MJADALA: Kwanini Wanawake wanaongoza kuwa na majini/mapepo kwa kasi kuliko Wanaume?

Teamo

JF-Expert Member
Jan 9, 2009
12,272
1,035
MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU:

Salaam wakuu wangu!

It's been long time since i posted a thread herein lakini haina mbaya kiviile manake makamanda mnawakilisha kama ilivyo ada!

STRAIGHT TO THE TOPIC:

Nimeangalia sana kwa uchunguzi wangu wa muda mrefu nikagundua kuwa:


1) Asilimia kubwa sana ya wanawake wanaandamwa na majini/mashetani/mizimu/mapepo....! Hii nimeifuatilia sana kuanzia makanisani, misikitini, hadi uraiani kwenye maisha ya kawaida ya kiswazi.

2) Wanawake ndo watu pekee wenye hofu ya mwenyezi Mungu..(makanisani wamejaa wao, misikitini, mikutano ya injili, jumuiya ndogondogo n.k)


Sasa mi nashindwa kuelewa wala kuziunganisha hizo hoja mbili hapo juu..

Mnisaidie wakuu!

ANGALIZO: Sina nia yoyote ya kuwa-humiliate wanawake


=====
BAADHI YA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU:

===
===
===
===
 
Naomba nijaribu, (kama nakosea au kuwakwaza watu natanguliza kuomba msamaha!)

Shetani
anatumia udhaifu mwanamke tokea kuumbwa kwake! Nathibitisha; Kwanza naomba tuwe na Biblia kwenye majibu yangu. Tusome Mwanzo 2:18,12; Mwanamke aliletwa ili awe msaidizi(company) kwa mwanaume(koz ya kuwa weak no.1). Soma Mwanzo 3:1-6,13 Hapa inaonyesha, nyoka(ibilisi) anajua mwanamke ni dhaifu na hajiamini hivyo ndo alikuwa wa kwanza kufanikiwa kumdanganya!(weakness no.2), bado Soma Mwanzo3:15 kuwekwa uadui kati ya nyoka(ibilisi) na mwanamke (koz no3) Soma Mwanzo 3:16 haswa sehemu b, ananyimwa utawala so weakened even the more! (koz no.4).

Tuhame hapo, twende Mwanzo 6:1-3;' Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,wana wa Mungu waliwaona hao binti wa wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. BWANA Mungu akasema Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele!.............'

Hapa inaonyesha Mungu alichukizwa na mchanganyo huu maana watu wake(wenye maadili na kufuata sheria zake) wanaingia kwa mabinti wa wanadamu(wasiokuwa na hofu ya Mungu, hivyo ulinzi hawana kwa kufuata mila a matambiko yao, hivyo ni wazi wana mapepo) kwani huko mbele inaonyesha jinsi walivomuasi Mungu hata akakifutilia mbali kizazi hicho kwa gharika kasoro Nuhu tu na wanawe.

Hapa naonyesha shetani alipitia kwa watoto wa kike wa wanadamu. (Soma Kumbu 7:3,4 wanavyokatazwa kujichanganya. na sababu zake). Kwa kifupi ; kwa vile wanawake kwa ujumla wao hawana confidence hasa katika kumiliki, wamejikuta wanaingia mikataba mingi(kwa hiyari au kuingizwa aidha kwa kulazimishwa/ kulazimika ama wakiwa bado wadogo na wazazi wao na haswa wa kike awe mama,bibi, shangazi, nyakanga n.k) au yeye mwenyewe kwa kutaka kumiliki say mume, nyumba, utawala n.k) na yule muovu shetani!

Ikumbukwe kuwa Ibilisi amewekewa uadui na mwanamke, hivyo kila siku yuko bize kutaka kumuingia mwanamke, sasa anapojipeleka mwenyewe ili apate utawala, shetani anamuingia 'in four' tena mbaya zaidi anapitiliza mpaka ktk uzao wake.

Nijibu kuhusu wazungu au kwa ujumla walioendelea na wasomi, kwa kifupi hawa wengi wameachana na mila potofu, hivyo hawajiingizi kwenye mikataba hii, lakini akijiingiza tu shetani anaye haijalishi msomi, mzungu,wala mhindi, si tunawaona!

