HOJA Mapendekezo ya maboresho ya mfumo wa "Lipa kwa Simu"

HOJA Mapendekezo ya maboresho ya mfumo wa "Lipa kwa Simu"

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

azithromycim

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2019
Posts
553
Reaction score
1,223
Ukuaji wa huduma za malipo ya kidijitali mitaani ni hatua muhimu kuelekea uchumi usiotegemea fedha taslimu (Cashless Economy).

Hata hivyo, ili kufikia malengo ya kitaifa ya ujumuishaji wa kifedha, kuna haja ya kufanya mapinduzi katika muundo wa sasa wa malipo.

1. Kuanzishwa kwa Namba Moja ya Malipo (Universal QR/Lipa Namba)

Badala ya kila kampuni ya simu kuwa na mfumo wake unaojitegemea, Serikali inapaswa kuanzisha Universal Lipa Namba itakayounganishwa na leseni ya biashara au TIN ya mhusika.

Urahisi: Mteja wa mtandao wowote ataweza kulipa kwenye namba hiyo moja bila vikwazo vya "mitandao kutofanya kazi pamoja" (Interoperability).

Uwazi wa Mapato: Mfumo huu utaiwezesha Mamlaka ya Mapato (TRA) kuona mzunguko halisi wa biashara kwa wakati (real-time), jambo litakalorahisisha ukadiriaji wa kodi ya mapato kwa haki na usahihi.

2. Kuondoa Tozo za Miamala (Transaction Levy) kwenye Malipo ya Bidhaa

Ili kuhamasisha matumizi ya kidijitali, Serikali inapaswa kuondoa tozo za miamala kwa mteja anayenunua bidhaa au huduma (Consumer End).

Motisha kwa Mteja: Ikiwa kununua kwa simu kutakuwa na gharama sawa na kutoa fedha taslimu mfukoni, wananchi wengi watapendelea kutumia simu.

Kupunguza Mzigo: Hii itamuondolea mwananchi mnyonge mzigo wa makato yanayofanya bidhaa ionekane ghali zaidi inapolipiwa kidijitali.
 
Ndio maana tunaiyomba serikali ije na universal QR isiyokuwa na tozo kwa mteja na mfanyabiashara.
Ilk kuhamasisha Cashless Economy
 
Shida ya lipa makato mfano en em b makato ya LIPA yameongezeka sasa hivi hata kitu kidogo tu unakuta makato ya LIPA kwa simu 1,600/-
 
Back
Top Bottom