Mitihani yote amefaulu, vizingiti vyote amevuka bado kimoja tu

Mitihani yote amefaulu, vizingiti vyote amevuka bado kimoja tu

Ni Magufuli Tenaa Mitano Tenaaa.

Congratulations in advance President Magufuli

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
✝️


Zaburi 91
3 Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji,Na katika tauni iharibuyo.
4 Kwa manyoya yake atakufunika,Chini ya mbawa zake utapata kimbilio;Uaminifu wake ni ngao na kigao.

Zaburi 35
6 Njia yao na iwe giza na utelezi,Malaika wa BWANA akiwafuatia.
8 Uharibifu na umpate kwa ghafula,Na wavu aliouficha umnase yeye mwenyewe;Kwa uharibifu aanguke ndani yake.


Mungu uliyehai yakiwa yamebaki masaa machache ya uchaguzi na siku imeshawadia tunakushukuru kwa uaminifu wako, tunaendelea kunyunyiza damu ya Yesu kwenye moyo wa uchaguzi, tunaendelea kunyunyiza damu ya Yesu juu ya Watanzania wote katika jina la Yesu. Baba nakushukuru kwa kuwa njia za kutoka mautini Zina Jehovah Bwana. Adui kaandaa mtego wa mauti kwa Watanzania Lakini wewe Ni Mungu uliyehai na njia za kutoka kwenye huo mtego zipo kwako Bwana, Baba nakushukuru kwa kutuokoa na mtego wa mauti wa mwindaji, uko mtego wa mauti kupitia mapolisi, uko mtego wa mauti kupitia Jeshi la Wananchi, Lakini njia za kutoka mautini Zina Jehovah Bwana, Baba Farao alipowanyima WATOTO wako ruusa waende wakakutumikie bahari iligeuka kuwa mkono wako ikameza majeshi yote ya Farao. Nasi tunakushukuru kwa kuwa sisi tunakuangalia wewe Bwana, wao wanataja farasi, wao wanataja magari, risasi na mabomu na majeshi na polisi, sisi tunalitaja jina la Bwana Mungu wa majeshi, nakushukuru Bwana maana najua ipo bahari itakayo yapinga majeshi yote yaliyokinyume na wewe Mungu uliyehai. Ipo bahari itakayomeza majeshi yote ya Farao katika jina la Yesu, Baba nakutukuza kwa kuwa wavu waliouficha ndani ya uchaguzi huu utawanasa wao wenyewe katika jina la Yesu, iko mipango zipo njama ndo nyavu zenyewe hizo Bwana Lakini kwa kuwa wewe Ni Mungu uliye hai wavu wao umewanasa wao wenyewe katika jina la Yesu na kwa uharibifu wameingia ndani yake, Shimo walilolichimba wameingia wenyewe katika jina la Yesu, Baba nakushukuru kwa kuwa Njia yao imekuwa giza na utelezi katika jina la Yesu, kila wanachokifanya kimekuwa giza na utelezi, kila mpango umeteleza kwa jina la Yesu, kila mpango hautafanikiwa katika jina la Yesu, Wao watapatwa na giza mchana wakienda wakipapasa papasa Kama usiku katika jina la Yesu, mashauri yao yamebatilika katika jina la Yesu, maneno yao hayatasimama katika jina la Yesu, vitisho vyao havitasimama naona vikiyeyuka katika jina la Yesu, naona majeshi ambayo wanayategemea Asante Mungu naona umewaondolea ujasiri, naona wanakuwa na hofu kuu, naona wakiweka Silaha chini wakikimbia Kama majeshi ya washami, Asante Yesu naona umeyasikilizisha majeshi yao vishindo na hofu kuu imewapata katika jina la Yesu, Baba nakushukuru nakutukuza kwa kuwa wataibika, wamefedheheka, wametayarika kwa mkono wako mkuu Sana katika jina la Yesu, Baba nakushukuru kwa kuwa Njia yao imekuwa utelezi, nakushukuru kwa kuwa Njia yao imekuwa giza katika jina la Yesu. Neno lako linasema washindanao na Bwana watapondwa kabisa nami nakushukuru kwa kuwa wote washindanao na makusudi yako, na Mapenzi yako, naona mkono