NostradamusEstrademe
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 3,032
- 4,028
Inakuwaje mtu umechukua line ya mtandao fulani ukawa unatumia lakini kuna uwezekano kibinadamu kuna sababu mbalimbali kiuchumi hali ngumu au ukaugua muda mrefu kiasi kwamba huwezi hata kutumia simu kwa maana ya kununua hata vocha. Sasa baada ya siku au miezi kadhaa unaambiwa namba yako amepewa mtu mwingine?
Kumbukeni hizi namba ndio zimesajiliwa NIDA kwa maana hiyo kwa mawazo yangu kiusalama hii haijakaa sawa kabisa.
Nilikuwa na wazo mtu akisajiliwa namba yake hata kama hataitumia asipewe mtu mwingine kama mtiririko wa namba za magari ambapo haurudi nyuma hata kama gari limepata ajali halifai tena au umeamua ulipaki lisitembee.
Kumbukeni namba huwa hazina mwisho.Hakuna mwisho wa kuhesabu aslani kuna ubaya gani mkaendeleza namba kwenda mbele?
Waziri mhusika mhe naomba chunguza hili kwa mapana yake na ulifanyie kazi linahatarisha usalama na kuvuruga taratibu za taarifa za watanzania kwenye mifumo ya utambuzi kiserikali.