Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,379
PICHA: Padri Martin Luther
Moja ya madai yake ilikuwa ni kuondoa kibali cha kwamba baada ya kuungama muumini asipewe stakabadhi ya kuonesha ameungama kwa kuwa kitubio ni siri ya mtu. Hili lilifanyiwa kazi. Mengine ikiwemo kurekebisha mfumo wa sala ya Kanuni ya Imani. Na mambo mengine mengi ambayo alipojibiwa, yeye hakuridhika pamoja na kueleweshwa vya kutosha. Alikuwa ni Great Thinker sana.
Mbaya zaidi alipokuja kusababisha mpaka akajitenga na kanisa ni kitendo cha kuondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia ikiwemo pia kupunguza baadhi ya mistari kwenye vitabu kama cha Esta na cha Danieli.
Aliondoa vitabu vya Deutrokanoni na vingine baadhi na kuwa jumla ya vitabu 7 vilivyotolewa kwenye Biblia. Na kila kitabu alikuwa na sababu yake aliyoibainisha. Kimsingi alipata wafuasi wengi wa kumuunga mkono hoja yake hasa wale ambao walikuwa wanatafuta njia ya kuchuma pesa kiulaini. Na hapo Biblia mpya ilianza yenye Vitabu pungufu.
Na ndio maana leo watu hawaujui Ukristo vizuri na wanakinzana bila kujua historia ya kanisa. Watumishi wengi wa Mungu hasa hawa wa kileo wasiojua historia vizuri wao kila kitu wanapinga. Sio kosa lao Bali ni kosa la kutokujua historia ya kanisa.
Matumizi ya Ubani yalipingwa sana, na hapa ilikuwa ni kuondoa idadi ya waelewa. Kutokana na watu wengi walikuwa wamegeuka kama waganga kila mapepo ya kiwakabili walitumia ubani kuyafukuza na yalikimbia, lakini watu walijisahau kusali na kuomba na hata kufika ibadani ikawa nadra maana wanajua kujiponya kuondokana na majini na wachawi. Hapa Padre Luther na wenzake wakapiga marufuku matumizi ya ubani na kuwa sihi wakazanie Neno zaidi.
Hapa walichotakiwa kufanya ni kuliishi Neno la Mungu na wakati wa ibada basi ubani uchomwe kama Mungu alivyo agiza.
Luther na wenzake lengo lao lilikuwa ni biashara hapo baadae na kimsingi mpango huo ulifanikiwa. Na ndio maana mpaka Leo watu wametawaliwa na mfumo wa majini katika maisha yao kwa kuwa wamefungwa akili ya kujitambua na wanaamini maneno ya mdomoni na sio Maandiko ya Biblia kama yanavyosema.
Nimengi sana ya kujifunza lakini kwa Leo naishia hapa.
ZAIDI TAZAMA HAPA
deogratius Nalimi Kisandu.
1. 1. 2017.
MAONI YA WADAU
-------------Mkuu kwa hili huna data.... Martine hakuwa Askofu, alikuwa Padre na miongoni mwa sababu zilizomuondoa kwenye kanisa Katoliki ni hili la Uaskofu, alipinga hairakia ya Kanisa na vyeo kama Uaskofu, Upapa na mengineyo. Sema tu mengi aliyoyapinga aliishia kuayatenda akiwa kwenye kanisa lake. Mengine ni suala la Useja, hakutaka kabisa kulisikia na alipoondoka aliondoka na Mtawa wa kike aliyeishia kuwa mkewe.
Mambo ni mengi sana na yanahitaji muda wa kutosha. Lakini niseme tu kwamba "siyo kila alilolipinga lilikuwa baya" mengine aliyapinga kihalali kabisa japo njia aliyoitumia haikuhalalisha kitendo chake!!!