wako uko juu yao kuwapondwa kabisa katika jina la Yesu. Baba nakushukuru kwa kuwa Silaha zote zilizoandaliwa na Adui kwa ajili ya dhuluma, wizi, utapeli, mauaji, uonevu Silaha hizo hazitafanikiwa katika jina la Yesu. Silaha hizo zimewageukia wenyewe katika jina la Yesu, Baba katika jina la Yesu sasa tunawachafulia semi wasielewane katika jina la Yesu, tunaziteka nyara Silaha zao nakuamuru wageuziane wao kwa wao katika jina la Yesu, Baba tunawafarakanisha wao kwa wao katika mashauri yao, wasielewane katika jina la Yesu, Eee Bwana tunawachafulia semi, na kuwafarakanisha kabisa wasielewane wao kwa wao katika jina la Yesu. Ee Bwana Kama vile ulivyowateka maadui wa Daudi kipindi kile Sauli alivyotaka kumuuwa Daudi, ukawapiga usingizi na ukawaweka mikononi kwa Daudi wewe Ni Mungu yuleyule Jana leo na hata milele, Asante kwa kuwa umeyateka majeshi yote ya Sauli, Asante kwa kuwa umeyabadilishia hata ufahamu na moyo walking nao, majeshi badala ya kuwa kinyume Cha Daudi yakawa pamoja na Daudi. Asante Bwana maana naona hayo yakitimia katika jina la Yesu. Asante kwa kuwa majeshi yatakuwa na Daudi wako katika uchaguzi huu katika jina la Yesu, kwa kuwa hakuna linaloshindikana kwako Bwana, hayatakuwa na Sauli maana Sauli wewe Mungu umemkataa katika jina la Yesu. Baba nakushukuru kwa kuwa wewe ni Mungu katikati ya dhuluma yao, katikati ya hila yao, katikati ya udanganyifu wao, katikati ya mabavu yao, katikati ya utapeli wao, katikati ya vitisho vyao, katikati ya uonevu wao, Baba Mungu wa miungu utapita katikati yao na kubatilisha mashauri na hila zao katika jina la Yesu na kila kiumbe kitajua wewe Ni Mungu wa Israeli. Na kila kiumbe kitajua wewe ndiwe uzitawalie mbingu na nchi, na wewe humweka kwenye kiti cha ufalme yule umtakaye. Na wewe Mungu humwondoa Yule usiyemtaka, Maana mbingu zako Mungu Jehovah ndizo zinazo tawala dunia, na si majeshi, Wala farasi, Wala risasi, Wala mabomu viwezavyo kushindana na uweza wako Baba Mungu wa mbinguni uliyeziumba mbingu na nchi, Wala HAKUNA kikosi wala majeshi yanawezayo kumweka mtu awe Mfalme kwenye kiti chako, isipokuwa kwa kibali chako Baba Mungu wa mbinguni, Bali wewe Bwana wa majeshi, humweka umtakaye, humwondoa umchukiaye katika jina la Yesu, Asante kwa kuwa uweza wako utajulikana, nguvu zako zitajulikana, ya kwamba hakuna Mungu aliye Kama wewe. HAKUNA Mungu wa haki Kama wewe, hakuna Mungu wa kuabudiwa Kama wewe, hakuna Mungu wa kushukuriwa Kama wewe, hakuna Mungu mwaminifu Kama wewe. Hakuna Mungu mwenye uweza Kama wewe. Ni wewe peke yako wastahili kuabudiwa kushukuriwa kusujudiwa, kupewa sifa na heshima na utukufu. Baba nakushukuru kwa kuwa umefanya umetenda zaidi ya nilivyoomba kufikiri na kuwaza katika jina la Yesu nimeomba na kushukur
 
Ni Magufuli Tenaa Mitano Tenaaa.

Congratulations in advance President Magufuli

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
IMG-20201027-WA0055.jpg
 
Nusura ya vifungo
Nusura ya kifo
Nusura ya kurejea ngamani
Nusura ya kukamatwa
Nusura ya kuteuliwa kugombea
Nusura ya kupitishwa na tume
Nusura ya kufanya kampeni
Nusura ya kuruka na chopa
Bado nini tena?

Nine lives count! Bado ya mwisho kubwa kuliko yote! Tunatazamia!
Kukichwa kutapambazuka lakini kabla Jua halijachomoza kiza huwa kinene na giza huwa totoro.

