Mkuu mpaka sasa hivi nimetembelea Kata 20 za Jimbo la Hai, nimepita Uroki, Nkira, Aishi, Uswaa, Nshara, Mamba, Kalali, Uraa, Kisiki, Nkoraya, Sonu, Kyeeri, Nkuu, Kisereni, Mwowe Msikitini, Kashinsha na Lyamungo Sinde, Nkweseko, .Nkwarungo, Ng'uni, Masama Magharibi na Masama Kusini nimeweka watu 162 katika vijiji vyote ili nipate taarifa za uhakika za mwenendo wa kupiga kura na matokeo sahihi ya Jimbo la Hai.
CCM wamepitiana nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda, hata wagonjwa wamebebwa na kutafutiwa jinsi gani bora ya kupiga kura na wamejipanga kweli kweli.
Sasa hivi nipo Bomang'ombe mistari ni mirefu na mingi katika kila kituo cha kupiga kura. Wanasema kila wapiga kura 100 wana wahamasishaji 2. Wakipiga kura watu wao 42,000 jimbo zima la Hai zitatosha. Zingine wamuachie kaka Mbowe ajisaidie.
CCM wanasema mpaka saa 10 jioni watakuwa wamemaliza kazi ya kupiga kura. Na kupata matokeo sahihi. Ila sina hakika kama kila mpiga kura anapewa zawadi. Pombe ni nyingi mnoo karibu kila sehemu ila hawauzi mpaka wamalize kupiga kura.
Tusubiri tuone yanayoendelea. ASANTE.