Pili, Biblia za wapeotestanti na wapentekoste zina vitabu 66 wakati biblia ya Wakatoliki ina vitabu 72. Hili lilitokana na kuwa baadhi ya yaliyomo kwenye vitabu hivyo (deuterokanoni) vinapingana na mafundisho yao. Sababu nyingi ni za kibinadamu tu!!! Hili lilikuwa rahisi sana kwake kwani suala zima la "Utaifa" liliingizwq kwenye huu mchakato wa Luther kujiondoa kanisa, matokeo yake kwa vile alikuwa Mjerumani, dhehebu lake likawa "dini dora" ya Ujerumani, katika hali kama hii, ni rahisi kwa uwezo wa kifedha kuchapisha Biblia zenye vitabi 66 na kuviondoa vile vingine!!!!
-------------Kwa kifupi Martin luther naweza kusema alikuwa ni Opportunistic...Alipata loop hole ya kuondoa vitabu vya Agano la kale, baada ya kurejea mitaguso ya Kanisa(hasa mtaguso wa trent) masahihisho yanahitajika hapa....
Wakati Kanisa Katoliki lina-compile Bible, Kuna vitabu 7 vya Agano la Kale ambavyo vilipokelewa kwa lugha ya Kigiriki...Hivyo Wayahudi(Waisrael) hawakuvitambua vitabu hivyo simply bze of language....Hivyo Luther akatumia mwanya huo kuviondoa....
Ila alishindwa kuondoa vya Agano jipya maana hivyo vilikuwa nje ya uwezo wake.....Ila ni bahati tuu, maana alisha viondoa vitabu 3... Calvin alimsihi sana kuvirudisha...
Kituko
-------------Deogratius Kisandu,
Father Martin Luther alikuwa ni padre mwenye akili nyingi sana kuliko watu wengi wa kizazi chake cha karne ya 15.
1. Martin Luther aliviondoa baadhi ya vitabu katika canon ya Biblia baada ya kutoka katika Kanisa Katoliki.
2. Mambo mengi ambayo Martin Luther aliyasema katika karne ya 15 na kupingwa ndio ambayo Kanisa Katoliki linayatekeleza kuanzia karne ya 20. mfano. Kuchapisha Biblia katika Lugha asilia kama Kiswahili nk, kuruhusu lugha za kienyeji katika ibada ya misa nk
3. Kanisa Katoliki lililazimika kuitisha mtaguso mkuu wa Trenta ili kujibu hoja za martin Luther na kwa kuwa lilikuwa alikujiandaa liliishia kutoa makaripio ya kukemea tu anathema sit
4. Martin Luther ndio alisababisha katika kila chuo kikuu duniani lazima awepo padre anayeitwa chaplin
5. Martin Luther alipunguza pia idadi ya sakramenti kutoka 7 sa kanisa katoliki mpaka 3 za walutheri.
6. Martin Luther aliungwa mkono na taifa la Ujerumani.
Ahsante kwa sasa
-------------Martine hakuwa Askofu, alikuwa Padre na miongoni mwa sababu zilizomuondoa kwenye kanisa Katoliki ni hili la Uaskofu, alipinga hairakia ya Kanisa na vyeo kama Uaskofu, Upapa na mengineyo. Sema tu mengi aliyoyapinga aliishia kuayatenda akiwa kwenye kanisa lake. Mengine ni suala la Useja, hakutaka kabisa kulisikia na alipoondoka aliondoka na Mtawa wa kike aliyeishia kuwa mkewe.
Mambo ni mengi sana na yanahitaji muda wa kutosha. Lakini niseme tu kwamba "siyo kila alilolipinga lilikuwa baya" mengine aliyapinga kihalali kabisa japo njia aliyoitumia haikuhalalisha kitendo chake!!!
Pili, Biblia za wapeotestanti na wapentekoste zina vitabu 66 wakati biblia ya Wakatoliki ina vitabu 72. Hili lilitokana na kuwa baadhi ya yaliyomo kwenye vitabu hivyo (deuterokanoni) vinapingana na mafundisho yao. Sababu nyingi ni za kibinadamu tu!!! Hili lilikuwa rahisi sana kwake kwani suala zima la "Utaifa" liliingizwq kwenye huu mchakato wa Luther kujiondoa kanisa, matokeo yake kwa vile alikuwa Mjerumani, dhehebu lake likawa "dini dora" ya Ujerumani, katika hali kama hii, ni rahisi kwa uwezo wa kifedha kuchapisha Biblia zenye vitabi 66 na kuviondoa vile vingine!!!!
