Sehemu ya barabara ya Ubungo mataa Dar kufungwa kesho na keshokutwa usiku kupisha ujenzi

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
unnamed.gif


KAMPUNI ya ujenzi ya Strabag International GmbH inayojenga barabara ya Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) imetangaza mabadiliko ya muda katika eneo la Ubungo jijini Dar es salaam kuanzia kesho na kesho kutwa usiku kutokana na ujenzi unaoendelea wa barabara.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Bwana Yahya Mkumba, alisema kazi hiyo itahusu ujenzi katika makutano ya barabara za Morogoro, Sam Nujoma na Nelson Mandela katika eneo la Ubungo.

Alisema ujenzi huo utakaoanza leo utasababisha kufungwa kwa baadhi ya njia katika barabara hizo kuanzia saa nne usiku hadi saa 12 asubuhi Jumamosi.

Akielezea zaidi alisema katika awamu ya kwanza ujenzi huo utahusisha eneo la upande wa kulia la makutano la barabara ya Sam Nujoma na Morogoro ambalo litafungwa.

"Hali hii itasababisha magari yanayotoka maeneo ya Buguruni na Tabata kuelekea maeneo ya Mwenge kutoweza kutumia njia ya Sam Nujoma watakapofika taa za Ubungo," alisema.

Alifafanua kuwa magari hayo yatalazimika kufuata alama zitakazowaelekeza kupita katika barabara za mradi zinazojengwa hadi barabara ya Shekilango ambapo wataweza kukutana tena na Sam Nujoma kwa kutumia barabara ya Igesa.

Pia magari yatakayokuwa yanatokea Sinza kupitia barabara ya Igesa hayataweza kuelekea eneo la Ubungo yatakapofika katika makutano ya barabara za Igesa na Sam Nujoma.

Alifafanua kuwa magari yanayotumia barabara ya Morogoro kutokea maeneo ya Mbezi na Kimara yatalazimika kuchepuka kulia na kutumia barabara za mabasi ya mwendo wa haraka yatakapofika eneo la Kibo ambapo patakuwa na kizuizi.

Bw. Mkumba alisema katika awamu ya pili ya ujenzi huo, eneo la upande wa kushoto la makutano ya barabara za Morogoro na Nelson Mandela litafungwa siku ya Jumamosi kuanzia saa nne usiku hadi saa 12 asubuhi siku ya Jumapili.

Katika awamu hii, alisema, watumia magari yatakayokuwa yanatokea eneo la Mwenge kutumia barabara ya Sam Nujoma yatalazimika kuchepuka kushoto kukamata barabara ya Igesa kisha Shekilango.

Pia magari yatakayokuwa yanatokea barabara ya Nelson Mandela na kutaka kuelekea mjini kwa kutumia njia ya Morogoro yatalazimika kuchepuka kushoto na kwenda kugeukia eneo la Kibo ili kuikamata barabara ya Morogoro.

"Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaotokea," alisema Bwana Mkumba na kuongeza kuwa pamoja tunajenga na hivyo usumbufu utakuwa ni wa muda mfupi.

Mradi wa Mabasi yaendayo haraka unatarajiwa kuondoa adha ya foleni katika jiji hilo na kuleta ufanisi wa usafiri.
 
Mkuu, hii habari ya lini? Mbona kesho sio Jumamosi? Au ni habari ya gazeti iliyotakiwa itoke kesho
 
sitaki kushuhudia huo usumbufu wa foleni...yaan dar inachosha sahizi..
 
Ubungo Tabata Diversion

NELSON MANDELA RdSAM NUJOMA Rd
M OR O G OR OR d M OR O G OR OR d
SAM NUJOMA Rd
ROAD BLOCKED BETWEEN10:00pm & 06:00am
SHEKILANGO Rd
I GE S AR d
UBUNGO JUNCTIONCONSTRUCTION PHASE 1
UTURN KIBO
u n d e r c o n s t r u c t i o n
ROADBLOCKEDROADBLOCKED
Public Service AnnouncementTraffic Diversion Ubungo Junction
We Are Building For You
Strabag International GmbH and all concerned parties would like to informthe general public and the users of Morogoro road that due to the on goingconstruction, traffic using the Ubungo Junction from Tabata will be askedto divert in to the concrete lanes as shown in the above sketch,from20th June 2014 10:00pm to 21st June 2014 06:00am.Please bear with us as we build for you the Bus Rapid Transport System
key
Road BlockedVehicles asked to Divert


1-ec0f5fd547.png







Barabara itafungwa kwa muda, sijui kama nime- capture vizuri make watu wengine computer sio fani zetu!
 
