T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 13,927
- 47,182
Marekani huwa hana show off ya silaha. Tangu nizaliwe sijawahi ona popote Marekani anafanya military parade, wakati fulani niliwahi waza hivi wanajeshi wa Marekani wanajua kweli kupiga gwaride sawasawa kama North Korea, China, India na Russia wanavyojua.Nakwambia hivi siku ya kushehekea uhuru hapa ni maonyesho na ku test makombora hapa unakumbuka ile iliyo rushwa ikaenda kutua baharini pwani ya Carlifonia USA??
Na hapa tulizungumzia artillery systems na multiple rocket launchers sio nuclear missiles. Isitoshe Marekani haina mobile nukes kwenye maroli. Sio strategy yao badala yake wanazo nuclear attack submarines za Ohio class zipo 14 na kila moja inabeba nuclear missiles 24 za Trident II. Hizo ndio hukaa majini zikifanya shift muda wowote 24/4 zinasubiri yeyote ajichanganye. Urusi anazo Borei na Typhoon class zinabeba makombora mengi pungufu kidogo ya Ohio. Alafu sio lazima uwe na makombora mengi ya nyuklia, vita ikitokea hayatotumika mengi hivyo. Mradi uwe na survivability yake kubwa.