-------------Mtoa post nimpotoshaji mkubwa ningekuona ningekuhukumu kwa Sheria ya Mussa kukufungia jiwe jiwe la kilo 70 shingoni nakukutumbukiza baharini.
Sasa nakujibu Mnamo mwaka 333 kabla ya kuzaliwa Yesu nchi ya Palestina (Israeli) ilitawaliwa ns Wagiriki.Iliopopita miaka 70 yaani mwaka 403 Ndipo ilitolewa tafsiri ya kwanza ya torati na vitabu vya manabii katika lugha ya Kiyunani(Kigiriki).
Tafsiri hiyo iliitwa SEPTUAGINT,viliingizwa vitabu 11 ambavyo havikuwa katika orodha rasmi ya maandiko matakatifu ya Wayaudi wa Parestina.Vitabu hivyo vya nyongeza vilikuwa vimetafsiriwa kuanzia mwaka wa 363 ikiwa nimiaka 30 wa utawala wa Kagiriki na vilitokea Iskanderia (Alexanderia) ambavyo vilikuwa vikitumiwa na watu waliojiita Wayahudi.Kuingizwa vitabu hivyo kwenye SEPTUAGINT kulifanya Wayahudi waitishe mkutano mkuu wa wazee 70 wa Palestina.
Kikao kile kilijadili suala la maandiko ya Iskanderia yasiyokuwa matakatifu kuingizwa kwenye SEPTUAGINT ya Palestina.
Kikao hicho kijulikanacho kwa jina la Canon na ndicho kilichoviondoa vitabu 11 vya Iskanderia nakuvithibitisha kuwa ni batili.
Swari apo Martine Ruther alikua ameishazaliwa?
Kwamujibu wa maelezo ya Padre J.Bouguet des Chaux mwandishi wa kitabu cha JIFUNZE BIBLIA TAKATIFU,mnano karne ya 5 baada ya Yesu Kristo yahani karibu miaka 700 ya mkutano mkuu Canon,Papa Augustno aliamua aliamua kuongeza vitabu 6 kati ya vile 11 vya Iskanderia vilivyoondolewa na wazee 70 katika agano la kale.
Miaka 1,000 baadaye (1546) uamuzi wa Papa Augustino ulipata kibali rasmi kwenye mkutano mkuu wa Maaskofu wa kanisa Katoliki mjini trent-Uingereza bila kuwashirikisha wale wazee sabini wa Kipalestina.Lakini wale wazee hawakukata tamaa kufuatia matengenezo ya kanisa (Reformation) Vitabu hiyvo viliondolewa tena na ndipo palipotokea mpasuko wa Kiprotestanti ambao hadi leo wanaitambua orodha rasmi ya vitabu vya Wayahudi wa Palestina tu nakuvichukulia vile 6 viloongeza na Papa Austino kuwa ni batili.
Kwakumbukumbu sahii kati ya mwaka 93 hadi 130 baada ya Yesu viliandikwa vitabu vingine vingi ambavyo navyo vilionekana batili .kimojawapo kilifahamika kwa jina la Protevangelium, nyaraka za Clement,Iginatius,na Polycarp ambavyo vyote havikuruhusiwa kuingizwa ata kama maandiko kadhaa yalifanana na nyaraka sahii za Biblia lakini havikuwa maandiko matakatifu kwamaana tuipotayo 2Petro1:20-21.
Kwahiyo Martine Ruther alisimamia alichokikuta siokweli kwamba alifukuzwa kwasababu ya kuondoa maandiko matakatifu.Wakatoliki kwa hofu yakupinduliwa waliongeza vitabu hivyo vya sheria zao ambavyo mpaka leo Makasisi Mapadre,Maaskofu Makardinal na Papa wanajua hili na ndonapaswa kuulizia kwanini wanaendelea kushikilia vitabu batili wakijua kuwa sio sahii?
Mwisho:Tafuta kitabu kiitwacho Je nabii issa ndiye YESU KRISTO? na kingine kiitwacho Jifunze Biblia Takatifu
Usome kwa faida ya ubongo wako.