View attachment 1613849
onyo kwa wahusika mpango wa Mungu hauchakachuliwi. Wote waliofanya hivyo Mungu aliwaua na ndivyo itakavyokuwa
 
Ikiwa atashinda na asitangazwe basi atakaye tangazwa bila kushinda ajue Mungu anampenda zaidi hivi karibuni. Neno la kinabii
Unabii wa shetani hauwezi timia, kama unayo kumbukumbu rejea unabii wa mheshimiwa Lema pale arusha,
Baada ya kutupwa jela unabii nao ukafa mpaka leo.
Hivyo wa kwako nao ni wa kishetani.
Pia hakuna ushindi wa dhurma nduyi atashindwa mpaka apate pressure na kurudi kutibiwa huko ublj
 
Leo Lisu atajuta kuijua Dar na kuwa mkazi wa Dar CCM tutakavyompiga chini kwenye kura
 
Unabii wa shetani hauwezi timia, kama unayo kumbukumbu rejea unabii wa mheshimiwa Lema pale arusha,
Baada ya kutupwa jela unabii nao ukafa mpaka leo.
Hivyo wa kwako nao ni wa kishetani.
Pia hakuna ushindi wa dhurma nduyi atashindwa mpaka apate pressure na kurudi kutibiwa huko ublj
std 7 kama wewe humu sio mahali pako, unajiabisha bure
 
Ama tcra wameweza kuzima mitandao, basi tarajieni akipita magufuli, ndani ya miaka mitano kila jambo ambalo haramu ambalo CCM wanaenda kulipitisha, mf kuingeza ukomo wa rais, basi watazima. Ushakuwa utamaduni wao

Sent from my TECNO KD6 using JamiiForums mobile app
 
Sikutegemea angekuwa na guts za kuamuru chopa irushwe baada ya kuona anazinguliwa na mamlaka
Mkuu mpaka sasa hivi nimetembelea Kata 20 za Jimbo la Hai, nimepita Uroki, Nkira, Aishi, Uswaa, Nshara, Mamba, Kalali, Uraa, Kisiki, Nkoraya, Sonu, Kyeeri, Nkuu, Kisereni, Mwowe Msikitini, Kashinsha na Lyamungo Sinde, Nkweseko, .Nkwarungo, Ng'uni, Masama Magharibi na Masama Kusini nimeweka watu 162 katika vijiji vyote ili nipate taarifa za uhakika za mwenendo wa kupiga kura na matokeo sahihi ya Jimbo la Hai.

CCM wamepitiana nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda, hata wagonjwa wamebebwa na kutafutiwa jinsi gani bora ya kupiga kura na wamejipanga kweli kweli.

Sasa hivi nipo Bomang'ombe mistari ni mirefu na mingi katika kila kituo cha kupiga kura. Wanasema kila wapiga kura 100 wana wahamasishaji 2. Wakipiga kura watu wao 42,000 jimbo zima la Hai zitatosha. Zingine wamuachie kaka Mbowe ajisaidie.

CCM wanasema mpaka saa 10 jioni watakuwa wamemaliza kazi ya kupiga kura. Na kupata matokeo sahihi. Ila sina hakika kama kila mpiga kura anapewa zawadi. Pombe ni nyingi mnoo karibu kila sehemu ila hawauzi mpaka wamalize kupiga kura.

Tusubiri tuone yanayoendelea. ASANTE.
 
Nusura ya vifungo
Nusura ya kifo
Nusura ya kurejea ngamani
Nusura ya kukamatwa
Nusura ya kuteuliwa kugombea
Nusura ya kupitishwa na tume
Nusura ya kufanya kampeni
Nusura ya kuruka na chopa
Bado nini tena?

Nine lives count! Bado ya mwisho kubwa kuliko yote! Tunatazamia!
Kukichwa kutapambazuka lakini kabla Jua halijachomoza kiza huwa kinene na giza huwa totoro.

View attachment 1613849
Tukapige kura kwa wingi viongozi
 
Lowassa sio Lissu...2015 sio 2020 lakini
Sasa wewe kwa akili yako unafikiri Lissu atashinda kweli, Mshana Jr najuwe wewe ni mshirikina sana....hii ramli yako ya upareni leo inakuambua na ninakuhakikishia Lissu hawezi kuwa eais wetu kamwe. Yule kalaaniwa, anataka wewe na watanzania wenzako muwe mashoga ili mpate misaada toka Marekani na Uingereza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom