Mjadala: Gharama na njia nafuu za kujenga nyumba ya kuishi Tanzania

Tumia interlocking bricks mkuu, na kupaua tumia style ya hiden rooftop, dirisha zako za aluminium na milango ya mchina, tires siku hizi bei kitonga pamoja na gypsum.....itawezekana tu, lakini punguza ukubwa wa nyumba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
chumba cha wazazi wakienda wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mada imepamba moto; naombeni kujua, hivi kwa hapa Tanzania nikitaka prefabricated houses zinapatiakana? Kwa yeyote mwenye kufahamu naomba anisaidie kujua katika hilo kwa undani
 
Kwa mahitaji ya Mbao kwa Bei nafuu tuwasiliane 0674344436View attachment 1026672

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu, nina kiwanja cha square kilometer 400, nimeshazungusha ukuta upande mmoja bado pande tatu ni kama tofali elfu 2 kasoro hivi za nchi 5 na 6 jumla.
Nipeni gharama zake au fundi mzuri aende aone site then tuongee bei.
Contacts 0716282670.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasikia hata gereji watu hawataki tena kuiweka pamoja na nyumba. Wanapenda iwe pembeni. Vipi wakuu hili mnalionaje? Kuna sababu za kiufundi, kiusalama au ni maamuzi ya watu tu?
Nahisi hii ya kuweka garage kwa nyumba ni zile plans tunazo copy and paste kutoka Ulaya
Inawezekana wao huweka hivyo kutokana na hali ya hewa(wakati wa barafu) au kuna wezi werevu sana wa magari kuliko huku kwetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeah akikwambia mbao ni kiasi fulani lazima a justify amefikiaje kwango hicho au tiles au bati
Kuna mmoja alinifanyia estimations za gypsum aka overestimates makusudi ili zitazobaki azivushe
Bahati nzuri nilikuwa nakopa kwa jamaa yangu ana Hardware akaniuliza unajenga nyumba ya ukubwa gani nikamuelekeza akaniambia ni nyingi sana zaidi ya 1/3 ya mahitaji zichukue lakini tight ulinzi na kweli nika tight ulinzi kuna kijana mmoja nilimuweka mlinzi akaniambia fundi huwa anakuja saa 4:00 usiku anadai amesahau kitu flani hivi then akajaribu kumshirikisha jamaa kwenye issue ili wachukue zile gypsum zilizobaki. Mlinzi akamwambia jamaa kila saa anasililizia mimi mwenyewe hapa kuna watu wananilinda
Kweli ilipofika mwisho more than 1/3 ya gypsum nilizirudisha
Wana overestimates ili wavushe mzigo au wana underestimate kama anajua uko busy kazini anakupigia simu saa 5 asubuhi bwana kazi zimesimama huku tofali zimeisha anajua huwezi toka utamtumia pesa au utamtuma sehemu akachukue tofali sehemu ya kwenda chukua tofali 300 atachukua 500
Hao ndio mafundi wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BY then hapo kwa mchanganuo wa mdau cjaona aweke cost za water system,electricity na hata toilets (amesema just masink tena ya ukutan or yanauzwa yakiwa complete na vyoo vyake?) .kama vp atusaidie please.
Hata hapo kwenye ma Sink ameweka
Masink 30 bei 45,000= 135,000
Ukicheck sio 135,000/= bali 1,350,000/=
Halafu masink 30 hiyo imekuwa boarding School
Au alikimaanisha masink 3

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna psychological relief unaipata ukifikia hapo. Unakuwa uko tayari hata kushindia mkate ili ufikie finishing

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unachokizungumza you are more than correct. Tatizo kubwa linalotufanya tukipata pesa kukimbilia kujenga ni kwamba hatuna confidence ya kukaa na pesa na tukazifanya pesa zikatutumikia badala ya kuzitumikia(ref Kiyosaki) nitakupa case studies 2

1.Kulikuwa na Dada nafanya nae kazi maeneo ya Muhimbili alikuwa akiishi Mbagala Charambe, ili kuwahi ofisini inabidi aamke saa 10 usiku, jioni akitoka saa 11:30 anafika home saa 4:30 usiku ana mtoto mchanga na ndio amemaliza ile likizo yao ya kunyonyesha hivi huyu Mwanamke anamuangalia mumewe saa ngapi ? watoto jee ?? Kutwa anasinzia kazini sikwambii poor decisions anazozifanya kwa kutopata muda wa kupumzila
Jaribu kuangalia gharama na adhabu anayoipata for the sake of Personal Status kwamba na yeye amejenga nyumba

2. Kuna kijana mwingine anaitwa Hassan huyu sio Mwarabu wala Muhindi yeye Mluguru. Anafanya biashara ya jumla ya mitumba ananunua kwa dealers wa Kihindi ambao akinunua mzigo wa 30m wanamkopesha mwingine wa 30m kutokana na uaminifu alioonyesha
Haya haya mambo ya Social Status akafanya matusi yake akajenga kitu kinafika 110m Mbezi. Baada ya muda wale wahindi wakaanza kumshangaa spidi ya kuchukua mzigo imekata wakamtahadharisha na unajua mtu ambaye alikuwa ananunua mzigo wa 30m anakuja nunua mzigo wa 7m hata kama ulikuwa unamkopesha unaanza kuogopa. Jamaa akakaa chini akatafakarii akaona biashara anayofanya ni kama ya miaka 5 iliyopita. Akagundua kuwa ujenzi umekata mtaji yaani umemrudisha nyuma kibiashara miaka 5.
Akapiga moyo konde na ashukuru Mungu alishtuka mapema akaiuza ile nyumba iliyogharimu 110m kwa 70m akaenda kupanga Magomeni upande mmoja wa nyumba. Nawapa history ya mtu ninaemjua na hayo yamemtokea kama miaka 2 au 3 iliyopita hivi sasa ukiacha ile biashara ya mwanzo ana maduka mengine mawili kariakoo na huwezi kuamini ile pesa aliyokuwa anatumia mbezi kwa petrol kutokana na distance inazidi kodi ya nyumba ya Magomeni

Kitu ambacho jamaa kimemsaidia sio mshamba wa hela anajua kuizungusha na pesa haimuendeshi yeye ndio anaiendesha




Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Tengeneza shamba lako kabla ya nyumba yako" Wafalme

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…