Ikiwa mnapenda kujadili kwa kina mambo ya ndani ya Biblia nendeni mkasome Katika vyuo vya Biblia ndipo mtaandika habari za usahihi. Luther alitafsiri Biblia sio kwa kibiashara bali alihoji kwa nini Neno la Mungu libakie katika lugha wasioielewa watu wengi? Aliwapa Wajerumani Biblia katika lugha Yao. Hakupunguza kitu kutoka Hebrew Old Testament na Greek New Testament alivyotumia Kama Source Text.
Sana aliongeza vitabu vya Apokrifa vile 6 vilivyokuwemo katika Latin Vulgate. Unaposema deutero-canonical unaelewa una maana gani? Unasema kusoma Historia ya Kanisa? Sema soma Biblical Studies, sema soma Historical Criticism ya vitabu vya Biblia, sema soma Textual Criticism ya hayo Maandiko. Sema soma Canonical texts za Biblia. Hapo ndipo utaelewa mengi kuhusu Maandiko ya Biblia. Luther si mfanya biashara.
Luther ni msomi aliyebobea katika Theolojia na kuona mapungufu na makengeufu ya Kanisa na kudiriki kusema. Luther aligundua kuwa wokovu ni kwa Imani na si kwa matendo ya kidini ama kazi za mtu. Unasema nini juu ya Luther Mwana mageuzi mkubwa alienusuru Imani sahihi ya kanisa kwa enzi hizo. Acha kabisa!!!!
-------------Ntuzu,
Kaka Mambo ya dini sio Magumu ni watu kuwa wagumu wa kuelewa na wengi hawampi Roho Mtakatifu muda wa kuwafunulia maandiko na Wachungaji na Wainjilisti ndio wanakuwa kila kitu
Kuhusu Bikira Maria, hiyo ni Habari kubwa na sio ya mchezo mchezo,
Kiimani ya Kikatoliki Yesu ni Neno la Mungu nae pia ni Mungu, na Kimaandiko sisi wote ni wakosefu kwa maana tuna dhambi ile ya kurithi, ile laana waliopewa Adam na Hawa mpaka leo tunayo, Mungu akalifanya Neno lake lije Duniani kuwakomboa wanadamu kwenye ile laana iliyotoka kwenye Mti wa katikati kupitia mti wa Msalaba
Yesu kama Mungu alikuwa hawezi kuja kupitia binadamu mwenye dhambi, Hivyo Bikira Maria alikingwa na ile dhambi ya ya Urithi, alikuwa PURE AND FRESH
Malaika Gabriel anatumwa kwa Mungu na anampa Maria ujumbe huu, kwamba MARIA AMEJAA NEEMA, BWANA YUKO NA WEWE NA UMEBARIKIWA KULIKO WANAWAKE WOTE, Pia hiyo Mimba itakuwa ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, So Maria ndio Binadamu wa kwanza Duniani kuzipokea nafsi zote tatu za Mungu, BABA, MWANA NA ROHO MTAKATIFU
Baada ya Malaika Gabriel kumwacha Maria, Bikira Maria hakuwa wa Dunia hii tena, alikuwa anatembea na Nafsi zote tatu za Mungu, na alikuwa kwenye Dunia ya Kiroho, Dunia ya watakatifu kwani alikuwa na Mwana wa Mungu ndani yake kwa Uwezo wa Roho mtakatifu
Alipofika kwa Elizabeth na kumsalimia, Yohana aliruka ndani ya tumbo la Elizabeth na Elizabeth alijazwa roho mtakatifu hapohapo Maria hakuwa mtu wa kawaida, na Eliza akijazwa na Roho mtakatifu akajikuta ananena kuwa MARIA WEWE UMEBARIKIWA KULIKO WANAWAKE WOTE
Nae Maria akiwa kwenye utakatifu wake Akasema Luka 1:48- vizizi vyote vitaniita MBARIKIWA
Na kwenye kitabu cha ufunuo kinaonyesha ni kwa jinsi gani Shetani akupenda mpango wa Mungu wa mkombozi kuzaliwa,
Na ishara kubwa ikaonekana Mbinguni, mwanamke mwenye mImba , mwanamke ALIYEVIKWA JUA NA MWEZI UKIWA MIGUUNI MWAKE, anataka kujifungua, na Shetani (Joka) anajitahidi kwa nguvu zote azuie mwokozi asizaliwe
Kasome Ufunuo 11:19 na 12:1-6 kwa habari kamili
Lakini pamoja na hayo yote, kwa Wakatoliki, BIKIRA MARIA SIO MUNGU, BIKIRA MARIA HAWEZI KUSAMEHE DHAMBI, BIKIRA MARIA HAWEZI KUOKOA MTU
KIKATOLIKI BIKIRA MARIA NI KAMA DARAJA LA KUTUUNGANISHA NA MWANAE (Yesu Kristo)
Nitaelezea baadae kivipi?
