Mjadala: Gharama na njia nafuu za kujenga nyumba ya kuishi Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjadala: Gharama na njia nafuu za kujenga nyumba ya kuishi Tanzania

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Guantanamo Bay, Sep 24, 2010.

 1. G

  Guantanamo Bay Member

  #1
  Sep 24, 2010
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Jamani naomba niulize kwa wana JF ambao ni wataalamu wa ujenzi.

  Naomba wanipatie bajeti ya kujenga nyumba ya kawaida yenye vyumba 5, sebule, kitchen, dinning na sitting room ina cost kwa makisio shilingi ngapi?

  Naomba nielimishwe,

  Asanteni.

  ======
  SIMILAR CASES:
   
 2. L

  Lady JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Gharama ya kujenga nyumba inategemea ni nyumba aina gani unaitaka, ni single or double storey etc.

  Unajenga mkoa gani, ipo karibu au mbali na mji, material gani unataka kutumia, labour cost, unataka professional au mafundi wa mtaani, quality ya material etc,

  So mimi nakushauri tafuta Architect akuchoree ramani, Structural Engineer kwa ajili ya michoro ya columns etc. then mpe Quantity Surveyor mchoro yeye atakupa estimate, BUT estimate nyingi wanazotoa Quantity Surveyors huwa naona wanazidisha mara mbili ya gharama.
   
 3. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Ushauri mzuri huo, bila kkusahau finishing na gadgets anatakaje!
   
 4. m

  manyusi JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2010
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 274
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Kwa haraka haraka nitakupa makadirio maana ndizo kazi zangu hizo chukua square meter za ramani yako times 500,000 utapata garama ya morden house with everything you need.

  Kama hujaelewa nina maana Urefu X Upana X 500,000=Construction cost

  Hapo nina maana unatumia mkandarasi.
   
 5. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Average in DSM TZS Million 100/=

  With Kigae, Tiles, Fence, paint, plumbing, electricity etc.
   
 6. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  manyusi nimefaidika na uwezo wa kufanya mahesabu ya haraka katika ujenzi.

  Jee ya ghorofa unazidisha gharama hizo mara mbili (ikiwa ni floor moja)?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Vyumba vitano? hiyo siyo ya kawaida ni jumba kubwa tu! Kama upo Dar, andaa kwa uchache milioni 200.
   
 8. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na SMU huo mjumba balaa, yaani mkubwa kweli kweli.

  Ukijenga mjumba wa size hiyo jee watoto wako wakishaondoka wamemaliza shule utaufanya nini? Vile vile ni kujihakikishia idadi kubwa ya wageni kwa muda wote kwani kuna nafasi ya kutosha.

  Maintenance costs ndio hazisemeki, unaweza kufaidi for the first four to five years, baadae ndio harakati za maintenance zinapoanza hapo.

  Halafu TRA watakapokupiga hiyo property tax ndio utakoma ubishi.

  Majumba ya aina hiyo yalikuwa yanajengwa mnamo miaka ya tisini sio sasa hivi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Engineer mmoja aliwahi niambia gharama za ujenzi pamoja na mambo mengine zinategemea pia na client mwenyewe.

  Kama familia yako ni ndogo na pesa ya ujenzi siyo ya Richmond, vyumba vitatu vya kulala ni standard, cha ajabu watu wanajipinda na vyumba vya ziada vinavyokuja ishia vumbi.
   
 10. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Manyusi nadhani biti mkongwe alikua na swali la nyongeze, hata mimi nimependa urahisishajiwako wa matumizi ya namba. Simplification. tafadhali malizia, ukipata nafasi.
  Shukran.
   
 11. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Kwa bei za bongo andaa millioni 500 kama unataka kujenga na mafundi wetu. Njia rahisi kama wewe sio mhandisi/uliyebobea mambo ya ujenzi nunua zilizojengwa/zinazojengwa na NHC bei itakuwa nafuu zaidi kuliko hawa wanaotaka kuganga njaa. kila lakheri.
   
 12. G

  Guantanamo Bay Member

  #12
  Sep 25, 2010
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwanza kwa wote mliochangia hii post nawaomba niwagongee senksi,kwa sababu ile kitufe cha kubofya senksi hakionekani kwangu.

  Pili kuna nyumba (flat) ni mpya vya vyumba vitatu inauzwa kwa milioni 53 hapa Tanga.

  Naomba wadau mniambie ni deal nzuri kununua au ni vizuri kujenga mwenyewe kwa hapa Tanga?

  Asanteni.
   
 13. K

  Kimla JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2010
  Joined: Jun 8, 2008
  Messages: 1,509
  Likes Received: 1,402
  Trophy Points: 280
  Ndugu wanaforum,

  Naomba Ushauri wenu juu ya ujenzi wa nyumba Dar.

  Kutokana na uwezo mdogo, nimeshauliwa nitumie system inyoitwa interlocking blocks, amabyo inatumia tofari zinazotokana na mchanganyiko waudongo wa kisuguu na cement.

  Swali:
  Je, hii teknolojia ipo Dar?
  Je inasaidia kupunguza gharama za ujenzi na kwa % ngapi ukilinganisha na nyumba ya tofali za Cement za kawaida?
  Je, nyumba hiyo inaweza kudumu mda mrefu kama ya cement?

  Nipeni ushauri ndugu zangu.
   
 14. m

  manyusi JF-Expert Member

  #14
  Sep 25, 2010
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 274
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Yes kama ni gorofa unazidisha mara mbili au unachukua square meter za juu times 500,000 plus sqm za chini times 500,000 sum up the two values u will and get the roughly approximation.

  Tatizo wabongo hampendi kutumia wataalam wa kazi hizo unajikuta mafundi wanawaibia wanafanya vitu vya low quality,jifunzeni kutumia wataalam katika kazi ambazo hamna utaalamu wake.

  Kwa mfano unaweza ukamtumia quantity surveyor akakupa quantity ya material na garama yake hapo unapata picha halisi ya garama ya nyumba yako na ni kwa garama nafuu tu pale UCLAS wapo vijana wazuri tu hata mtaani. Ukihitaji contact za hao watu ni PM
   
 15. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #15
  Sep 26, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  manyusi, Shukran. Kwa msaada wako.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2010
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Manyusi, hapa ni pamoja na ghrama za mafundi au ni ghrama za material peke yake?
   
 17. T

  Tata JF-Expert Member

  #17
  Sep 26, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,737
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 280
  Tatizo la hawa wataalam wengine kazi yao ni copy and paste. Creativity sifuri kabisa. Sana sana wanaishia kukuchorea maboxi tu.
   
 18. Ncha

  Ncha JF-Expert Member

  #18
  Sep 26, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hawazidishi, ni information utakayotoa. kumbuka kumwambia kama utatumia mkandarasi au standard na quality ya materials. hivyo vina mchango mkubwa kwenye bei. usipompa taarifa zote yeye ili kuwa safe ataenda kwa bei za juu.

  500,000/= hata mi nakubaliana nayo kwa kiasi kikubwa. hapo ni labour, materials na kila kitu kasoro loose furnitures
   
 19. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #19
  Sep 26, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Sasa hwa si ndiyo umesema tusiwatumie?!
   
 20. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #20
  Sep 26, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hii imekaa sawa kweli? ina maana kwa nyumba ya vyumba 5 alioulizia mkuu inaweza kuwa around Tzsh 25 - 30 Million?.

  Hii ukikadiria kwamba kila chumba kitakuwa na ukubwa wa 10 square meters. ((10 x 5) x 500,000) = 25,000,000.

  Kwa utaratibu huu mbona gharama zitakuwa ni ndogo ukilinganisha na gharama tunazozisikia kila siku?
   
Loading...