Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,845
Ni aina ya sanaa mfanano wa prank (kuwafanyia wengine mizaha), lakini ya kwake ikiwa pengine kwa kukosa umakini na miongozo inawadhalilisha na kutweza utu wa watu.
Kusingizia kwa mzaha tuhuma mbalimbali na kubadili maneno ya anayemhoji ni mtindo anaoupendelea zaidi
Ni kweli kafanya ubunifu wa sanaa unaomuingizia kipato lakini sasa anatakiwa kuwa na miongozo yakinifu ili asivuke mipaka ya mizaha na kujikuta anadhalilisha watu wenye staha zao.
Hilo tayari limeshamletea shida mahali pengi na kujikuta anaambulia vipigo vya wastani, lakini si kila siku ni Jumapili atakuja kuingia mahali pasipohitaji mizaha na kukuta watu/mtu ana stress zake akabamizwa akaumizwa sana hata kupelekea majeraha makubwa, ulemavu na si ajabu hata kifo!
Nina hakika hajajikatia bima ya sanaa anayofanya, ili likimtokea la kumtokea asianze kutembeza bakuli la msaada
Serikali nayo kupitia BASATA na BAKITA wampe miongozo sahihi ili aweze kufanya sanaa yake kwenye misingi isiyovuka staha na privacy za watu
Hakuna kitu kinakosa bahati mbaya.. Lakini iwe bahati mbaya kweli na si kwasababu ya uzembe na kutofuata
Miongozo
Sent using Jamii Forums mobile app