Jeshi la polisi pangeni matrafiki wanaojua mwenendo wa foleni Ubungo

kerubi afunikaye

JF-Expert Member
May 20, 2013
1,147
2,000
Natoa wito kwa jeshi la polisi kupanga matrafiki wanaopajua vizuri Ubungo.Foleni ya magari katika njiapanda ya Ubungo inahitaji uelewa wa wapi magari mengi yanatoka na kuelekea wapi kulingana na muda.Kuna askari wanaowekwa ambao inaonekana hawapaelewi vizuri utakuta mtu kang'ang'ania kuvuta magari ya upande mmoja ambao hauna foleni na kuacha wenye foleni.Mfano ni leo ambapo kuna foleni kubwa ya magari yanayoelekea mjini kutoka kimara ambayo imeanzia Ubungo hadi maeneo ya korogwe na inasogea taratibu mno.Mie nimekaa pale saa nzima ndio nimevuka wakati huu na nilipofika njia panda huyu trafiki katusimamisha na kuanza kuvuta magari yatokayo Mwenge hadi yakaisha na kuanza kuja moja moja lakini bado aling'ang'ania upande huo kwa dk 10.Alipomaliza akaruhusu upande wa magari yatokeayo buguruni ambapo kwa kawaida upande huu matrafiki wazoefu huufanya wa mwisho kutokana na kujaa malori mengi ambayo ukiwahi kuyaruhusu yakakaa mbele ya msafara yanaleta foleni kwa mwendo wake wa taratibu.Huwa yanaruhusiwa machache baada ya kumaliza njia nyingine zenye magari yaendayo haraka.Jamaa aliendelea kuvuta malori mpaka trafiki mwingine akaja na kumwelekeza aanze kuvuta upande wetu na wa magari yatokayo mjini ambayo ni mengi zaidi.Kuna jamaa yangu kanipigia anasema foleni imefika kimara resort.Jamani jeshi la polisi hebu tupangieni matrafiki "watoto wa mjini" wanaojua mji huu.Hawa wakuja wapelekeni mikoani huko mtupunguzie kero.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom