MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 12,695
- 31,480
Ni nyege tu, nyege zinaleta ujasiri sana
Nipe mstari unaosema Maria alipaa kwenda mbinguni.Biblia inasema Bikra Maria ataitwa mbarikiwa, na dunia itamsifu kuwa yeye ni mbarikiwa. Bikra Maria kwa mujibu wa kumbukumbu za kanisha hakufa, alipaazwa. Ujui historia, huyu mama ni the special, hata waprotestant wakimtupa sisi Wakatoliki tutaendelea kutimiza unabii kwa kumuita mbarikiwa
Padre Luther alikuwa miongoni mwa Mapdre wenye karama nyingi ndani ya Kanisa Katoliki wakati wake, yeye alikuwa na Madai mengi sana juu ya mapungufu kwa kanisa. Hata hivyo madai yake mengi hayakuwa na msingi wowote.
Moja ya madai yake ilikuwa ni kuondoa kibali cha kwamba baada ya kuungama muumini asipewe stakabadhi ya kuonesha ameungama kwa kuwa kitubio ni siri ya mtu. Hili lilifanyiwa kazi. Mengine ikiwemo kurekebisha mfumo wa sala ya Kanuni ya Imani. Na mambo mengine mengi ambayo alipojibiwa, yeye hakuridhika pamoja na kueleweshwa vya kutosha. Alikuwa ni Great Thinker sana.
Mbaya zaidi alipokuja kusababisha mpaka akajitenga na kanisa ni kitendo cha kuondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia ikiwemo pia kupunguza baadhi ya mistari kwenye vitabu kama cha Esta na cha Danieli.
Aliondoa vitabu vya Deutrokanoni na vingine baadhi na kuwa jumla ya vitabu 7 vilivyotolewa kwenye Biblia. Na kila kitabu alikuwa na sababu yake aliyoibainisha. Kimsingi alipata wafuasi wengi wa kumuunga mkono hoja yake hasa wale ambao walikuwa wanatafuta njia ya kuchuma pesa kiulaini. Na hapo Biblia mpya ilianza yenye Vitabu pungufu.
Na ndio maana leo watu hawaujui Ukristo vizuri na wanakinzana bila kujua historia ya kanisa. Watumishi wengi wa Mungu hasa hawa wa kileo wasiojua historia vizuri wao kila kitu wanapinga. Sio kosa lao Bali ni kosa la kutokujua historia ya kanisa.
Matumizi ya Ubani yalipingwa sana, na hapa ilikuwa ni kuondoa idadi ya waelewa. Kutokana na watu wengi walikuwa wamegeuka kama waganga kila mapepo ya kiwakabili walitumia ubani kuyafukuza na yalikimbia, lakini watu walijisahau kusali na kuomba na hata kufika ibadani ikawa nadra maana wanajua kujiponya kuondokana na majini na wachawi. Hapa Padre Luther na wenzake wakapiga marufuku matumizi ya ubani na kuwa sihi wakazanie Neno zaidi.
Hapa walichotakiwa kufanya ni kuliishi Neno la Mungu na wakati wa ibada basi ubani uchomwe kama Mungu alivyo agiza.
Luther na wenzake lengo lao lilikuwa ni biashara hapo baadae na kimsingi mpango huo ulifanikiwa. Na ndio maana mpaka Leo watu wametawaliwa na mfumo wa majini katika maisha yao kwa kuwa wamefungwa akili ya kujitambua na wanaamini maneno ya mdomoni na sio Maandiko ya Biblia kama yanavyosema.
Nimengi sana ya kujifunza lakini kwa Leo naishia hapa.
ZAIDI TAZAMA HAPA
deogratius Nalimi Kisandu.
1. 1. 2017.
MAONI YA WADAU
-------------
-------------
-------------
-------------
-------------
-------------
--------------
--------------
--------------
-------------
Wenyewe wanasema Adam alikuwa mwislamu.Kanisa Katolik limekuwepo hata kabla ya Uislam. Hivyo maktaba ya Vatican imeshiba
Alipalizwa hakupaaaNipe mstari unaosema Maria alipaa kwenda mbinguni.
Unazungumzia hiyo karne ya 14, Martin Luther aliikuta Biblia ikiwa na vumbi katika maktaba. pamoja na usomi wake hakuwa kukutana na biblia hata ikitajwa kanisani au popote. Hiyo ndivyo ilivyokuwa Kanisa la Roma, ilikuwa inaelekea kuwa dola zaidi ya Kanisa. Uasi wa Martin LUther ndio iliyofanya Kanisa la katoliki kurudi nyuma na kuanza tena kutumia Bibliamtu yeyote akiamini kanisa linatumia biblia lazima atalipinga, maana yaliyopo kwenye biblia na yanayoendelea kwenye kanisa haviendani
ukielewa misimamo ya kanisa na chanzo cha imani yao huwezi ongelea biblia
hawafuati biblia, na ndio maana hawapendi watu wasome biblia. wanaona haina umuhimu
Luther alivoanza kufundisha chuo kikuuu akapata access ya kusoma biblia akashangaa sana, akaona mbona hatufuati biblia. katika kuhoji akaonekana muasi
ingekuwa vyema kama ungemrekebisha kama ulivyo sema hapo huku unamuonesha na huo mstari unaosema kuwa alipalizwa ili kusupport jibu lako hvyo ndivyo mkristo hutakiwa kujibu maswali ya kiimaniAlipalizwa hakupaaa
Weka mstari wa Biblia kuthibitisha hilo.kuwa Maria alipalilizwa mbinguniAlipalizwa hakupaaa
Yameulizwa maswali mawili, kwanini aliachana na kanisa katoliki na kwanini alinyofoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia?Luther alivoanza kufundisha chuo kikuuu akapata access ya kusoma biblia akashangaa sana, akaona mbona hatufuati biblia. katika kuhoji akaonekana muasi
Neno la MUNGU halijipingi unataka kudhihirisha kua unasema uongouongo wa mchana hebu lete andiko.
maana maria ndiye aliyesema hivyo.
LUKA 1:46-48.
anasema watamwita mmbarikiwa lakini sio Mungu kusema tutamwita hivyo
sijawahi kusoma popote juu ya kwamba huyo jamaa aliondoa vitabu kwenye bibliaYameulizwa maswali mawili, kwanini aliachana na kanisa katoliki na kwanini alinyofoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia?
Umejibu swali la kwanza, kujiondoa kwake kwenye ukatoliki. Swali la kwanini alinyofoa baadhi ya vitabu halijajibiwa.