaka wakati dereva anapolala! Yaani hata kama gari imepaki ofisi au kwenye shughuli za mheshimiwa hakuna kuzimwa, kisa eti gari liwe na baridi ndani! Yaani jamaa wanaponda hela za mlipa kodi kama hawana akili nzuri..Sasa fikiria nimeona kama 2 au 3, je yako mangapi serikalini yanafanya hivi? Si mchezo hela zinavyochomwa moto..
 
Kama wanataka magari ya kwenda off road basi wanunue double cabin kama ford ranger, hillux, Isuzu kB, Mitsubishi Triton nk. Bei chini, running cost chini na zinafika kokote.
 
Najua kinga ni bora kuliko tiba. But, seriously kati ya Rais wa Ufaransa na wa Tanzania nani anayehitaji hilo secured car? Rais Magufuli anaogopa nini? Vipi kuhusu marais wa nchi kadhaa Ulaya ambao wanatumia tu public commuter trains?



Mimi naongelea kuhusu matumizi ya kodi na pesa za umma. Sijali kama kiongozi hata akinunua Maserati kwa pesa zake. Hiyo ni mipango yake, ili mradi tu pesa kazipata kihalali.


Naona una overplay umuhimu wa usalama hapa. Pengine ufafanue usalama gani unauongelea na una husika vipi na gari? Je, kwa Macron kutumia hiyo Peugeot Citroen DS ali-comprise usalama wake?
niongezee hapo vp kuhusu jose Mujika kama ni issue ya usalama?
 
Mkuu hicho kichwa cha habari kimenikumbusha dereva wa mkurugenzi anayelala na gari la serikali tabata aamke nalo asubuhi kumchukua boss bunju ili ampeleke kazini posta.

Kwetu kuna mambo huwa sijui kwanini hayaingizwi kwenye vitabu vya Guiness.
Na huyo mkurugenzi analo shangingi alilouziwa na serikali kwa bei che eti atalitumia kwenda kazini! Wakati fulani JPM akiwa waziri wa ujenzi alichachamaa na kujaribu kuthibiti matumizi mabaya ya magari ya umma. Amekuwa Rais, kwake hilo siyo tatizo tena. Sijui lini Watz watapata kiongozi anayewahurumia kwa dhati! Ni haki kweli kutoza nyumba ya mbavu za mbwa kodi ya majengo ili mkurugenzi anunuliwe na kutembelea shangingi? Badala ya kuimba Mungu Ibariki Tz tuanze kuomba AIOKOE!
 
Mkuu hicho kichwa cha habari kimenikumbusha dereva wa mkurugenzi anayelala na gari la serikali tabata aamke nalo asubuhi kumchukua boss bunju ili ampeleke kazini posta.

Kwetu kuna mambo huwa sijui kwanini hayaingizwi kwenye vitabu vya Guiness.
 
ki ukweli kwa hali ya barabara zetu haya ma VX na GX haya kwepekii kabisa...

Kwa hiyo umeona VX na GX tu kwenye hoja? Hujaona kuhusu hizo BMWs na Mercedes Benzs?

Sawa, kama kweli kuna haja ya kuwa na hizo shangingi, angalau ziwe kwenye mfumo wa government car pool. Hii ni kuzuia hii tabia ya viongozi kutumia magari ya umma 24/7. Gari zikiwa kwenye pool zita-control matumizi. Waziri anapewa mkopo wa gari la ubunge, halafu bado anapewa na gari ya bure ya serikali. Akienda jimboni hatumii gari yake ya ubunge, anatumia la bure la serikali. Anatumia gari hilo kupeleka watoto shule na nyumba ndogo saluni!

Kwa upande mwingine, kwanini hakuna msisitizo wa kujenga barabara za uhakika? Miaka 55 sasa, tunasema wimbo huo huo.

Lakini, VC wa chuo, mkurugenzi wa idara au katibu mkuu wa wizara anahitaji VX/GX ku-commute home and office? Yaani anakaa Masaki anafanya kazi Posta. Anahitaji hayo majini kweli?

Serikali ya CCM inajisifia kila siku kuhusu kujenga barabara za lami, kumbe inatudanganya eh?
 
