Asa'rile
JF-Expert Member
- Jun 29, 2012
- 438
- 120
Kweli ilkuwa kama 'Movie' vile. ilikuwa ni jana tu, around saa mbili usiku, nikiwa maeneo ya Ubungo-Kibo, Dar es Salaam, Tulisikia kwanza pilikapilika za misafara ya wazito- Vingora vikali vya 'kusafisha njia' na pia kuweka mazingira ya usalama, vilisikika kutokea Kimara -Baruti kuelekea kituo cha Kona, Ving'ora na mbwembwe za msafara viliongeza kasi zaidi kuelekea Ubungo-Rombo.
(Kwa taarifa tu ni kwamba wajenzi wa barabara hii- wamefunga njia mbili, na kuruhusu moja tu kwa waendao town na kurudi). Haya, msafara wa kizito wetu huyo ukatiririka na kuishia Ubungo Kibo, ilipoanzia foleni hiyo, hadi kwenye 'Mataa!!'
Ving'ora vimeunguruma mpaka Betri zimeisha bila mafanikio. malori ya makontena na daladala hazikuweza kupisha msafara huo, maana pembezoni mwa barabara zimeinuliwa kingo ndefu zinazozuia magari ya upande mmoja kwenda njia nyengine.
sasa ilibidi wale Ma-FFU waruke na kwenda kui-Guard gari ya mweshimiwa upande huu na huu, kama ile dizaini ya Obama vile, Bonge la Movie
Lisaa lizima