Leo basi itakuwa ni taabu kufika town kuanzia mida hiyo.

Ila ajabu, barabara hiyo especially kwenye makutano ya ubungo imefungwa muda sasa kama zaidi ya mwaka, huku madari yakipita kwa shida sana, mi naona wahusika wanafurahi wanavyo ona wakazi wa maeneo hayo wakipita kwa shida, mpaka kukawepo na uvumi kwamba dereva wa boda boda wanachangishana pesa na kuwapa matrafic wanao ongoza magari kutengeneza foreni kwa makusudi, huku baadhi ya njia zikiwa zimefungwa bila kutumika kwa muda mrefu na bila sababu za ki ufundi.
 
Watafunga kuanzia saa4 usiku Wa Leo na kesho pia!

Habari hii pia iko kwenye magazeti ya Leo karibu yote!
 
ubungo.jpg

KAMPUNI ya ujenzi ya Strabag International GmbH inayojenga barabara ya Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (Dart) imetangaza kufungwa kwa baadhi ya njia katika eneo la taa za Ubungo, Dar es Salaam kuanzia leo usiku hadi keshokutwa kwa ajili ya kuruhusu ujenzi.



Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Uhusiano wa Dart, Yahya Mkumba, alisema kazi hiyo itahusu ujenzi katika makutano ya barabara za Morogoro, Sam Nujoma na Nelson Mandela katika eneo hilo.


Kutakuwa na awamu mbili za ufungaji wa njia kuanzia leo saa 4 usiku hadi keshokutwa saa 12 asubuhi; kwa ajili ya kutoa nafasi kwa ujenzi unaoendelea.


Akielezea zaidi, alisema katika awamu ya kwanza, ujenzi huo utahusisha eneo la upande wa kulia la makutano ya barabara ya Sam Nujoma na Morogoro ambalo litafungwa.


“Hali hii itasababisha magari yanayotoka maeneo ya Buguruni na Tabata kuelekea maeneo ya Mwenge kutoweza kutumia njia ya Sam Nujoma watakapofika taa za Ubungo,” alisema.


Alifafanua kuwa magari hayo yatalazimika kufuata alama zitakazowaelekeza kupita katika barabara za mradi zinazojengwa hadi barabara ya Shekilango ambapo wataweza kukutana tena na Sam Nujoma kwa kutumia barabara ya Igesa.


Pia magari yatakayokuwa yanatoka Sinza kupitia barabara ya Igesa hayataweza kwenda eneo la Ubungo yatakapofika katika makutano ya barabara za Igesa na Sam Nujoma.


Alifafanua kuwa magari yanayotumia Barabara ya Morogoro kutoka maeneo ya Mbezi na Kimara, yatalazimika kuchepuka kulia na kutumia barabara za mabasi ya mwendo wa haraka yatakapofika eneo la Kibo ambapo patakuwa na kizuizi.


Mkumba alisema katika awamu ya pili ya ujenzi huo, eneo la upande wa kushoto la makutano ya barabara za Morogoro na Nelson Mandela litafungwa kesho kuanzia saa nne usiku hadi keshokutwa saa 12 asubuhi.


Katika awamu hii, alisema, watumiaji wa magari yatakayokuwa yanatokea eneo la Mwenge kutumia barabara ya Sam Nujoma yatalazimika kuchepuka kushoto kukamata barabara ya Igesa kisha Shekilango.


Pia magari yatakayokuwa yanatoka Barabara ya Mandela na kutaka kwenda mjini kwa kutumia njia ya Morogoro yatalazimika kuchepuka kushoto na kwenda kugeukia eneo la Kibo ili kukamata barabara ya Morogoro.


“Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaotokea,” alisema Mkumba na kuongeza kwamba anaamini kutakuwa na usumbufu ambao hata hivyo utakuwa ni wa muda. Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka unaoendelea, unatarajiwa baada ya kukamilika utaondoa adha ya foleni katika Jiji la Dar es Salaam na kuleta ufanisi wa usafiri.


Chanzo;Habari leo
 
foleni haitakuja kwisha dar bila fly overs kujengwa ktk makutano ya barabara zote ambazo ni bize..,otherwise mipango yoyote itakayoendelea ni kuwanufaisha viongozi wanaosaini hiyo miradi kwa niaba ya serikali through 10%
 
Back
Top Bottom