Wacha Mkuu aburudike hayo mambo yanatokea mara moja kwa miaka kumi mimi ningeshauri atumie hata Limo aka The beast kama la Trump
 
Umeshawahi kutafakari,ukiwa na Suzuki grande au hiyo RAV 4 unayoizungumzia,unaweza kwenda vijiji vingapi ambavyo barabara zake asilimia 80 ni rough roads,na mara ngapi ili hiyo gari angalau iweze kuishi miaka 5?Hizo gari kama Landcruiser V8 kiuhalisia ni gari ngumu sana,kwa hali ya barabara za vijijini ukipeleka gari kama Rav4,Suzuki,Xtrail,Klugger na gari za mtindo huo maisha yake yatakuwa mafupi sana.
Kwenye hoja ndiyo umeona hilo tu?
Btw, nani sasa wa kulaumu kwa hizo barabara mbovu? Na suluhisho la barabara mbovu ndiyo kununua hayo mashangingi ama kutengeneza hizo barabara?

Kama yana ulazima sana, yawekwe kwenye mfumo wa pool. Yanakuwa wilayani. Kiongozi akiwa na safari za kikazi za umma anakodisha kutoka kwenye pool ili matumizi yake yaweze kuwa controlled. Akimaliza anarudisha gari kwenye pool, kisha arudi alipotoka kwa usafiri wa umma. Hivi, nini kinamshinda waziri kutoka Dar kwenda Dodoma kwa Shabiby? Yaani wanapenda starehe wakati nchi masikini hii!
 
Unakuta kijitu kimekaa kwenye dude kubwa kama chelewa ndani ya kikombe cha chai...kisa yeye ni mkuu wa taasisi au DC...gharama kubwa inatumika kuyaendesha hizo VX au GX halafu tunajiita taifa la kubana matumizi....na wabongo tulivyo na akili nzuri tunadhani ukiwa kwenye gari kubwa ndo uRC au uDC au ukuu wa taasisi unaonekana...ndo maana hata akipata ubunge au pesa anakimbilia kununua VX au GX watu wamwone...mi nashauri serikali iachane kabisa na hayo magari yanaitia nchi umaskini tunashindwa hata kupeleka pesa nusu ya bajeti kwenye mambo ya uzalishaji kama kilimo kwa sababu ya gharama za kununua na kuyaendesha mashangingi.
 
Nipe justification ya Spika kutumia S class 500 ku-commute kati ya Uzunguni-Bungeni-Uzunguni. Au PM kutumia S class 500 au LC 200 ku-commute kati ya home and office. Ama VP kutumia GL class ya mwaka 2015 ku-commute home and office.

Kwani wakitumia VW Passat kuna shida gani kwa hizi home and office commuting?
So basically unataka wawe na magari ya kutumia mjini na ya kutumia kwenda nayo vijijini sio. Sasa hapo wanasave au watatumia gharama zaidi
 
Hii ni Leo bado unataka watumie Passat!! Uhalisia unakataa hayo mawazo huo Ndo ukweli wenyewe ila haina maana kwamba barabara zenye viwango hazijengwi, hadi hapo haya magari yataendelea kutumika tu sababu biashara zingine Lazima ziendelee. Hatuwezi jibana kutumia Passat eti pesa tunayosave inajenga barabara itakua wendawazimu itamaanisha sehemu zingine kama hizi viongozi hawatafika hadi hizi barabara ziwe sawa na who knows inaweza kuwa 10yrs from now

Screenshot_20170522-154404%7E2.png
 
So basically unataka wawe na magari ya kutumia mjini na ya kutumia kwenda nayo vijijini sio. Sasa hapo wanasave au watatumia gharama zaidi
Kwa hiyo hizo 7 series, S class na GL class ndiyo wanayatumia kwenda nayo vijijini?

Unaelewa gari inapokuwa kwenye mfumo wa pool? Kama umesoma hoja yangu vizuri, utaona gharama za haya magari kubwa zipo kwenye matumizi na matengenezo yake. Unaweza kuwa na hata Yaris ya kiongozi kutumia katika kufanya home and office commuting. Kisha kuwa na Hardtop ya kwenda nayo off road kwa kukodisha kwenye car pool. Car pool inaendana na car sharing. Hivyo huhitaji kuwa na hardtop ya kila kiongozi kama kuna ziara ya pamoja.
 
