Mizaha kila sehemu.....

Wahenga walisema "Jasiri haachi asil" huenda ikawa ndio asili yetu.

  • Viwanja vywa wazi, tunajenga magodown, ili watoto wakacheze barabarani.
  • Fukwe za public tunazibinafsisha, kesho tunaandamana kudai punguzo la kiingilio getini,
  • Rais anafungua hoteli ya kifahari leo, Alfajiri manispaa wanaivunja, ipo wrong sited.
  • Wazirti anamiliki mabilioni anaita Vijisenti.
Si mizaha hii wazee............!!!!!
 
06_10_51h89e.jpg
 
Unategemea wafanye nini hapa kwenye reli kama siyo kufanya biashara? maana treni zenyewe hazipiti ni mbovu.

kwa vile treni haipiti wabongo wameona wafanya mzaha kwenye reli, lakini mzaha ulianzia kwa waheshimiwa viongozi wetu kwa kuamua kuwapa wahindi TRC. Tena mimi naona ni masihara.
 
magari ya ikulu tuliweka chakachua,nati tulifunga za china,baada ya miaka mitano kila mwanafunzi atkuwa na kompyuta,tutajenga bararbara za juu kesho kutwa,wasomi wa yudom wamemchangia jk hela ya kuchukua fomu,tulinunua ndege ya rais isiyokuwa na injini,rada ya mwaka 47,tumempa mhindi vichwa vyote vya treni mshahara wa wafanyakazi tukalipa sisi,tbc tumewapa wachina,raisi mstaafu aliiba mgodi wetu tukamlipa fidia,nyumba za serikali tumegawana utafikiri tunahama,barabara wanatujengea wajomba zetu wachina baada ya miaka miwili repea,tuna flying presidaa,wafanyakazi hatuwezi kuwalipa kcc kinacholingana na hali ya maisha hata yesu akirudi,magereza tumeweka sofa ili wanene wakazuge huko wadanganyika wakipiga kelele,bajeti yetu inategemea pombe na fegi,uchumi unakuwa kwenye makartasi,tanzania bila ukimwi imewezekana bila kula.nk every where just jokes
 
Kama hao jamaa waliokalia taruma la reli, wana uhakika wa maisha yao kama treni haijapita hapo miaka kibao wafanye nini, wameshaona ni hali ya kawaida. Kule TANGA tayari watu wameshaanza kung'oa taruma kuuza kama vyuma chakavu.
 
Mate tu, mbona madogo... kuna wengine wanapua kwa makususdi kabisaaa na hali wakijuwa kuwa wamekula maharagwe.

hebu mwambie mtu aliye ktk bus asitupe chupa ya maji (viplastic vya azam) akimaliza kunywa barabarani uone atakavyokushangaa, unaweza kuonekana ni mtu mwenye majivuno...
Sijui ustaarabu liwe somo kuanzia chekechea nchini?? nashindwa kuelewa kabisa jamii yetu ni ya namna gani.
 
Huu ni ujinga, na hii hali itaendelea kututafuna WaTZ, unaona kitu na madhara yake lakini bado unaendelea kuchukulia mzaha tu. Sitegemei mabadiliko ya haraka katika hii nchi.

Mtaro wa maji machafu uko hapo mbele ya nyumba yako lakini utakuta unafagia na kisha kufukia huo mtaro masika ikianza mafuriko yanakuoiga mwenyewe.

Kuelekea uchaguzi Rais anakuja Chuoni kwako anakuambia tutaboresha Mfuko wa Mikopo, unachekelea na kutoa hicho chako kidogo kumchangia. Wakati wa tatizo lenyewe alikaa kimya. Hii si mizaha hiii.
 
Kwa kweli mizaha hii imekuwa kero sana, unakuta raia wanadanganyiika kwa kanga, vitenge, t-shirt na kofia na maisha mazuri
Nyakati za chaguzi kisha wanasahauka kabisa wakidai haki fulani wanafananishwa na aina fulani ya ndege (bird)
Kaazi kwelikweli! :angry:
 
Hao jamaa wanajaribu kuona je mtu akikaa kinatokea nini. Pia walioweka kibao hicho wala hawafuatilii, yawezekana na wenyewe wanakaa hapo! Pia vile vile watanzania wengi hawasomi, hata wakisoma hawaelewi; mfano, nilikuwa kwenye daladala binti mmoja akasoma kibao nje kinasema: 'ni marufuku kuegesha malori au magari kwenye hifadhi ya barabara'. Akamwuliza mwenzie 'hifadhi ya barabara ni wapi', na mwenzio akajibu 'sijui'. Kwa ujumla ni ujinga tu.
 
Mmesahau ile ya ofisi ya mtendaji wa kata ya Msasani kubomolewa kisa! kiwanja cha mtu.Viwanja vyetu vya wazi vya kuchezea watoto wetu vinauzwa na kujengwa baa,hizi akili zetu matope!
 
Do we (you and me ) care attitude , hi ndio attitude yetu kwenye kila kitu kuanzia nyumbani, ofisini, barabarani, mpaka kwenye vitu vya msingi vinavyotuhusu. Huu sio mzaha ila ni ujinga wa watanzania.

Gari tani 7 anapakia tani 10, gari abiria watano utaona limepakia 8, daraja uzito tani 10 semi trailer inapitishwa. Taa nyekundu dereva anakwenda tu, mtu anaumwa mguu anapasuliwa kichwa. Loliondo anakuja mtu wa Longido

Masa nchii hii we acha tu.


Niliwahi kusimuliwa trafiki mmoja kule maeneo ya Iringa,aliwahi kuwakamata jamaa kisa wamebeba abiria wachache badala ya kubeba abiria wengi zaidi.
 
Back
Top Bottom