kacherokachero
Member
- Aug 5, 2018
- 74
- 43
Hujatuambia unataka kujenga kijijini au mjini na unatumia materia utakayotumia yanaweza kutoa mwelekeo WS matokeo makubwa sasa
chumba cha wazazi wakienda wapi?Umesahau sebule ambalo mara nyingi ni kubwa sana, chumba cha wazazi ambacho nacho ni kikubwa na kina kuwa self-container, chumba cha kulia chakula,vyoo , bafu, jiko, stoo, korido, sehemu inayochukuliwa na kuta, gereji n.k.! Nyumba ya vyumba vitano VYA KULALA kwa matashi ya kitanzania haitapungua mita za mraba 200!
Ukizidisha hiyo na hizo namba zinazotajwa utajikuta uko kwenye milioni 500! Dawa ni kuwa realistic kitu ambacho kinatushinda wengi. Mfano ni kuita nyumba yenye vyumba vya kulala vitano kuwa ya kawaida! Itakuwa ya kawaida tu kama utaijenga mithali ya nyumba zetu za kiasili za kiswahili. Vyumba bila kutofautisha, korido katikati, ua na jiko, bafu na choo nje!
Amandla.......
Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya kiumbe kipya khaa uko era ipi weye
Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu, nina kiwanja cha square kilometer 400, nimeshazungusha ukuta upande mmoja bado pande tatu ni kama tofali elfu 2 kasoro hivi za nchi 5 na 6 jumla.Kwa mahitaji ya Mbao kwa Bei nafuu tuwasiliane 0674344436View attachment 1026672
Sent using Jamii Forums mobile app
Nahisi hii ya kuweka garage kwa nyumba ni zile plans tunazo copy and paste kutoka UlayaNasikia hata gereji watu hawataki tena kuiweka pamoja na nyumba. Wanapenda iwe pembeni. Vipi wakuu hili mnalionaje? Kuna sababu za kiufundi, kiusalama au ni maamuzi ya watu tu?
Kuzidisha au kutozidisha gharama za QS hazisababishwi na kuwa na taaluma au kutokuwa na taaluma ya QS ni character ya mtu na jinsi gani anavyoheshimu kazi yakeWewe unayesema qs wanazidisha bei mara mbili una taaluma gani coz mimi qs
Yeah akikwambia mbao ni kiasi fulani lazima a justify amefikiaje kwango hicho au tiles au batisijasoma post zote zilizotangulia kama narudia points samahanini ndugu zangu
Mimi nyumba ya vyumba 5, vyoo 2- kimoja self container, nimejenga kwa milioni 15 na kidogo kuanzia kiwanja, ramani, msingi, kuta (incuding baraza ya mbele na nyuma), paaa na gutters. Imesimama kwa sasa ...nimetumia mafundi hawa wa mitaani baada ya kuona kazi zao kwa macho yangu au kupata good report kutoka kwa wenye nyumba, na nikasimamia mwenyewe... personally, na hii ndio taabu yake, inabidi kusimamia kweli maana mafundi hawa wa mitaani wanaiba sana...
mfano, kuna siku fundi alipanga njama na muuza mbao ... fundi akanitajia idadi ya mbao kuliko kiasi kinachohitajika mimi nikanunua mbao za kutosha na extra kidogo just in case!, kesho yake asubuhi jirani yangu akaniambia nilipoondoka jioni yule muuza mbao alirudi jioni na gari yake akachukua sehemu ya zile mbao, nikampigia simu fundi kumuuliza aliruka na hakurudi tena kazini, sikuwa na muda wa kufuatilia saaana kwa hiyo nikabadilisha fundi na duka la vifaa...hopeful utajifunza kitu kutokana na experience yangu..kama unasimamia mwenyewe inabidi pia uwe na rough idea ya kiasi cha vifaa kinachohitajika la sivyo utatapeliwa
Umenifurahisha ulivyoweka mahesabu yako ingawa inaweza ikawa nyumba haijaisha hapo kuna vitu kamaAsante sana. Je nyumba yako ina ukubwa gani?
Hata hapo kwenye ma Sink amewekaBY then hapo kwa mchanganuo wa mdau cjaona aweke cost za water system,electricity na hata toilets (amesema just masink tena ya ukutan or yanauzwa yakiwa complete na vyoo vyake?) .kama vp atusaidie please.
Kuna psychological relief unaipata ukifikia hapo. Unakuwa uko tayari hata kushindia mkate ili ufikie finishingMkuuuu,tupe progress baada ya kuweka madirisha,miundombinu ya maji taka,safi,milango,ceiling boards n.k,huko ndio kwenye balaa,mbona kupandisha boma sio kazi,kazi finishing mkuu,hapo ndo utakapotoa macho utakapoambiwa wiring tu milioni unusu na ndipo utakapoanza kuwachukia mafundi
Unachokizungumza you are more than correct. Tatizo kubwa linalotufanya tukipata pesa kukimbilia kujenga ni kwamba hatuna confidence ya kukaa na pesa na tukazifanya pesa zikatutumikia badala ya kuzitumikia(ref Kiyosaki) nitakupa case studies 2My Opinion
Hapa Tanzania kuwa na nyumba ni suala la KIJAMII zaidi. Yaani kuna heshima fulani mtu akiwa na nyumba yake. Watu wengi huifuata hiyo heshima, hata kama hana hitajio la nyumba wakati huo.
Nakupa mfano, kuna mtu amejenga mbezi ya kimara ndani ndani huko akahamia vizuri tu. Kilichotokea ni kwamba analazimika kuamka saa 10 alfajir na hurud saa 4 usiku akawa anawaona watoto wake na kufanya mambo ya kifamilia weekend tu. Kahama kaacha nyumba karudi kupanga karibu na mjini. Sawa unakaa kwako, unajua opportunity cost ya kukaa kwako? Subiri uzeeke utaenda kukaa huko fo the rest of ur life!!!
Unawajua wahindi na waarabu wa pale katikati ya mji wa Dar? Wangapi wanamiliki nyumba? Hawana uwezo wa kujenga wale? Tena wapo nchi hii tangu Nyerere alipotaifisha baadhi ya nyumba zao, kwa hiyo wanaijua vizuri Tanzania. Jitazame, kama huna hitajio la nyumba binafsi kuishi kwa wakati huu, jenga pole pole tu. Usikurupuke eti kisa upate heshima. Hata Mungu hakuumba ulimwengu siku moja, ipo siku utahamia kwako comfortably.
Lipa kodi kwa baba mwenye nyumba, jenga polepole.
MullaX
"Tengeneza shamba lako kabla ya nyumba yako" WafalmeWabongo hawatakuelewa ila kwa uchunguzi Mdogo ni kwaba wanawake hushawishi waume wao kujenga baada ya umbea kwenye makutano yao vicoba au bombani na sentensi "NINA KWANGU" imekuwa kama siasa za UKUTA na vunja ukuta bila kuangalia mbele.
Jamaa wawili walifanya kazi ofisi moja. Mmoja akaanza kujenga na wa pili akaanza biashara ya kilimo chenye miundombinu ya umwagiliaji kiasi kwamba habahatishi. Ile kazi mradi ulifika mwisho wrote wakarudi kijiweni. Aliyejenga alianza kutafuta kazi huku mkulima akinyanyua nyumba bila wasiwasi na bila shaka ya chanzo cha kipato. NI VIGUMU SANA KUANZISHA BIASHARA IKAKOMAA ILA NI RAHISI KUJENGA. Amua unaanza na kipi.
Sio Wafalme mkuu ni Mithali 24:27. Ukisoma English versions ndo unaweza kupata tafsiri nzuri