Hii ni Leo bado unataka watumie Passat!! Uhalisia unakataa hayo mawazo huo Ndo ukweli wenyewe ila haina maana kwamba barabara zenye viwango hazijengwi, hadi hapo haya magari yataendelea kutumika tu sababu biashara zingine Lazima ziendelee. Hatuwezi jibana kutumia Passat eti pesa tunayosave inajenga barabara itakua wendawazimu itamaanisha sehemu zingine kama hizi viongozi hawatafika hadi hizi barabara ziwe sawa na who knows inaweza kuwa 10yrs from now

View attachment 512976
Braza ni aidha unajitoa ufahamu ama uwezo wako wa kuelewa ni mdogo. Mimi sijasema hizo Passat zitumike off road. Ebu usome na kuelewa basi mzee.

Nimekuuliza unipe justification ya Rais kutumia BMW 7 Series na BMW X5 kwenye entourage yake. Ukimaliza hilo unipe pia justification ya VP kutumia Mercedes Benz GL Class kwa home and office commuting. Kisha, unipe justification ya PM na Speaker kutumia Mercedes Benz S Class 500 kwa home and office commuting. Yaani kutoka Uzunguni hadi Bungeni, kiongozi wa nchi masikini anatumia S Class 500!! Kisha, unipe justification ya VC wa UDSM kutumia LC 200 kwa home and office commuting: kutoka Makongo Juu hadi Mlimani Campus. Sawa na VC wa UDOM, kutumia LC 200 kutoka Uzunguni hadi UDOM. Hadi sasa hujanijibu kuhusu haya, zaidi kujitungia mambo yako kama Bashite!
 
Hii ni Leo bado unataka watumie Passat!! Uhalisia unakataa hayo mawazo huo Ndo ukweli wenyewe ila haina maana kwamba barabara zenye viwango hazijengwi, hadi hapo haya magari yataendelea kutumika tu sababu biashara zingine Lazima ziendelee. Hatuwezi jibana kutumia Passat eti pesa tunayosave inajenga barabara itakua wendawazimu itamaanisha sehemu zingine kama hizi viongozi hawatafika hadi hizi barabara ziwe sawa na who knows inaweza kuwa 10yrs from now]
On the other hand, ulichoandika kinadhihirisha jinsi CCM isivyostahili kuendelea kuwa madarakani hata nusu saa! Haiwezekani miaka 55 ya uhuru, tuwe bado na barabara kama hizo. Sasa CCM imefanya jambo gani kwa asilimia 100 toka ishike madaraka?
 
Huyu Rais wa ufaransa anahitaji kupimwa akili umri wake miaka 39 kaoa mke miaka 66. Hata hivyo anastahili pongezi kwa kutangaza biashara ya magari yao na kufanikiwa kuwazuga wengine kwa muonekano wa gari analotumia eti ni la kawaida tu. Kwa hali ya kiusalama nchi kwake ilivyo wengine wameamini kioo cha gari hilo hata nchale unapenya.


Na washawasha!
 
kufanikiwa kuwazuga wengine kwa muonekano wa gari analotumia eti ni la kawaida tu!
Hata kama siyo la kawaida, Ufaransa wana deserve hiyo lixury kwani angalau wameshasahau kuhusu huduma mbaya za afya, elimu, barabara, maji, umeme n.k. miaka mingi iliyopita.

Sasa siye hata Dar bado huduma hizo zipo saghalabaghala, halafu unataka viongozi wa-stunt kama Hollywood celebs?
 
mim ndio nikiwa rais uo mwaka 2025,wabunge wote watapanda BUS aina ya YUTONG,Kanda ya ziwa bus 2,kanda ya kati bus 2,nyanda za juu bus 2 na kwingineko pia bus 2 WAJAZANE UMO UMO HADI DODOMA....ni mwendo wa bus tuuu hakuna cha BMW
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom