Mizengo Pinda akwama kwenye foleni Ubungo-Kibo lisaa lizima, usiku!!

Safi sana! Tumekuwa tukilalamika siku zote kuhusu huyu mkandarasi kutotengeneza diversion kwenye hii barabara lakini hatusikilizwi.
 
Sijaelewa ujumbe wa Pinda kupiga picha akiwa amepanda pikipiki (bodaboda) iliyo simama juu ya stand zake!
 
sijawahi kuwa comfotable na zile kingo jinsi zilivyoinuliwa kwenye ile barabara. unless wabadilishe aisee. foleni siku itakuja kufika kimara mwisho
 
Ndio atakapofahamu ubaya wa ubabe was magufuli kuuingilia mchakato was resettlement actio plan ya Benki ya dunia na kumuingiza mkandarasi site kwa pupa pasipo tanesco na dawasa kulipwa fidia ili waondoshe miundo mbinu yao na kumuwezesha mkandarasi kupata sehemu ya kutengeneza diversions
 
Pole sana Mkuu, jaribu kuvumilia maumivu kwani hakuna maendeleo yasiyo na karaha

hii si karaha ni upu..mb.avu, kwa nini njia za mbadala hazikujengwa kabla ya kuanza huu mradi usio na tija!!!! nimefurah kusikia pm kaonja nini maana ya ujenzi duni wa hao strabag
 
sijawahi kuwa comfotable na zile kingo jinsi zilivyoinuliwa kwenye ile barabara. unless wabadilishe aisee. foleni siku itakuja kufika kimara mwisho

Yah..mkuu hata me nilikuwa najiuliza siku itokea gari likaharibika itakuwaje na pembeni kuna kingo?
 
Ahamie Dodoma kwani Nyerere alijua ipo siku jiji litafurika magari ya mikopo ya akina dada na magari ya nyumba Ndio Maana akataka wahamie Dodoma lakini wamegoma wanabanana jijini matokeo yake wabunge wote Nchi nzima wanaishi Dsm yaani ni kioja Duniani Nchi zingine wabunge wanaishi huko huko majimboni kwao
 
Tz kila mtu anataka kuishi Dsm sijui ni kwa nini?dodoma kumeshindikana kuhamia sasa ni bora wahamie Moro au Tanga ili kulinusulu jijji na msongamano huu
 
Tusiingilie taaluma za watu mitandaoni humu kama wapumbavu..

Kama unaona kuna kitu wanakosea ni bora kwenda mahakamani kuwashtaki, hivi vitu vipo kwenye mikataba na hakuna maendeleo yanayokuja bila maumivu..

Hata marekani tunayoiona nzuri sana leo napo watu waliumia na kulalamika sana wakati maendeleo yanawekwa..

Germany wanasifiwa kwa miundominu mizuri sana na sana, watu waliumizwa sana kipindi cha Hitler ili miundombinu hiyo ikamilike..

STRABAG sio wehu, na BRT Tanzania sio kazi yao ya kwanza na hata waliowapa Contract sio wapumbavu na huu mradi hawakupeana kirahisi kama kupeana namba na mademu Bar..

Soma mabango ya Strabag utaelewa namaanisha nini, World Bank, SMEC, IBRD na Brand nyinginezo wengi zilizopo kwenye mabango ya Strabag sio wajinga kuwasapoti Strabag..

Mfano hai ndio huu waziri mkuu mizengo Pinda kawekwa kwenye foleni na halalamiki maana anajua STRABAG ni kina nani na wamekuja kufanya nini? Na hakuna kiongozi wa Tanzania ataeweza kufanya chochote maana hii sio politics ni Taaaluma na watu wapo kazini na wanajua wanachokifanya


Acha vitisho wewe hata SAP ina baraka za IMF na WB haya sema faida zake!!!!!!
Mradi mzuri lazima uwe efficient na effective tangu wakati wa implementation sio kuangalia end product tu!!!!!!


Kama wamekutuma waambie siku hizi tunajua na.tunaweza kisema kiwa "hiki sio sawa" hata kama kimeletwa na UN achilia mbali hizo label unazopigia kelele!!!!!

Hata kuua ni profession sasa ulikuwa unataka kusemaje kuhusu hili kwa kuingiza majina ya watu na vyeo???!!!
Kama walikuwa na utaalamu huo hii tabu isingekuwepo kwa watumiaji wa hiyo njia! !!!!!!!
Unaweka mifano ya Hittler zama hizi??!!!!!Mbona we husafiri kwa miguu na punda kama zamani???!!!
 
Kweli ilkuwa kama 'Movie' vile. ilikuwa ni jana tu, around saa mbili usiku, nikiwa maeneo ya Ubungo-Kibo, Dar es Salaam, Tulisikia kwanza pilikapilika za misafara ya wazito- Vingora vikali vya 'kusafisha njia' na pia kuweka mazingira ya usalama, vilisikika kutokea Kimara -Baruti kuelekea kituo cha Kona, Ving'ora na mbwembwe za msafara viliongeza kasi zaidi kuelekea Ubungo-Rombo.

(Kwa taarifa tu ni kwamba wajenzi wa barabara hii- wamefunga njia mbili, na kuruhusu moja tu kwa waendao town na kurudi). Haya, msafara wa kizito wetu huyo ukatiririka na kuishia Ubungo Kibo, ilipoanzia foleni hiyo, hadi kwenye 'Mataa!!'

Ving'ora vimeunguruma mpaka Betri zimeisha bila mafanikio. malori ya makontena na daladala hazikuweza kupisha msafara huo, maana pembezoni mwa barabara zimeinuliwa kingo ndefu zinazozuia magari ya upande mmoja kwenda njia nyengine.

sasa ilibidi wale Ma-FFU waruke na kwenda kui-Guard gari ya mweshimiwa upande huu na huu, kama ile dizaini ya Obama vile, Bonge la Movie
Lisaa lizima

Nilishuhudia spika pia aliwahi kukwama maeneo ya rombo
 
Barabara ya ubungo haifai kabisa foleni masaa 3. hawa wajenzi wanafanya makusudi kuumiza watu kwanini wasijenge njia muda?

Labda mkataba hausemi hivo!!!!! Si wajua twenty percent mh!? Sijui ten percent watajua wenyewe:D:D:D:D:confused::confused::confused:
 
TANROADS ndio walipasa kusimamia ili kuhakikisha ujenzi katika barabara inayoendelea kutumika unafanyika ukiwa na madhara machache pande zote. Kumsimamisha waziri mkuu saa nzima barabarani siyo sifa hata kidogo, si kwa waziri mkuu au mtu yeyote...
 
Back
Top Bottom