Mizigo yapungua bandari ya DSM

Mizigo yapungua bandari ya DSM

WAKATI Mamlaka ya Bandari (TPA) ikithibitisha ufanisi katika upakuaji na uondoshaji mizigo na usalama wa mali katika Bandari ya Dar es Salaam, imebainika idadi ya mizigo katika bandari hiyo, imepungua tofauti na matarajio.

Akizungumza wakati akifunga warsha ya Wahariri wa Habari mwishoni mwa wiki, Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Hebel Mhanga, alitoa mfano wa shehena ya magari yanayokwenda Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC).

Kwa mujibu wa Mhanga, shehena ya magari yanayokwenda katika nchi hiyo kutoka Januari 2015 mpaka Januari 2016, imepungua kwa asilimia 50 huku shehena ya Zambia ikipungua kwa asilimia 46. Beira Mhanga alisema walipochunguza sababu ya kupungua kwa shehena hizo, walibaini sehemu ya shehena hiyo hasa iliyokuwa ikienda Zambia, DRC na Malawi, inashushwa katika Bandari ya Beira nchini Msumbiji.

Sababu za kushushwa katika Bandari ya Msumbiji, badala ya Bandari ya Dar es Salaam ambayo ndiyo yenye unafuu wa umbali kutokana na jiografia yake, Mhanga alisema ni unafuu wa kusafirisha shehena hiyo kwa reli ya Beira mpaka Malawi, tofauti na ilivyo kwa barabara.

Alisema usafirishaji wa reli ni nafuu kwa asilimia 30, ikilinganishwa na usafirishaji wa barabara na kwa kuwa Msumbiji wameshakamilisha ujenzi wa reli ya kisasa, wafanyabiashara wameona unafuu wa kupitisha mizigo katika Bandari ya Beira kuliko ya Dar es Salaam.

Athari hiyo katika Bandari ya Dar es Salaam, huenda ikawa mbaya zaidi baada ya kukamilika kwa reli ya kisasa inayoanzia katika Bandari ya Mombasa mpaka DRC, kwa kuwa itaongeza unafuu wa usafirishaji wa mizigo katika bandari hiyo shindani kwa Tanzania.

Katika warsha hiyo, ilifafanuliwa kuwa dunia nzima bandari zimekuwa na mafanikio, kutokana na kuwa na mfumo wa reli za kisasa unaotoa mizigo bandarini na kufikisha kwa mteja, jambo linalokosekana katika Bandari ya Dar es Salaam.

Durban Shehena nyingine iliyokuwa ikipitia nchini, imebainika kupelekwa katika Bandari ya Durban nchini Afrika Kusini kutokana na unafuu uliotokana na matumizi ya fedha ya nchi hiyo, Rand, katika utozaji wa gharama za kutoa mizigo, tofauti na Tanzania ambako gharama hutozwa kwa Dola ya Marekani.

Akifafanua hali hiyo, Mhanga alisema kwa sasa Rand imeshuka thamani na hivyo mfanyabiashara mwenye Dola ya Marekani, atatumia Dola chache za Marekani kulipia tozo hizo kwa Rand ya Afrika Kusini iliyoporomoka thamani.

Kutokana na hali hiyo, ingawa gharama za utoaji mizigo kati ya Bandari ya Dar es Salaam na Bandari ya Durban zinalingana, lakini mfanyabiashara akipitisha mzigo Afrika Kusini, atatakiwa kubadilisha Dola ili apate Rand ya kulipa gharama hizo; na kwa kuwa Rand imeporomoka thamani, atatumia Dola chache kuliko ilivyo kwa Tanzania.

Utambuzi wa mizigo Changamoto nyingine aliyotaja Mhanga ni ya mfumo wa kutambua shehena zilizoko katika meli, unaotumiwa kukadiria gharama za utoaji wa mizigo bandarini pamoja na kodi. Akifafanua, Mhanga alisema mzigo unapopakiwa katika nchi unakotoka, mpakiaji anapaswa kueleza aina ya mzigo katika fomu maalumu ya kutambulisha mzigo.

Fomu hiyo inayojazwa na mpakiaji, ikifika Dar es Salaam kabla ya kupakua mzigo, hutumiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kukadiria kodi. Hata hivyo Mhanga alisema fomu hiyo inapokosewa na mpakiaji, TRA wakati wa kuhakiki mzigo huhisi harufu ya ukwepaji kodi na hivyo utaratibu wa utoaji wa mzigo husika, huchukua muda kuliko kama fomu hiyo isingekosewa.

Mhanga alisema wakati utaratibu wa kurekebisha makosa hayo ya fomu ukichukua muda mrefu kabla ya kuruhusiwa na TRA, mzigo huo huchajiwa adhabu ya kukaa bandarini kwa muda mrefu na kama ni wa nje ya nchi, mteja hulazimika kukaa Dar es Salaam kwa kosa lililofanywa na mpakiaji wa mizigo.

Meneja huyo wa Bandari ya Dar es Salaam, alisema mteja huyo anaporuhusiwa na TRA kuchukua mzigo, wakati ameshaingia gharama ya kuishi Dar es Salaam kwa muda mrefu, akifika bandarini na kukutana na adhabu ya kuhifadhi mzigo ambayo hakuisababisha, wengi hukasirika na hajui wanapeleka ujumbe gani kwa wateja wengine katika nchi zao.

Ufanisi Pamoja na changamoto hizo, Mhanga alisema kama wadau wengine wakikamilisha taratibu za ukaguzi wa mzigo mapema, mzigo huchukua muda mfupi kupakuliwa katika meli na kuondolewa mapema bandarini, ili umfikie mteja katika muda mfupi zaidi.

Alitoa mfano wa mwaka 2011, ambapo mteja alitumia siku 4.7 kusubiri mzigo wake utoke bandarini, lakini leo mteja huyo huyo atasubiri siku 0.2 mpaka apate mzigo wake na hilo limesababishwa na uboreshaji wa utaratibu wa kupata vibali vya nyaraka, ambao kwa sasa unafanyika kwa mtandao.

Mhanga alisema bandari hiyo kwa sasa inakamilisha ujenzi wa jengo la ghorofa 35, ambalo litakuwa refu kuliko yote Afrika Mashariki na Kati, litakalohifadhi wadau wote wa bandari katika jengo moja, ili mteja akiingia katika jengo hilo, akitoka akatoe mzigo wake moja kwa moja.

Kwa sasa mteja anaweza kujikuta akihangaika na nyaraka zake kwa wadau mbalimbali wa Bandari ya Dar es Salaam kupata vibali, ikiwemo Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchikavu (Sumatra), Shirika la Viwango (TBS), Mamlaka ya Dawa na Chakula (TFDA), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Idara ya Uhamiaji, Idara ya Afya, Mkemi Mkuu na wengineo
wacha porojo labda wewe ni wale wakala wa kutoa mizigo waliyofungiwa kwa utapeli wenu. mbona husemi kama mapato ya serikali yameongezeka kiasi gani. sifa kuu ya bandari ni kiasi cha mapato yanayopatikana kama ushuru. wingi wamizigo iwe kiashirio cha ufanisi na mapato. mizigo inaweza kupungua kutokana na wale waliyokua wanapitisha mizigo bila kulipa ushuru wa serikali kutimka. hata hivyo hii taarifa ni porojo kwani taarifa rasmi ni kwamba mapato ya ushuru yameongezeka sana na msangamano bandarini umepungua.
 
saa izi Wazimbabwe wanakuja kuchukua magari wenyewe hapo Trafiki wanawafanya dili njia yoote hiyo toka dar mpaka tunfuma wanataka rushwa kwa dola wakikimbia mnaanza wamejenga reli wakati sisi wageni katika bara bara zao hatusumbuliwi labda awe amekuja Tanzania ndio atataka rushwa kwa jinsi aluvyosumbuliwa bara barani gari inatoka unaisimamisha unataka nini zaidi...
 
Ok, vipi kuhusu mapato nayo yamepungua au yamepanda?
 
Mimi sababu ya msingi ni za kiujanjaujanja tu mfano bandari ya BEIRA malawi kuna haikuwepo mwanzon kwa nin sasa waone ndio yenye unafuu , nimegundua bandari ya daa ilikuwa inaficha sana wakwepa kodi wengi sana na kwa sasa hiyo mianya imebanwa
wanasifia tu bandari za nje kama kasuku hata hawajui zina hali gani. huko kwingine unaweza kukuta walikua wanasifia bandari ya dsm wakati ikiwa shamba la bibi.
 
Wabongo kwa visingizio hatuna mfano. Hapa hakuna uchawi...jaribu kuleta mzigo bandarini Dar uone huo urasimu...kama mtu ana option kwa nini asikimbie? Mnasingizia wenye malori? Serikali na wenye malori nani mwenye nguvu ni uamuzi na nia tuu. Kwa jinsi tulivyozungukwa na nchi zisizo na bahari treni na malori yanaweza share biashara vizuri tuu tena nchi ndio inafaidika mara mbili kutoka kwenye malori na kwenye treni. China na marekani kuna treni kila mahali lakini bado kuna maelfu ya malori yanabeba mizigo.
 
wacha porojo labda wewe ni wale wakala wa kutoa mizigo waliyofungiwa kwa utapeli wenu. mbona husemi kama mapato ya serikali yameongezeka kiasi gani. sifa kuu ya bandari ni kiasi cha mapato yanayopatikana kama ushuru. wingi wamizigo iwe kiashirio cha ufanisi na mapato. mizigo inaweza kupungua kutokana na wale waliyokua wanapitisha mizigo bila kulipa ushuru wa serikali kutimka. hata hivyo hii taarifa ni porojo kwani taarifa rasmi ni kwamba mapato ya ushuru yameongezeka sana na msangamano bandarini umepungua.
Huoni aibu? Hayo maneno kayatoa meneja wa bandari... au ni uvivu wako wa kusoma unacomment bila kusoma habari?

Hizi division five kweli majanga
 
Tanga kuna reli imekufa, yaani wangefanyia ukarabati reli ya tanga ingeshindana na mombasa since sipo karibu , lakini serikali inawekeza dar es salaam tu...
Mkuu Tanzania ni Nchi ya ajabu Yaani wao Akili zao zote wamezielekeza Dsm kila Mbunge kahamia Dsm wakuu wa wilaya, mikoa nk wote ni wakazi wa Dsm huko wapo kikazi tu, hii dhana ya kulundikana mji mmoja ni ya Ajabu na kijinga sana , maendeleo hayapanuki , ilipaswa tuwe na Bandari kubwa nne au zaidi , kila Bandari iwe maalum Kwa kitu Fulani , mfano kule Afrika kusini kuna Bandari nyingi kubwa na kila moja ina kazi yake, Bandari ya Darban ni maalum Kwa mizigo ya Nchi Jirani , kule pot Elzabeth ni maalum Kwa mizigo ya ndani pia Bandari za east London na capetown , Tujifunze huko Bandari ya mtwara iwe maalum Kwa mizigo Fulani ya tanga pia na hii ya Dsm iwe ya Nchi Jirani nk .
 
Sie huku reli inaoza, vichwa vya tren vipo karakana, mkurugenzi kasinzia tu shirika linakufa taratibu
Kwa miaka mingi Tanzania imetesa wateja wake wa bandari na sasa hayo ndio malipo. Wakati tunawatesa wajanja walikesha wakipanga namna ya kuwaponya kwa kwatafutia mbadala. Ndio hapo reli ya Beira malawi kujengwa na sasa reli ya Mombasa DRC Congo inajengwa. Hicho tayari ni kitanzi kwetu kilichosababishwa na awamu zilizopita. Kweli sikio la kufa halisikii dawa.
 
Wabongo kwa visingizio hatuna mfano. Hapa hakuna uchawi...jaribu kuleta mzigo bandarini Dar uone huo urasimu...kama mtu ana option kwa nini asikimbie? Mnasingizia wenye malori? Serikali na wenye malori nani mwenye nguvu ni uamuzi na nia tuu. Kwa jinsi tulivyozungukwa na nchi zisizo na bahari treni na malori yanaweza share biashara vizuri tuu tena nchi ndio inafaidika mara mbili kutoka kwenye malori na kwenye treni. China na marekani kuna treni kila mahali lakini bado kuna maelfu ya malori yanabeba mizigo.
China na marekani sheria zinafuatwa na hukana magumashi ni vigumu kulinganisha hizo Nchi na Tanzania ambapo kila jambo linawezekana Kwa mwenye pesa.
 
