Wauza barafu,ice cream za majubani,wauza juice,soda,maji ya baridi,fruit za baridi,hali ni ngumu,ngumu sana.Hakuna umeme,wakufanya barafu zinfande na ice cream kuganda,,nq juice na maji kupata baridi,hakuna kipato.Umeathiri kila kitu.
Wajasiliamali wadogo kama vinyozi, mafundi wa kuchomelea hela sasa hivi wanazishika kwa manati, huduma za kijamii zimekuwa hovyo mfano kuna maeneo utokaji wa maji unategemea uwepo wa umeme kama umeme hakuna maji inakuwa msamiati mwingine.
TANESCO na waziri wa hii wizara ajitafakali sana kwanini enzi za jiwe umeme ulikuwa hauna shida wao wanashindwa nini, kuna biashara gani wanafanya kwenye huu mgao wa umeme?
Kama wachuuzi wa barafu,ice cream,juice na maji ya baridi,maisha yamekuwa ni shida kwao.Hawana cha kuuza,barafu hazigandi,maji na juice hazipati baridi,ice cream za kutengeneza majumbani hqzigandi.Maisha magumu sana.Watu wengine tena walio wengi "bila umeme mkono hauendi kinywani ". Athari ni kubwa. Kama kuna uzembe, huyo mzembe ni "MUUWAJI ".
Hali ni ngumu.wachuuzi wa barafu,ice cream za majumbani,juice,maji ya baridi,hali ni ngumu.Wengi walinunua freezer kwa biashara hizo,zi wakimu kimaisha.Watu wengine tena walio wengi "bila umeme mkono hauendi kinywani ". Athari ni kubwa. Kama kuna uzembe, huyo mzembe ni "MUUWAJI ".
Tumia inverter ya pure sine na betri N 100 au 200 ya kampuni Fulani hivi inaitwa Ritar SEMA bei zao zimechangamka kidogo.Nalaza kazi za ofisi katika matumizi ya computer, nalazimika kusafiri km 15 kufuata mafuta sheli ili generator liwake.
Wakati mwingine umeme urudipo usiku kama hivi leo nalazimika kwenda ofisini nikafanye kazi kwa kuwa sina uhakika kama kesho asubuhi umeme utakuwepo, tabu tupu ni mgogoro tu na wife kunihisi nipo mchepuko wakati napiga kazi muda huu.
Mkuu waweza tafuta fundi akakusukia inverter ya pure sine ambayo inaundwa kulingana na matumizi yako. Alafu unatafuta betri za kwenye minara, au za kampuni za Rita ya N100 au N200 kulingana na matumizi yako. Then unapeta maana inverter inakuwa na sehemu ya kuchajia umeme ukirudi. Pia Kuna mfumo unafungwa ambao utafanya kazi zako zisitetereke pale ambapo umeme umekuja Kwa ghafla au kukatika.Nilikuwa natotoresha vifaranga kwa kutumia incubator. Nilikuwa natotoresha vifaranga 1000 vya kuku, Bata na Kanga. Niliacha toka mwezi wa 10 tokana na changamoto ya umeme nikajua baada ya muda utastablelize.
Tokana na pressure ya wateja, ikabidi nitafute generator na kuanza kupiga kazi mwezi 12. Gharama zimekuwa juu kwani inabidi nitumie ⛽️ ⛽️ kuendesha mtambo. Sasa sipati faida kwani nafanya kuridhisha wateja tu.