--------------Binafsi huwa naamini katika Imani Baina ya Mtu Binafsi na anachoamini kwa Mungu; Mlengo wa madhehebu umekuja ili kutupa Mwanga; baada ya hapo Mtu binafsi anatakiwa awe na Jitihada Binafsi za kumtafuta MUNGU yaan kibinafsi kabisa, na si tena kwa Mlengo wa Kidhehebu; Of which ukishafika hizo Level ukiwa kanisa lolote still hutaweza Fanya Baadhi ya Vitu kwa kufuata Mkumbo na hili linawezekana.
Binafsi nimeona tofauti sana, Ulaya na Huko Africa Especially Nyumbani Tz, Ulaya Issue za Imani huwa zinachukuliwa Personal zaid ya kuchukulia kwa mlengo wa Kundi; Hivyo ni rahisi kuona mtu wa Ulaya anafanya jambo lake kwa namna alivyoelewa yeye si kwa namna ya Mlengo wa kanisa lake.
Mfano: Baadhi ya makanisa Kuna maji unachovya Mkono na Unapiga ishara ya Msalaba; Sasa wako ambao kwa sababu zao wao hawachovyi kwasababu zao binafsi, Ijapokuwa Mlengo wa dini imeruhusu hichi kitu.
Sasa kwa wazungu kwasaababu wao hawana mambo ya Kutenga, Ila Tz nadhani watu wanaongopa mambo ya kutengwa,
Lakini pia nilishakuwa na mwaamini mmoja rafiki yangu tulikuwa tunafanya naye workshop moja, yeye binafsi ni High church Anglican Sala ya Salamu maria haikubali, Hivyo inapofika kuisema yeye hasemi anakausha tu au anafanya maombi yake binafsi, Jamaa alinifungua mambo mengi sana kuhusu Imani, alinisaidia sana.
Muhimu ni wewe kufahamu MUNGU binafsi, pia ninachoamini Mungu anatufahamu kuwa sisi tu Viumbe dhaifu, na tena Tumepungukiwa na utukufu wake, Hivyo hatuwezi sisi kujifanya kuweka taratibu nzuri za ibada, utaratibu fulani wa kusema sala kana kwamba Mungu ndio atakuwa kwenye Mlengo wetu, no Mungu haangalii Mlengo mungu ataangalia Mtu mmoja mmoja, Hivyo tujitahidi kusoma Vitu vingi zaidi, pia usijiwekee mipaka soma Biblia lakini pia soma Vitabu vya kihistoria, Kuumbuka kwamba hata baadhi ya waandishi wa bile walisema kwamba waliandika mambo machache sio kila kitu kiliandikwa maana isingetosha, sasa kwa nini usisome zaidi? tena kama mtu anayetafuta maarifa, kwanini usiwe na biblia zote mbili? kwanini utenge biblia za mlengo fulani, je ni kweli unahitaji kufahamu mambo? Kama imani ni suala binafsi kwanini wewe usiwe na bible yako yenye vitabu vingi zadi hata nyumbani kwako ukawa unajisomea? yaan kwasababu Mlengo wa dhehebu lako hawatumii na wewe usitumie? Africa kuna tatizo mahali, lakini naamini ni suala la Muda tu, mambo yatakaa sawa; maana watu wanapata expsure taratibu.
