Tumeshuhudia hivi karibuni nchi yetu ya Tanzania ikishadadia kwa mtindo wa copy and paste falsafa ya 'big result now" kutoka nchini Malaysia. Huu ni mpango mrefu wa maendeleo nchini humo ambao umeleta mafanikio katika sekta zote. Watazania kupitia viongozi wetu tumebeba kama ilivyo tukitaraji falsafa tupu itapike maendeleo kama tuloshuhudia kwa wenzetu. Mfano hvi karibuni nmesikia Waziri wa elimu na msaidizi wake wakishadadia falsafa kisiasa pasipo kujua kuwa matokeo bora yanatokana uwekezaji wa fedha, usimamizi madhubuti ambapo kinyume chake ni porojo za uchaguzi. Huwezi kupata mavuno ya maana bila kutumia njia za kitaalamu. Huwezi zungumzia matokeo mazuri ya elimu bila kugusia mishahara ya watumishi wa elimu, mafunzo kazini kuwajengea uwezo, vitendea kazi, uboreshaji wa mifumo ya kufundishia na kujifunzia, teknolojia ya habari na mwasiliano pamoja na usimamizi madhubuti. Hatutataki siasa za uchaguzi, tunataka uwekezaji katika sekta za afya, kilimo na elimu.