Mjadala: Basi kubwa na pikipiki vikitembea vyote kwa 120km/hr nani atatangulia?

Nomba wataalamu mnitoe tongotongo, ikitokea basi la mkoa na pikipiki aina yeyote vikatembea speed moja ya 120km/hr na pasipo kizuizi cha aina yeyote njiani ( Take every thing is constant) .

KATI YA BASI NA PIKIPIKI NANI ATATANGULIA KUFIKA?

Naombeni wataalam mtusaidie hapa.
Lakini swali lako lina utata kidogo. Kwanza halijielezi kama hilo basi na hiyo pikipiki vimetokea sehemu moja na vinaelekea sehemu ileile ambapo vitafika, pili swali halielezi kama hiyo safari vimeanza pamoja au vimekutana point fulani vikiwa katika speed hiyo ya 120km/hr.
Ukitoa ufafanuzi huo ndipo jibu litaweza kupatikana.
 
Mwendo wa gari hupimwa kwa mzunguko wa tairi lake, kadhalika pikipiki. Sasa kufikia 120km/hr kwa gari na pikipiki mzunguko wa tairi unaweza kuwa tofauti lakini mwendo bado utakuwa sawa.

Sasa kwa mujibu wa swali la mtoa mada, vyombo vyote viwili vitafika sawa kwa kuwa vitakuwa na mwendo sawa yaani 120km/hr kwa maana kwamba kama kutoka Dar mpaka Moro ni kilomita 240 basi vyombo vyote vitatumia 2hrs kufika.

Inanikumbusha kg 1 ya pamba na kg 1 ya mawe kipi kizito
 
Kazi ya turbo ni ipi sasa.....?kuna gari kuna factor nyingi tu ndg haziwezi kwenda sawa hats siku moja ingawa umeeleza vzr....
Usichanganye mambo Mkuu. Kwani Gari kubwa zote zina turbo? Au Gari ndogo zote zina turbo? .

Swali la hapo juu, limeundwa kama maswali ya physics ya kipindi kile under ceteris peribus.

Labda nifafanue tena uzi kivingine:-
Hapa umeambiwa kuwa basi kubwa na pikipiki tayari ziko kwenye mwendo wa 120km/hr ( yaani mishale ya kwenye speed gauge ya pikipiki+basi kubwa inasoma 120km/hr). Hatuongelei zime anzaanzaje hadi kufikia 120.

Hapa Chukulia akilini kuwa pikipiki na basi kubwa vikimbie kwa constant speed ( yaani mishale ya speed meter isome same figure) under ceteris peribus kwa muda flani , utapata ngoma droo
 
Swali liko wapi hapa. Baada ya saa 1 pikipiki itakuwa imetembea umbali wa kilomita 120. Vilevile baada ya saa moja hilo basi litakuwa limetembea umbali wa kilomita 120.
 
Mbona sijaona jibu muhafaka hapa,Anko magu na ant ndalichako endeleeni kuwakazania madogo waipende sayansi,yaani waliocomment wote hapo juu wameshindwa yaani inaonyesha ni kiasi gani wabongo wanapenda sana mambo ya umbea na vitu virahisi rahisi,
 
Hii imenikumbusha miaka ya 90 mwalimu wetu aliingia darsani na kutuuliza
"Mzigo wa Kg 3 za unga na mwingine wa Kg 3 za mchanga, upi ni mzito kuliko mwingine?"

Wote tuliosema ni Mchanga,tulicharazwa viboko. Wengine walipoona tunachapwa kwa kusema mchanga ni mzito nao wakasema ni Unga,nao walilambwa vivyo hivyo.

Kumbe zina ulingano sawa bhanah! Sisi kwa ujinga wetu wa wakati huo tuliamini mchanga ni mzito kutokana na nature yake.
 
ACHA MASIHARA WEWE! CHOMBO SCANIA KAMA ZILE CITY BOY ULINGANISHE NA BOXER? PIKIPIKI HAFATI KWANZA MATAILI YA SCANIA NI MAKUBWA NA SPEED YAKE KUBWA
Ingawa jibu lako ni sahihi, lakini umejichanganya kwenye umaliziaji
 
Mbona sijaona jibu muhafaka hapa,Anko magu na ant ndalichako endeleeni kuwakazania madogo waipende sayansi,yaani waliocomment wote hapo juu wameshindwa yaani inaonyesha ni kiasi gani wabongo wanapenda sana mambo ya umbea na vitu virahisi rahisi,
Jibu muafaka ni kwamba swali halijitoshelezi, kasema kufika, je ni kufika wapi? je kama pikipiki safari yake mwisho ni kilometa 50 baada ya hapo na basi ni 100 si wa pikipiki atakuwa kafika anakokwenda kabla ya basi? na je kama basi liliondoka asubuhi pikipiki ikaondoka jioni yake? si basi litakuwa lilishafika safari yake? waliotoa majibu wote hawajafikiria kwamba je hivyo vyombo vimeanza safari pamoja? kutokea point moja? na destination point ni hiyohiyo au tofauti? La sivyo mwenye swali aliandike vizuri kwa ufafanuzi zaidi la sivyo hakuna jibu sahihi hapo
 
Elimu Elimu Elimu ni physics tu hapo hakuna uchawi,Zote zitafika sawa.

Na ni sawa ukienda sehemu ambapo hakuna gravity(g=9.8) yaani ni 0 ina maana ukiachia gunia la mahindi na changarawe kwenye height moja kwa mda mmoja vyote vitafika pamoja ingawa vina tungamo (mass) tofauti.
 
Back
Top Bottom