Ukiweza hayo mambo hutapata shida na dhehebu la mtu, ama taratibu zo namna wanavyosali/swali kwenye Hekali zao/ Sinagogi/misikiti yao;
Lakini kitu kingine ambacho mimi huwa naamini ni kwamba Moja wapo ya Vitu amabvyo Yesu alisisitiza ni UPENDO, na akasema kwamba Amri ya kwanza ni Kumpenda Mungu kwa Moyo wako wote,akili na Roho na ya pili akasema ni Kumpenda jirani yako kama nafsi yako; Ukiangali kwa karibu zaidi Hakuna Mlengo wa Dini ambayo inapinga UPENDO au haihubiri Upendo ( Achilia mbali watu amabao kwa itikadi zao binafsi wanafanya mauaji/ vurugu kwa mwamvuli wa dini etc, nazungumzia Msimamo wa hiyo dini katika ujumla wake) Maana kama ni vurugu wapo watu katika Christianity, Muslim, Budhist etc huwa wanafanya vurugu, lakini sio dini yao ni wao binafsi wanakuwa wamekengeuka.
Ni muhimu sana Kuheshimu Taratibu za watuwengine, na si kutoa maneno ya kashfa na yasiyofaa kuhusu taratibu zao; Infact sisi sote haya mambo tumepokea kutoka mahali, na kama ujuavyo kupokea kitu toka mahali mpaka kikufikie wewe ni nadra sana kukipata kama kilivyo.
Hata tu story tu za habari za cnn,bbc etc, the same information inakuwa reported tofauti kwa sababu mbalimbali, na ikitokea imekuwa the same tegemea kuwepo kwa tofauti kwa wapokeaji wa taarifa hiyo, kila mtu ataelewa kwa namna yake mwenyewe, naye anaweza kuelezea kwa namna alivyoelewa.
Last kabisa, Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vingi, ikumbukwe kwamba Vitabu hivyo viliandikwa Enzi hizo (Karne nyingi zilizopita) Si sawa kuleta tafsiri ya Moja kwa moja kwenye kipindi chetu hichi.
Ukiona kwenye biblia wanasema Farao alikuwa na magari na jeshi kubwa, lazima ufahamu gari hazikuwa kama izi za leo; ndio maana nikasema ukisoma Bible peke yake unaweza ukamiss baadh ya vitu, ndio maana ni vizuri kusoma vitabu vingine pia ili uongeze maarifa (Mimi naamini hata kama vitabu visingetolewa, bado isingewezekana kuandikwa kila kitu, hivyo kwa mtazamo wangu binafsi sioni tatizo sana, bado naweza tumia hivyo vilivyopo)
--------------VITABU VYA APOKRIFA
(Apocrypha – Hidden)
Apokrifa humanisha iliyofichika, ni maandiko yaliyokuwa yamefichika kwa maana ya kwamba hayakujulikana.
Neno Apocrypha linatokana na neno la kiyunani apokruphos ambalo ni muungano wa maneno mawil apo—mbali ya- na kruptolkruptos—iliyofichwa.
Vitabu vya apokrifa ni vitabu ambavyo Wakatoliki, na WaOthodox wa Urusi huvikubari kama maandiko makuu yanayofaa kufundishia imani.
Vitabu vya apokrifa ni maandiko ambayo yalichapishwa baada ya kipindi cha Nabii Malaki hadi kufikia mwisho wa Karne ya kwanza ya Ukristo.