Kwa leo naishia hapa, narudia kama nimewakwaza wengine, naomba msamaha, lakini kama umeinuliwa nakukaribisha tukate huo mnyororo wa laana kwa ajili ya watoto wako wa kike! Kuna mkataba mwingine ni wa damu, hii somo lake siku nyingin.
 
Naangalia kipindi cha utakaso kwenye Emmanuel TV (monday service ya (T.B Joshua).

Kwa mtazamo wangu naona idadi kubwa ya viumbe wanaosumbuliwa na mapepo ni kina mama na mabinti. Sijui kwanini inakuwa hivi?

Wenye ufahamu tafadhali!
 
Huko Nigeria umeenda mbali sana mkuu, huwa nawaangalia 'mtume' na nabii' Mwingira, yaana asilimia kubwa ya wanaokutwa na mapepo ni kina dada na mama, huwa nashindwa kabisa na kituko huwa pale 'anapoamurisha' mpepo yatoke na watu kuanguka, wanaume wengi huwa hawaanguki ukilinganisha na kina mama na dada.

Inanichanganya sana lakini mwisho wa siku, ni fumbo la imani
 
Bado jibu langu halitakuwa tofauti lakini naomba kwanza kukuondolea shaka juu ya kubaki kwa fumbo la Imani.

Kila mtu awe dada au kaka kama ana pepo mara nyingi huanguka chini,kisha pepo humtoka. Swala la wadada wengi kuanguka ni kwa sababu wanatumia vitu vingi vya mapepo.

Mfano mzuri sana ni pafyum kali sana lakini pia nguo nyingi wanazovaa zina mvuto kwa majini-referring to Wanajimu watakueleza.
 
Naangalia kipindi cha utakaso kwenye Emmanuel TV (monday service ya (T.B Joshua).kwa mtazamo wangu naona idadi kubwa ya viumbe wanaosumbuliwa na mapepo ni kina mama na mabinti. Sijui kwa nini inakuwa hivi? Wenye ufahamu tafadhali!

Kwa kuongezea swali lako, mimi kwa Tanzania, sijawahi kuona watu waliotoka kwenye familia zenye kipato kizuri, wakiwa na mapepo/mashetani. Wote nilioshuhudia, wanatoka katika familia fulani ambazo zipo duni ama kwenye kipato au kwenye elimu. Sijui kama wengine wameona hivi.

Halafu dalili nyingi za watu wenye mapepo/mashetani zinafanana sana na psychiatric disorder inayoitwa "Dissociative Identity disorder-DID" au zamani ikiitwa "multiple personality disorder MPD".

Disorder hii kwa nchi za wenzetu, huwapata baadhi ya waliokuwa abused utotoni. Tiba zake ni Psychological treatment including hypnosis. Basically hata tiba ya imani (kwa maoni yangu) ni psychological treatment. Inawezekana pia wanawake wa kiafrika TZ ikiwemo, wengi wao kutoka kwenye familia duni have been abused in one way or another ambayo ndio inapelekea DID. Ila kwa vile tunaamini sana ushirikina katika jamii zetu, sisi tunaona ni mapepo.

Kwa shule zaidi kuhusu DID/MPD, get it from google.com.
 
wewe ni atheists sio?
huwezi elewa haya....
eti stuka,huachi kabisa naona ..

Boss hebu kuwa muwazi hueleweki

Wanawake wengi wanapata hysteria na kwa sie tusojua sayansi husika tunafikiri mapepo.

Hiyo ya wanawake wote wanavutia mapepo ndo naipata kwako......nieleweshe :]
 
Boss hebu kuwa muwazi hueleweki

Wanawake wengi wanapata hysteria na kwa sie tusojua sayansi husika tunafikiri mapepo.

Hiyo ya wanawake wote wanavutia mapepo ndo naipata kwako......nieleweshe :]

nilicho ongea ni according to 'some religious teachings'
ndo maana nikakuuliza wewe ni atheist?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…