Mizengo Pinda akwama kwenye foleni Ubungo-Kibo lisaa lizima, usiku!!

Asa'rile

JF-Expert Member
Jun 29, 2012
438
120
Kweli ilkuwa kama 'Movie' vile. ilikuwa ni jana tu, around saa mbili usiku, nikiwa maeneo ya Ubungo-Kibo, Dar es Salaam, Tulisikia kwanza pilikapilika za misafara ya wazito- Vingora vikali vya 'kusafisha njia' na pia kuweka mazingira ya usalama, vilisikika kutokea Kimara -Baruti kuelekea kituo cha Kona, Ving'ora na mbwembwe za msafara viliongeza kasi zaidi kuelekea Ubungo-Rombo.

(Kwa taarifa tu ni kwamba wajenzi wa barabara hii- wamefunga njia mbili, na kuruhusu moja tu kwa waendao town na kurudi). Haya, msafara wa kizito wetu huyo ukatiririka na kuishia Ubungo Kibo, ilipoanzia foleni hiyo, hadi kwenye 'Mataa!!'

Ving'ora vimeunguruma mpaka Betri zimeisha bila mafanikio. malori ya makontena na daladala hazikuweza kupisha msafara huo, maana pembezoni mwa barabara zimeinuliwa kingo ndefu zinazozuia magari ya upande mmoja kwenda njia nyengine.

sasa ilibidi wale Ma-FFU waruke na kwenda kui-Guard gari ya mweshimiwa upande huu na huu, kama ile dizaini ya Obama vile, Bonge la Movie
Lisaa lizima
 
Ni vizuri kuyagawana matatizo ya wananchi wa vitendo na si majukwaani tu. mkuu Pinda hii ndiyo adha ya watu wa Kimara wanayoipata takribani kila siku asubuhi na Jioni.

Hata sisi wa kigamboni matatizo ya kivuko ni balaa, kwa mfano siku ya Ijumaa ilikuwa Zahma, Pantoni kubwa wakaliegesha saa nne wakati foleni ipo Ikulu bila kututolea sababu za msingi, likabaki lile dogo linalochukua magari si zaidi ya 20, ilipofikika saa sita usiku ikabidi rushwa ianze kutembea tembea pale ferry!! mida ya saa nane kasoro wananchi uzalendo ukawashinda wakachichukulia madaraka mikononi kwa kufungua mageti yote, sasa muziki ikawa kugombea kuingia kwenye ki-pantoni.

Nchi hii ukiamua kuyajadili matatizo yake basi unaweza kupata u-docta , maana ni mengi kila pande!!
 
Hakika nampongeza Waziri Mkuu Pinda kwa kushare maumivu ya foleni na wakazi wa Dar. Hakika huyu ndiye kiongozi tunayemuhitaji
 
Hakika nampongeza Waziri Mkuu Pinda kwa kushare maumivu ya foleni na wakazi wa Dar. Hakika huyu ndiye kiongozi tunayemuhitaji

unampongeza kwa lipi alishindwa kupita kwa sababu hakukuwa na uwezekano wa kupishwa. sio kwamba alipenda ili aone adha ya usafiri wa wananchi wake.
 
mimi nakaa Kimara Suka nina Mwezi sasa naacha gari nyumbani nimeshindwa ku afford cost za mafuta, maana unaweza kutumia saa 1 toka Suka hadi Kimara Mwisho kwa kifupi huku ni Jehanamu.
 
Mkuu Pinda isije ikawa ndiyo fitna hizo zimeanza taratibu taratibu kuelekea kukunyanganya ka-tonge mdomoni.
 
Barabara ya ubungo haifai kabisa foleni masaa 3. hawa wajenzi wanafanya makusudi kuumiza watu kwanini wasijenge njia muda?
 
mimi nakaa Kimara Suka nina Mwezi sasa naacha gari nyumbani nimeshindwa ku afford cost za mafuta, maana unaweza kutumia saa 1 toka Suka hadi Kimara Mwisho kwa kifupi huku ni Jehanamu.
Pole sana Mkuu, jaribu kuvumilia maumivu kwani hakuna maendeleo yasiyo na karaha
 
Barabara ya ubungo haifai kabisa foleni masaa 3. hawa wajenzi wanafanya makusudi kuumiza watu kwanini wasijenge njia muda?
Mkuu, hawafanyi makusudi. Tatizo ni kuwa hakuna njia mbadala kwani zilizopo hazijaboreshwa. Hayo yaliwakuta sana watu wa Mbagala wakati barabara ya Kilwa inajengwa.
 
Back
Top Bottom