Baadhi ya Vitabu vya apokrifa tutakavyo viangalia ni
1 Wamakabayo
2 Wamakabayo
Judithi
Tobiti
Wimbo wa Sulemani
Esdras
Baruch
Sira
Ombi la Manase
Hekima ya Sulemani
Walaka wa Yermia
Kutokana na Ushahidi tunaoupata katika agano jipya ni wazi kwamba Wayahudi walikuwa na Kitabu (Vitabu) ambavyo waliamini kuwa ni Sahihi na vinafaa kufundishia—CANON. Vitabu hivyo viliitwa Musa(Sheria), Manabii, na Zaburi au Torati na Manabii au Musa na Manabii. Tazama Math 5:17-18, 7:12, 11:13, 22:40. Luka 16:16-19, 24:27,44 Yohaa 1:45. Mdo 13:15, 24: 14. 28:23 na Rumi 3:2
Mwanahistoria Flavius Josephus (Karne ya Kwanza) akiandika katika mwaka wa 90 alitaja vitabu 24 vilivyokusanya historia ya Wayahudi ya kila ambacho kiliaminika kama Uvuvio.
Vitabu 5 vilindikwa na Musa, Vitabu 13 viliandikwa kati ya Musa na Mfalme Atashasta (Artaxerxes) wa Waajemi. Vitabu 4 vilikuwa vimejumuisha mashairi (vitabu vya Mashairi) na Nyimbo, Zaburi, Methali, Muhubiri, Maombolezo (Against Apion 1:38-40)
Kisha Josephus akaendelea kusema “Ni kweli kwamba Historia yetu imekuwa ikiandikwa toka wakati wa Atashasta, lakini maandiko hayo hayajachukuliwa kuwa ni maandiko sawa na maandiko ya kale ya Mababu zetu. Hii ni kwa sababu, hakuna mfuatano wa Manabii toka wakati huo.
Na ni kwa kiasi gani tumekuwa na msimamo mkali na kuaenze maandiko hayo na kuchunga asije mtu akaongeza katika maandiko—Toka wakati huo, haijawahi kutokea mtu kuongeza maandiko hayo au kupunguza au kufanya badiriko lolote ndani yake.” (Against Apion 1:38-40)
Hivyo Jusephus alishikilia msimamo wa Wayahudi wote kwamba maandiko yote yaliyoandikwa baada ya Utawala wa Atashasta (yaani baada ya Wayahudi kutoka utumwani Babeli) kuwa hayana Uvuvio kwa kuwa hakukuwa na Unbii katika kipindi hicho katika Israel.
Utagundua kuwa Sababu kubwa anayoitoa Josephus ya Kukataa maandiko hayo ni kwasabubu hakukuwa na unabii. Vitabu vyote nilivyovitaja hapo juu viliandikwa katika kipindi hicho.
Vitabu vilivyoorodheshwa na Josephus ndivyo hivyo ambavyo huunda jumla ya Vitabu 66 vilivyomo katika biblia inayokubaliwa na Waprotestant wote duniani. Sababu iliyowafanya waprotestant kuvikataa vitabu hivyo ni Sababu hiyo hiyo iliyotolewa na Josephus. HAVIKUANDIKWA NA MAANABII WALIOTUMWA NA MUNGU. NI WATU TU WALIKUWA WAKIJIANDIKIA HISTORIA NA MAMBO YA WAYAHUDI.
SABABU NYINGINE KWANINI WAPROTESTANT WANAVIKATAA VITABU HIVYO.
Yudith 1:17 Nebukadneza ni Mfalme wa Ashuru
- Makosa yaliyomo
Niwazi kabisa kwamba Vitabu hivi havina mafundisho yenye Uvuvio na vinapingana na vitabu vingine 66 vya Bibli.
- Tobit 5:13 Malaika alisema Uongo (Azalia Mwana wa Mzee…)
- Tobit 6:1-8. 14 Vinafundisha Uchawi
- Baruku 3:4 Baruku Mwandishi wa Yeremia ananukuru Daniel
- Baruku 3:4, 12:43-45 Vinafundisha Maombi kwa Wafu.
Ndiyo maana basi Biblia inayokubarika kwa Waprotestant wote ni ile yenye Vitabu 66.
--------------Hivyo vitabu vya ziada pamoja na vingine vingi ambavyo hawaja viamabatanisha kwenye biblia zao lakini wanaviamini vinaitwa vitabu vya apokrifa maana yake vitabu vilivyofichwa na wakatoliki wakati wakristo wa mwanzo walivichoma moto kwamadai kuwa si vitabu vya ukristo bali hadithi za kutunga.zifuatazo ni sababu
Sababu za vitabu vya ziada vya
Apokrifa kutokubalika.