Mkuu Bandari ya DSM ina mapungufu mengi kuliko Bandari zote huku Afrika na kero kubwa zaidi ni Foleni ya Meli kuingia bandarini huchukua mpaka siku 40 au zaidi , pili usumbufu na kutokuwa na mpangilio wa Ofisi za kuwashughurikia wateja, tatu uzembe wa makusudi ili mizigo iingie kwenye storage wapate pesa Kwa njia haramu , nne kuacha kutumia Reli makusudi ili kuwanufaisha Wamiliki wa Magari makubwa ya mizigo na mafuta . Hayo ni baadhi ya magumashi na kero lakini Kwa ujumla kuna kero nyingi sana.
Bado uko zama za kale? Hivi sasa hakuna meli inayosubiri O/A kwa zaidi ya siku mbili. Fanya utafiti kabla hujakurupuka
 
Hakuna namna serikali lazima iwekeze kwenye reli ,sasa sijui watatumia pesa zipi ,za pato la ndani au Wahisani ??
 
Hizo ni changamoto serikali ikijipanga inaweza kuzitatua, tumelala sana kwa sababu sisi ni wazuri kwenye plan na strategy ikifika kwenye utekelezaji ni zero, mfano reli toka dar- Bujumbura-DRC ilikua ijengwe tangu enzi za kikwete lakini hadi sasa hakuna kinachoendelea. Kenya kwa kuona hiyo fursa ambayo wameicopy toka hapa TZ tayari wanajenga reli. Labda tusubiri hii awamu huenda ikafanya kitu ingawa tutakua tumechelewa.
KWANINI HUSEMI INGEKUWA ISHAJENGWA TANGU KIPINDI CHA NYERERE?
 
Waafrika kujiendesha ni kazi sana, tunahitaji kuja kuwekewa mfumo wa kuendesha kuanzia serikali kuu mpk tawi. Hapa kumewekwa visingizio vingi ikiwemo cha watoza huduma kuwa sehemu tofauti. Hii sio hoja hata mkiwa pamoja Ni vigumu kuweza kuisaidia Tanzania. Waafrika mumeshindwa kiufanisi Na kiutendaji. Uzembe huu mlikua munaujua miaka yote 50 lkn hamkuweza kurekebisha Leo mnakuja kulalamika.
tuchane tu Mhindi, maana tumezembea kweli
 
12512792_1392231797470770_5533159620618514600_n.jpg
Loh! hii sasa ni mwisho wa somo mpaka miti imeota katikati ya reli, a very Good nite to us.
 
Bado uko zama za kale? Hivi sasa hakuna meli inayosubiri O/A kwa zaidi ya siku mbili. Fanya utafiti kabla hujakurupuka
Wewe ndiyo umekurupuka ukiona Meli imewahi ujue wametoa Rushwa , endelea kutetea maovu Nchi uendelee kuteketea .
 
Wenzetu wanajenga reli za kisasa wao wanaagiza mabewa feki huku wanasiasa wakipeta kwenye hizi kashifa.
 
tatizo kuna watu wanaandika wakiwa na hasira zao kuhusu yaliyotokea zanzibar....na wanatamani kila leo tuongelee hayo kama vile demu aliyeachwa anavyotamani mida yote muongelee habari za huyo mpenzi wake!
nakubaliana na aliyesema mambo ya ki fisadi ndiyo yaliyokuwa yakishamirisha mizigo mingi ya nchini ifike bandarini....deal zimekatwa basi watu hawana hela.
kuhusu mizigo ya zambia...drc...ukweli ni kwamba ukwepaji kodi haukuwa kwa watanzania tu...

nasikia waoaji bandarini mizigo toka nchi zote...tanzania..zambia...malawi...drc walikuwa wanapenda kukwepa kodi kwa kudanganya wapi mzigo unaenda...

eg...mtanzania anasema hili gari linaenda zambia
..hihihhhi
ok wapo watu kama hao, ila na wewe una upofu kutokana na ushabiki wako kwa magufuli, taarifa imetolewa na afisa wa bandarini na inaanzia January 2015 hadi January 2016, huo ni mwaka mzima mizigo imekua ikipungua, utawala wa magufuli una miezi 4, na afisa huyo katoa sababu kuu kwamba ni kutokana na urahisi unaopatikana kwingine...
jaribu ku reason sio kuandika mipasho
 
Back
Top Bottom