Mjadala: Kwanini shule za Kiislamu hazifanyi vizuri kwenye matokeo ya Mitihani

Mimi Muislam, sisi tuna matatizo kwenye taaisisi zetu tu ni majanga, kwenye misikiti tu majanga sasa utegemee shule zetu zifanye vizuri? wenzetu kuna nidhamu kubwa sana hata kama wametofautiana ila wana hali ya kuweka mambo sawa ndani na wanaheshimu viongozi wao na ukitaka kungalia hilo nenda shule za kiislamu na nenda shule za dini nyingine halafu angalia nidhamu na heshima za watoto utapata jibu.
 
Umemaliza kila kitu mkuu, elimu na maisha kwa ujumla vinataka nidhamu sana na umoja, na ata ukiona kwa Muslim waliondelea yani matajiri wako tofauti sana na Muslim wa hari za kati, wenye mafanikio Wana nidhamu sana na umoja ila wakina sisi nidhamu hakuna na ubinafsi umetujaa
 
Naongezea.

Nina ndugu yangu anafundisha shule ya islamic ya primary ukweli jamaa ana elimu kubwa tu.Hizo shule ziko mbili maneo tofauti

Mwaka 2013 alipelekwa kwenye shule moja wapo ili ainue iwe ya kisasa ,akaenda huko akawa mkuu wa shule ndani ya ile shule ina msikitini na kuna wazee wa msikiti,basi jamaa baada ya kufika akapiga sana kazi shule ikaanza kuinuka ikawa na wanafunzi wengi aliweka mikakati mingi sana.Wale wazee wa msikiti kwa kua walikua na watoto wao pale walimu tu wa kawaida wakaanza kuleta wivu na chuki basi wakafanya visa vingi mpaka kufika 2015 jamaa akashindwa,mbaya zaidi walimu wa pale walikua hawana elimu yoyote wanaunga unga tu.Shule ilikua english medium ila mwalimu kuzungumza kiingereza fasaha sentesi hata mbili ilikua shida tupu.

Jamaa akahamishwa kule akpelekwa shule nyingine huko nako hivyo hivyo wanaokotana tu walimu vilaza hakuna wanachojua hata hiyo dini tu nayo wanaunga unga..kiufupi taasisi hizi zina ukiritimba sana hakuna management nzuri kuna ukiritimba sana.
Hili nalikubali sana, yaani ni shaghalabagala.
 
Pitia kwenye academy zao utaelewa. Mambo ya dini ni mengi sana.

Nina jirani yangu mwanae alikua hwezi kusoma yupo miaka 6 anataka kuanza standard one hajui kusoma wakamkataa shuleni. nikamwambia Mwanao mfute huko madrassa asome kwanza shule za kawaida. Maana haiwezekani mtoto mdogo afundishwe Arif, Be .... alaf afundishwe ABC aelewe. Mwaka huu mtoto ameweza kusoma na kuandika ameanza Darasa la kwanza

Mambo ya dini yana nafasi kubwa kwenye maisha, lakini kwa upande wa kiislam inahitaji nguvu ya ziada mtoto ku master.

Inafika kipindi Dini inanoga hadi watoto wanaambiwa Hiyo elimu ya Makafiri haifai na propaganda nyingine
Labda ni maajaaliwa na jitihada za wazazi, ni hivi hapa jirani kuna dogo kahifadhi kichwani msahafu wote anatema aya si mcjezo na shuleni pia yuko vyema sana, ni form five kwa sasa na anachukua mchepuo wa sayansi.
Huyu utasemaje, na wako wengi sana kaka, anasoma madrasa lakini shule pia mtu anakywa yuko vyema sana.
 
Misingi ya dini ni Jambo kubwa linalopelekea utofauti huu

Kinachofanya baadhi ya shule kufanya vizuri ni kuchagua wanafunzi wachache ambao wana uwezo mkubwa kiakili. Ona shule ya St Francis, wale wote walikuwa ni wanafunzi waliochujwa na wakabaki na wachache wenye uwezo wa juu ili kukuza reputation ya shule. Mbinu hii inafanywa na shule nyingi unazoziona Leo hii ziko top na shule nyingi za kikristo ndio Zina huo mtindo.

Kwa shule za kiislamu Jambo hilo Kama lipo Basi ni kwa kiasi kidogo, shule hizi haziwezi kukataa mwanafunzi eti kwa sababu anauwezo mdogo darasani. Niwe mkweli tu kuwa katika uislamu jambo la kumtenga mtu kwa sababu ya uwezo wake halipo. Jitihada ni kubwa zinafanywa na shule hizi za kiislamu lakin kundi wanalodeal nalo ni kubwa ona shule Kama kilinjiko na namba ya wanafunzi walionao, Kama wangewachuja wangekuwa na matokeo mazuri zaidi ya yale.

