Mjadala: Kwanini shule za Kiislamu hazifanyi vizuri kwenye matokeo ya Mitihani

kombaME

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
2,115
2,807
Naomba uzi uwe safi, udini usiingie humu, nazungumzia shule za kiislam sio dini ya kiislamu, maana huko kweny shule hata walimu wakristo wapo, ila huwezi kumkuta mkristo kwenye dini ya Kiislamu.

Karibuni walimu mnaofundisha huko, wazoefu kt kuendesha shule, na wadau wote, Kwanini shule za kiislamu hatuzioni top ten kitaifa??
 
Kuna shule pia zina mfumo madhubuti wa kusolve mitihani ya NECTA siku kadhaa kabla ya mitihani. Mitihani inabadilishwa kidogo lakini ikija yenyewe ndio ileile. Sijui wanaipata wapi lakini ndio hivyo. Chanzo cha hii habari ni binti ya rafiki yangu alipata one kwenye shule moja
 
Hao wanasomea MTIHANI.
Kila jioni wanafanya mitihani iliyokwisha yaani ya miaka ya nyuma.
Lakini mishule ya serikali mnnakaa mnajazana MINOTES kibao.
Mpaka KUSOMA unaona kero..
Wenzetu wanafaulu sababu kuanzia mwezi wa kwanza mpaka mwezi wa mtihani wa taifa wao wanacheza na past papers tu.
Kuna shule pia zina mfumo madhubuti wa kusolve mitihani ya NECTA siku kadhaa kabla ya mitihani. Mitihani inabadilishwa kidogo lakini ikija yenyewe ndio ileile. Sijui wanaipata wapi lakini ndio hivyo. Chanzo cha hii habari ni binti ya rafiki yangu alipata one kwenye shule moja
 
Ila maisha yanachanganya, matokeo yakitoka km hv kuna kundi hulaumiwa kwa kufeli muda ukipita tunasahau, Lakini tena ikitokea habari ya graduate dereva wa bajaji au vile graduates wanavyogombea posts 20 za utumishi wakati wapo wapo 2000. Tutaanza tena kulaaumu "ooh kusoma sio ishu bora uende veta"
F*ck
 
Naongezea.

Nina ndugu yangu anafundisha shule ya islamic ya primary ukweli jamaa ana elimu kubwa tu.Hizo shule ziko mbili maneo tofauti

Mwaka 2013 alipelekwa kwenye shule moja wapo ili ainue iwe ya kisasa ,akaenda huko akawa mkuu wa shule ndani ya ile shule ina msikitini na kuna wazee wa msikiti,basi jamaa baada ya kufika akapiga sana kazi shule ikaanza kuinuka ikawa na wanafunzi wengi aliweka mikakati mingi sana.Wale wazee wa msikiti kwa kua walikua na watoto wao pale walimu tu wa kawaida wakaanza kuleta wivu na chuki basi wakafanya visa vingi mpaka kufika 2015 jamaa akashindwa,mbaya zaidi walimu wa pale walikua hawana elimu yoyote wanaunga unga tu.Shule ilikua english medium ila mwalimu kuzungumza kiingereza fasaha sentesi hata mbili ilikua shida tupu.

Jamaa akahamishwa kule akpelekwa shule nyingine huko nako hivyo hivyo wanaokotana tu walimu vilaza hakuna wanachojua hata hiyo dini tu nayo wanaunga unga..kiufupi taasisi hizi zina ukiritimba sana hakuna management nzuri kuna ukiritimba sana.
Kwa sababu ni chache. Hata zile nyingine za private Ni za waislam ila zimeandikwa majina ya private. Lakini pia udini unaingia, wana-base zaidi kwenye mafumdisho ya dini Na wanapendelea wanatumia zaidi walimu Wa waislam
 
Elimu Dunia 20%
Elimu Akhera 80%
Ila kwa hili si kweli mkuu. Waislamu wa Tanzania ni wakawaida sana si wa ile misimamo mikali kiviile. Ukifanya utafiti utagundua wengi ni waislam majina tu. Ukienda misikitini ukiondoa siku za ijumaa utakuta msikiti una watu watatu tu. Hata hiyo Ijumaa yenyewe watu hawaendi. Kuna sababu nyingine tu ambazo huwa hazitajwi
 
Pitia kwenye academy zao utaelewa. Mambo ya dini ni mengi sana.

