Kwa haraka haraka baada ya kupitia mitihani yote miwili nimegundua makosa yafuatayo:
SECTION A: GRAMMAR
 Swali namba 4 lina makosa ya kisarufi (swali limeandikwa "a big number of cow" badala ya "a big number of cows"). Nashindwa kuelewa kama hii mitihani ilichapwa kwa type writer au kwa compyuta kwani makosa kama haya husahihishwa na kompyuta yenyewe wakati wa kuchapa.
 Swali namba 17 haliko vizuri kisarufi. Ili liwe sahihi sentensi iliyopo ama ilipaswa kugawanywa katika sentensi mbili kamili au swali ingeandikwa upya kama hivi:
(i) These are our books.(They) are very useful (ambapo jibu lingekuwa D) au
(ii) Our books ARE very useful (au vinginevyo)
 Swali namba 19 (you must be take the punishment)-hii lugha haiweleki kabisa. Sijui kama baada ya kutungwa hii mitihani ilipitiwa kuangaliwa makosa yaliyomo ama vipi!
 Swali namba 20 lina majibu mawili [(a) & (c)]
 Kwa swali namba 24 hakukuwa na haja ya kuweka neno the kabla ya noun ‘tea'- lingeweza kuandikwa neno ‘tea' peke yake na likatosha kuleta maana, i,e: This is the place where tea is manufactured. Kwanza neno "manufactured" sio sahihi hapa-inaonekana watunzi walinakiri sentensi hii moja kwa moja kutoka kwenye vitabu feki vya kina Nyangwine (Kumbuka kilio cha Mbatia Bungeni). In a real sense, tea is not "manufactured" but it is processed-yaani majani ya chai hayatengenezwi kiwandani (manufactured) bali husindikwa (processed). Mpo hapo?
SECTION B: VOCABULARY
 Maelezo ya mwanzo katika hii section sio sahihi kisarufi (For each questions 31-36,………..). Maneno shahihi ambayo yangetumika ni "For each of the questions 31-36,…………….."
 Swali namba 34 (know us)-ni "known as"
 Swali namba 36 (two similar thing)-nadhani walikuwa wanamaanisha "(b) two similar things".
SECTION C: COMPOSITION
 Maelezo ya awali hayaeleweki-"a neaningful story giving then letters A-D". Nadhani hapa walikuwa na maana ya kuandika "a meaningful story, giving them letters A-D".
 Pamoja na makosa haya machache kuna typing errors zimeonekana hapo juu kwa mfano neno ‘shall' limeandikwa ‘shal'; ‘although' limeandikwa ‘althoug'; na ‘three' limeandikwa ‘thre'. Haya makosa yanaweza kuonekana madogo lakini kwa mwanafunzi wa shule ya msingi yanamchanganya na kumpoteza kabisa.
Kwanza nashangaa sana jinsi watoto wanavyokaririshwa maswali bila hata kupimwa kama wanajua kusoma au kuandika. Watoto wanapaswa kufundishwa kuandika insha fupi au composition katika mitihani yao ya Kiswahili na Kiingereza. Tunajenga taifa la watu vilaza wanaojua kugandamizia kila kitu bila kuhitajika kutumia akili wala ubongo. Sijui hasa ni wapi wanasiasa wetu wanataka kulipeleka taifa hili. Tatizo ni kwamba tumewaachia wanasiasa ndio watuamulie kila kitu hata kama hakina tija kwa mendeleo na ustawi wa wananchi.
HESABU
 Swali namba 13 halina jibu. Majibu yote yaliyotolewa sio majibu sahihi.
 Swali namba 14 halieleweki na halina jibu. Haieleweki watunzi walitaka hili swali lirahisishweje. Kama kuna ambaye ameelewa, atufafanulie. Swali lipo katika sehemu mchanganyiko (mixed fraction)-labda kama swali lingeuliza kubadilishwa kuwa improper fraction, hapo lingeeleweka kidogo!
 Swali namba 22 halifanyiki (limekosewa). Huwezi kupata thamani ya y ikiwa thamani ya x haijulikani.
 Swali namba 23 halina jibu sahihi miongoni mwa majawabu yaliyotolewa.
 Swali namba 29 halieleweki na hata kama ukilirekebisha kikakaa vizuri, bado hakuna jawabu sahihi miongoni mwa majawabu yaliyotolewa. Yaani ukilibadilisha likawa hivi 4/5a =21:12 au 4/5:a =21:12 na ukatafuta thamani ya a, bado hakuna jibu sahihi katika majibu yaliyopo.
 Swali namba 31 halijakamilika (limekosewa). Huwezi kupata thamani ya r (nusu kipenyo) ikiwa urefu wa mche duara haujulikani. Kwa maana hiyo ni kwamba huwezi kutafuta vitu viwili ambavyo havijulikani!
 Swali namba 32 limekosewa. Kwa jinsi swali lilivyo, thamani ya n=169º. Jibu haliwezi kuwa dogo kama hayo majibu yaliyotolewa. Kama nimekosea nisahihishe.
 Swali namba 33 linafanyika lakini swali hili ni gumu mno kwa watoto wa darasa la saba.
 Swali namba 35 halina jibu. Jibu sahihi ni 3646.5 sm2
 Swali namba 37 ni gumu sana kwa watoto hawa wadogo.
 Swali namba 38 halina jibu na ni gumu sana kwa watoto.
 Swali namba 45 halijakamilika. Jibu haliwezi kupatikana bila kutaja idadi ya pipi alizopata angalau mmojawapo wa hao marafiki watatu. Pili, majibu yake yamechanganywa. Hili ni kosa la kizembe kabisa.
 Swali namba 47 lina makosa ya kiufundi na halina jibu-eti tani 24,000/=!!!!!?????????? Hivi hawa watunzi huwa hawarudii kusoma haya maswali? Ama kweli walimu wamechoka! Hata kama tukichukulia kwamba hizo ni tani 24,000 bado hakuna jibu sahihi miongoni mwa majibu yaliyotolewa.
 Swali namba 48 halieleweki. Huwezi kupata umri wa yeyote kati yao ikiwa hujapewa umri wa sasa (au wa zamani) wa Anna au mjomba wake.
Katika hali kama hii, tutaimba sana ngonjera ya BRN lakini mwisho wa siku tutegemee matokeo 0; na hali hii itaendelea kuwa hivyo hadi mwisho wa dahari.
Nawasilisha.