Huwenda kweli sababu zilizotajwa na watu wengine zikawa na ukweli lakini hii ya kutowabagua watu Mimi naona ina mashiko na ni evident in almost all Islamic schools.

After all lengo kuu la elimu hasa katika dini ya kiislamu si ku-appear katika shule zilizofanya vizuri. Lengo kuu la elimu ni kumpa mwanafunzi ujuzi na maarifa yatakayomsaidia mwanafunzi kuishi kulingana na mazingira aliyopo. Kwangu mimi Kama msomi huu ushindani ulioko saivi unadumisha elimu yetu kwani shule nyingi zinashindana kufanya vizuri na baadhi ya shule zinahiari kutumia hata njia haramu, ili tu ufaulu wao ukue na watangaze jina la shule na mwisho wa siku wafanye biashara zao.
Shule zetu zinabidi zishindane kupata shule ipi inawaandaa wanafunzi kujitegemea hasa katika kipindi hiki ambacho elimu imeonekana haina Tena thamani.
 
Pitia kwenye academy zao utaelewa. Mambo ya dini ni mengi sana.

Nina jirani yangu mwanae alikua hwezi kusoma yupo miaka 6 anataka kuanza standard one hajui kusoma wakamkataa shuleni. nikamwambia Mwanao mfute huko madrassa asome kwanza shule za kawaida. Maana haiwezekani mtoto mdogo afundishwe Arif, Be .... alaf afundishwe ABC aelewe. Mwaka huu mtoto ameweza kusoma na kuandika ameanza Darasa la kwanza

Mambo ya dini yana nafasi kubwa kwenye maisha, lakini kwa upande wa kiislam inahitaji nguvu ya ziada mtoto ku master.

Inafika kipindi Dini inanoga hadi watoto wanaambiwa Hiyo elimu ya Makafiri haifai na propaganda nyingine
Mkuu tatizo sio dini tatizo ni mikakati ya hao wazazi na watoto wao.

Nina mdogo wangu yeye anasoma dini na dunia tena ni shule ya kata huko vijijini lakini matokeo haya ya form two kapata Div One ya point 11 licha ya kuwa anasoma na dini pia.

Huo ni mfano kwamba madrasa sio ishu kivile ya kwamba mtoto asijue kusoma,tatizo ni wazazi wa kiislamu wenyewe wanashindwa wafanye vipi.

Mimi nilimuwekea mikakati dogo kwanza nikamuambia kuwa usipojiangalia utajikuta husomi dini wala dunia huisomi akaniuliza kivipi ? Nikamuambia ukiwnda madrasa ukawa unapiga dufu tu muda wote ili ukacheze maulidi hapo dini hujaisoma umesoma dufu tu na huo muda umepoteza kuisoma dunia yako.

Kwa hyo dogo wangu mimi habari ya kupoteza muda kwenda madrasa kupiga dufu hana,yeye anaenda kusoma mambo muhimu na mengine namfundisha mwenyewe,hii inamfanya awe na muda wa kutosha kusoma dini.

Na mengine mengi yanachangia ikiwemo kutokuwa na malengo kwa watoto,na watoto wanatakiwa wafundishwe vipi wawe na malengo na zipi ni faida zake,imagine huyu dogo wangu yuko form three kaingia mwaka huu anajua yeye anataka kuja kuwa nani na yale masomo ambayo yanahusiana na ndoto zake kafaulu vizuri sana kwa hiyo anafahamu vizuri nini anatafuta katika maisha yake.

Tatizo hao wazazi na mikakati mibovu.

Mzazi eti anakubali mtoto wake kwa wiki apige dufu siku nne madrasa na kila siku inachukua masaa matatu hivyo siku nne masaa 12 sawa na nusu siku mtoto anapiga dufu,huu muda angetumia kusoma dunia angepandisha ufaulu
 
kweli kabisa
 
Naomba uzi uwe safi, udini usiingie humu, nazungumzia shule za kiislam sio dini ya kiislamu, maana huko kweny shule hata walimu wakristo wapo, ila huwezi kumkuta mkristo kwenye dini ya Kiislamu.

Karibuni walimu mnaofundisha huko, wazoefu kt kuendesha shule, na wadau wote, Kwanini shule za kiislamu hatuzioni top ten kitaifa??

Feza Boys na Feza Girls hazipo? hizi zinaendeshwa na Uturuki(Waislamu Wazungu Turkey) Ebu fuatilia na kama zinafanya vema basi kwa shuke zao nyingine tatizo litakuwa ni UONGOZI na siyo dini!!!!Period.
 
Asubuhi anafundishwa kuandika kutoka kushoto kwenda kulia, jioni anafundishwa kutoka kulia kwenda kushoto.. Unafikiri kuna kitakachoeleweka hapo?
 
Back
Top Bottom