Nina jirani yangu mwanae alikua hwezi kusoma yupo miaka 6 anataka kuanza standard one hajui kusoma wakamkataa shuleni. nikamwambia Mwanao mfute huko madrassa asome kwanza shule za kawaida. Maana haiwezekani mtoto mdogo afundishwe Arif, Be .... alaf afundishwe ABC aelewe. Mwaka huu mtoto ameweza kusoma na kuandika ameanza Darasa la kwanza

Mambo ya dini yana nafasi kubwa kwenye maisha, lakini kwa upande wa kiislam inahitaji nguvu ya ziada mtoto ku master.

Inafika kipindi Dini inanoga hadi watoto wanaambiwa Hiyo elimu ya Makafiri haifai na propaganda nyingine
 
wengi walioshikilia mifumo wana elimu hasa ya dini na ndio wenye maamuzi makubwa kwenye hizi shule ila ukija academically hawapo vizuri hivyo bas kuna uwezakano wa kushindwa kuweka mikakati mizuri ya uendeshaji na malengo ya ufaulu kwenye hizi shule.
 
Pitia kwenye academy zao utaelewa. Mambo ya dini ni mengi sana.

Nina jirani yangu mwanae alikua hwezi kusoma yupo miaka 6 anataka kuanza standard one hajui kusoma wakamkataa shuleni. nikamwambia Mwanao mfute huko madrassa asome kwanza shule za kawaida. Maana haiwezekani mtoto mdogo afundishwe Arif, Be .... alaf afundishwe ABC aelewe. Mwaka huu mtoto ameweza kusoma na kuandika ameanza Darasa la kwanza

Mambo ya dini yana nafasi kubwa kwenye maisha, lakini kwa upande wa kiislam inahitaji nguvu ya ziada mtoto ku master.

Inafika kipindi Dini inanoga hadi watoto wanaambiwa Hiyo elimu ya Makafiri haifai na propaganda nyingine
Kuna tafiti za kisayansi zinaonesha mtoto alisoma quran ni rahisi zaidi ku master stadi za KKK kwenye hii elimu ya kawaida. Hii nakuachia ukipata muda waweza hata ku gugo tu
 
Ila kwa hili si kweli mkuu. Waislamu wa Tanzania ni wakawaida sana si wa ile misimamo mikali kiviile. Ukifanya utafiti utagundua wengi ni waislam majina tu. Ukienda misikitini ukiondoa siku za ijumaa utakuta msikiti una watu watatu tu. Hata hiyo Ijumaa yenyewe watu hawaendi. Kuna sababu nyingine tu ambazo huwa hazitajwi
Mkuu jamaa anachosema kiko sahihi kabisa, kwa mtaani ulichosema wewe uko sahihi, kwa mtaani waislam hawafati sana misingi ya imani yao ila wanachokosea ni kwenye hizo shule za kiislamu kuweka mkazo kwenye mashart ya imani

Kwanza ajira wanatoa kwa kuangalia dini na sio ubora wa mwalimu, mtoto anatakiwa kusali alfajiri, mchana, jioni, usiku, lakini pia kuna shule wanafundisha hadi karate, in short kuna misingi mingi ya elimu wanaikosea, na ukikuta shule ya kiislamu inafanya vizuri ujue kuna vitu wao wamevipuuzia, sa unakuta mtoto anaenda kujua zaidi dini kuliko elimu iliyompeleka hapo
 
