Zijue kanuni za usafirishaji kwa njia ya bajaji na pikipiki, 2010, kama zilivyorekebishwa mwaka 2017

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411
*ZIJUE KANUNI ZA USAFIRISHAJI KWA NJIA YA BAJAJI NA PIKIPIKI, 2010, KAMA ZILIVYOREKEBISHWA MWAKA 2017*
*Utangulizi*
Ndugu wasomaji,
Kama tunavyofahamu, usafirishaji kw anjia ya pikipiki na bajaji unaongozwa na sheria ndogo au kwa jina jingine kanuni ambazo zimetungwa na Waziri wa Uchukuzi chini ya Sheria ya Utoaji Leseni za Usafirishaji yaani Thre Transport Licensing Act. Tangu mwaka 2010 zimekuwa zikitumika kanuni zilizotungwa wakati huo na kutangazwa kwenye gazeti la serikali Na. 144 la mwaka 2010. Kanuni hizo zilifanyiwa marekebisho mwaka 2017 na kutangazwa kwenye gazeti la serikali Na. 419 la mwaka 2017. Lengo tutaangazia marekebisho yaliyofanywa kwa mujibu wa kanuni hizo mpya.
*Sheria ya Usafiri wa Bajaji na Bodaboda*
1. *Leseni Ya Usafirishaji*
Kila pikipiki au bajaji inayobeba abiria ni lazima iwe na leseni ya kusafirisha abiria kwa mujibu wa kanuni ya 4(1) ya kanuni za Bodaboda na Bajaji, 2010. Kutokuwa na leseni hii ni kosa linalostahili kuadhibiwa. Hii ina maana kwamba, bila kuwa na leseni hii ya SUMATRA huruhusiwi kubeba abiria kibiashara.
1.1. *Nani anatoa Leseni za Usafirishaji Kwa pikipiki na Bajaji*?
Mwenye mamlaka ya kisheria ya kutoa leseni hizo ni SUMATRA. Hata hivyo kwa mujibu wa kanuni ya 6 (kama ilivyofanyiwa marekebisho 2017) leseni hiyo inatolewa na mamlaka za miji, wilaya na majiji,) kwa niaba ya SUMATRA, ili mradi tu mwombaji amekidhi vigezo na masharti ya kanuni ya 5 na amelipa ad azote zinazotakiwa..

2. *Vigezo vya kupata leseni ya usafirishaji kwa bajaji na pikipiki*
Ili kuweza kupewa leseni ya usafirishaji kwa pikipiki na bajaji, mwombaji anatakiw akukidhi vigezo vifuatavyo kwa mujibu wa kanuni ya 5:
(a) Kadi origino ya usajili wa pikipiki au bajaji;
(b) Cheti origino cha ukaguzi (Vehicle Inspection report) wa bajaji au pikipiki kutoka polisi na kopi yake iliyoidhinishwa(certified copy)
(c) Ikiwa inayoomba ni kampuni, basi iwe na cheti cha usajili wa kampuni hiyo
(d) Maelezo kuhusu eneo unalotaka kufanyia biashara
*Zingatia*: Sharti la kuwa na bima, barua ya utambulisho tokma kwenye kijiwe au chama,leseni ya dereva na picha, na mkataba wa ajira yameondolewa.

3. *Masharti ya Leseni ya Usafirishaji kwa bajaji na pikipiki*
Kanuni ya 13 inaweka masharti anayotakiwa kuzingatia Msafirishaji kwa njia ya pikipiki au bajaji kama ifuatavyo:
(a) bajaji au pikipiki yake ikidhi viwango vilivyowekwa na TBS
(b) iegeshwe na kuendeshwa katika maeneo yaliyoruhusiwa na kuainishwa na mamlaka ya mji,jiji, manispaa au wilaya.
(c) bajaji kwaajili ya kubeba abiria lazima iwe na pleti namba nyeupe
(d) dereva wa pikipiki asibebe abiria Zaidi ya mmoja (mishikaki)
(e) bajaji isibebe Zaidi ya abiria watatu na dereva
(f) dereva awe msafi na kuwa na kitambulisho wakati wote
(g) dereva azingatie ukomo wa mwendo (speed limit) na wakati wote asizidi mwendo wa kilometa hamsini kwa saa (50kph)
(h) asibebe abiria Zaidi ya uwezo wa kubeba abiria ulioandikwa kwenye kadi yake
(i) dereva wa pikipiki avae helmeti yenye namba za utambulisho za pikipiki yake
(j) ahakikishe abiria aliyembeba amevaa helmeti wakati wote
(k) asitumie simu wakati wa kuendesha
(l) bajaji au pikipiki iwe na bima hai kulingana na idadi ya abiria inaowabeba
(m) dereva awe na leseni halali kwa daraja analotakiw akuendeshe bajaji au pikipiki.
(n) mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 9 asibebwe kwenye pikipiki peke yake kama abiria.
*Zingatia*: Sharti la bajaji kuwa na mikanda na kizuizi upande wa hatari limefutwa kwenye kanuni hizi.

4. *Masharti ya kupakia watoto*
1. Kanuni ya 14 inapiga marufuku pikipiki kupakia mtoto mwenye umri wa miaka tisa kushuka chini.
2. Kanuni 14(2) inaelekeza kuwa mtoto yeyote wa chini ya umri wa miaka tisa ake kwenye pikipiki akiw ana mtu mzima.
5. *Matendo yaliyokatazwa*
Kwa mujibu wa kanuni ya 15(1) ni marufuku kwa mmiliki au dereva wa pikipiki au bajaji kufanya lolote kati ya yafuatayo:
(a) Kutumia lugha mbaya na za matusi;
(b) Kwa makusudi kuwazuia watoa huduma wengine;
(c) Kuendesha kwa spidi Zaidi ili kushindania abiria;
(d) Kukatisha safari;
(e) Kuendesha huku dereva akiwa amelewa pombe au ametumia madawa ya kulevya;

kumbuka bodaboda zinaua nguvu za kiume kwakuwa ile mashine inapigwa joto siku nzima
 
Mbona hao bodaboda ndio wanatembea sana na watoto wetu na kuwajaza mimba na wao kukimbia
 
Back
Top Bottom