(1) Havijatajwa au kunukunuliwa na
Kristo wala Mitume Wake; hata
Kanisa la Kiyahudi halikuvikubali.
Kuna takribani nukuu 263 na
vidokezo 370 kuhusiana na Agano la
Kale kwenye vitabu vya Agano Jipya,
lakini hakuna hata mojawapo
inayotaja vitabu hivi vya ziada!
(2) Viliongezwa baadaye (1546 AD
katika Baraza la Trent) katika orodha
ya vitabu vya Biblia kwa sababu vina
vipengele vinavyotetea mafundisho
potofu ya Kanisa Katoliki: fundisho
la Toharani, kuwaombea wafu,
hazina ya matendo mema ya
watakatifu, ukamilifu wa kutokuwa
na dhambi.
(3) Hakuna hata kimojawapo
kilichoandikwa kwa lugha ya
Kiebrania. Waandishi wa vitabu vya
AK walitumia lugha hii.
(4) Havikuwa miongoni mwa vitabu
takatifu katika karne nne za kwanza
za Kanisa la Kikristo.
(5) Vina kauli za uongo na kubuni
zinazokinzana na Maandiko na hata
yenyewe. Kwa mfano:
(A) Antiochus Epiphanes anatajwa
kuwa anakufa vifo 3 tofauti na
katika maeneo tofauti.
(B) “Kwa hiyo ni tendo takatifu na
pia wazo linalofaa kwa uzima
kuwaombea wafu, ili waweze
kufunguliwa kutoka katika dhambi
(2 Wamakabayo 12:39-46).
(C) Sira 25:19 Udhalimu wowote ni
mdogo sana ukilinganishwa na
udhalimu wa mke.
(D) Sira 22:3 …kumzaa binti ni
hasara
(E) Hufundisha mambo maovu:
kusema uongo, kujiua, kuua, na
mazingaombwe/uchawi
(6) Wanahistoria na wanazuoni wa
awali wa Biblia walidai kuwa vitabu
hivi havikuvuviwa sawa na vile vya
Maandiko Matakatifu (Melito, AD
170; Origen; Jerome, nk). Jerome,
Mkatoliki alikuwa wa kwanza kuvitaja
vitabu 7 hivyo kama “Apokrifa”
yaani vitabu vyenye kutiliwa
mashaka ya uhalisia wake. Na
hakuvihusisha katika fasiri yake ya
Kilatini (Vulgate).
(7) Kanisa Katoliki hudai kuwa
Mabaraza ya Kanisa ya Hippo (393)
na Carthage (397, 419),
yaliorodhesha vitabu vya Apokrifa
kama sehemu ya Maandiko. Kwa
sababu mabaraza haya ndiyo
yaliyokamilisha ukusanyaji wa vitabu
halali 66 vya Biblia ambavyo
Wakristo wote huvikubali, lazima
wavikubali vyote.
Hoja hii ni ya uongo. Vitabu halali
vya Agano Jipya vilijulikana tangu
mwanzo katika karne ya kwanza. Ni
ubunifu wa Kanisa Katoliki kuwa
lenye ndilo lililoupatia ulimwengu
Biblia!
-------------
Kwa kifupi Martin luther naweza kusema alikuwa ni Opportunistic...Alipata loop hole ya kuondoa vitabu vya Agano la kale, baada ya kurejea mitaguso ya Kanisa (hasa mtaguso wa trent) masahihisho yanahitajika hapa.
Wakati Kanisa Katoliki lina-compile Bible, Kuna vitabu 7 vya Agano la Kale ambavyo vilipokelewa kwa lugha ya Kigiriki...Hivyo Wayahudi(Waisrael) hawakuvitambua vitabu hivyo simply bze of language....Hivyo Luther akatumia mwanya huo kuviondoa.
Ila alishindwa kuondoa vya Agano jipya maana hivyo vilikuwa nje ya uwezo wake.....Ila ni bahati tuu, maana alisha viondoa vitabu 3... Calvin alimsihi sana kuvirudisha...
Kituko