Kuna tafiti za kisayansi zinaonesha mtoto alisoma quran ni rahisi zaidi ku master stadi za KKK kwenye hii elimu ya kawaida. Hii nakuachia ukipata muda waweza hata ku gugo tu
Unachosema ni kweli wala sio uongo, maana kiarabu ni kigumu sana kukalili hivo ukikuta mtoto anaweza kucrame quran hawezi shindwa kukalili biology ila tatizo linakuja pale ambapo umuhimu unahamia kwenye quran tu na sio masomo mengine na kuyapuuza, unakuta walimu, mzazi na ata mtoto anafurahi zaidi kwa mtoto wake kujua quran na sio kilichompeleka

na tuache unafki ukikuta Muslim kakorea kwenye dini anakuwa mkorofi, kiburi, dharau ila tunasahau elimu au maisha yanataka discipline kwa watu wote, hivo kama ni wanafunzi unatakiwa kuwa na discipline kwa wanafunzi wenzio, walimu, wafanyakazi wote kwa ujumla

Kwa shule za seminali iko tofauti sana, Kwanza zina wastani mkubwa na watoto wanasoma sana elimu ya darasani kuliko ukristo, ila hizi shule zinazingatia sana nidhamu, kufukuzwa shule kisa umeiba chungwa ni kufkia tu, kisa umemtukana mwenzio, umemtukana mfanya usafi au mmepigana, umekutwa hostel muda muda wa kusali au prep, in short ukikuta mtu kakorea ukristo basi inakuwa vice versa ya Muslim, atakuwa mpole na nidhamu itakuwa iko juu sana na moto ya hizi shule waga mara nyingi ni "study hard pray hard"
 
Pitia kwenye academy zao utaelewa. Mambo ya dini ni mengi sana.

Nina jirani yangu mwanae alikua hwezi kusoma yupo miaka 6 anataka kuanza standard one hajui kusoma wakamkataa shuleni. nikamwambia Mwanao mfute huko madrassa asome kwanza shule za kawaida. Maana haiwezekani mtoto mdogo afundishwe Arif, Be .... alaf afundishwe ABC aelewe. Mwaka huu mtoto ameweza kusoma na kuandika ameanza Darasa la kwanza

Mambo ya dini yana nafasi kubwa kwenye maisha, lakini kwa upande wa kiislam inahitaji nguvu ya ziada mtoto ku master.

Inafika kipindi Dini inanoga hadi watoto wanaambiwa Hiyo elimu ya Makafiri haifai na propaganda nyingine
Jibu lako halina uhusiano na mada husika. Binafsi nimesoma madrasa na shuleni nilikua nafanya vizuri kawaida. Hivyo huyo aliyetoa mawazo hayo sio kwamba hilo ndio tatizo la mtoto. Issue ni mtoto hakua sharp katika kuelewa masomo on his early days. I had a friend ambae alikua ni Christian utotoni mwake alikua na kichwa kigumu kweli mpaka darasa la nne ndio akaanza kujua kusoma vizuri hii nayo utaihusisha na madrasa.

Changamoto ya shule za kiislam ni kutotafuta walimu wazuri wa kufundisha wanafunzi wao. Pia budget zao sio kubwa kiasi hicho kuna haja ya kuboresha mazingira ya shule zao. Na kuanza kuchaji ada itakayoweza kupata walimu wazuri wa kufundisha ila kwa hizi peanuts fees hawawezi pata walimu wazuri na vifaa bora kwa ajili ya wanafunzi wao. Kwa maana hata kama ni suala la dini sio kigezo cha wao kufeli issue ni kutokua mazingira mazuri ya kusoma.

Budget Budget Budget
 
Na hili ndio moja kati ya majibu sahihi ya hizi shule kufanya vibaya. Wanaosema eti msisitizo uko kwenye elimu akhera wamekariri tu kwa sababu ingekua hivyo effect yake tungeiona vijana wanapokuja mtaani. Labda nachoweza kukubali ni zile Inshallah Inshallah nyingi, anakuja mzazi hana ada anakubaliwa kirahisi Inshallah ishallah
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom