Mitambo IPTL yazimwa, wakwama kufanya biashara ya umeme | Page 5 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mitambo IPTL yazimwa, wakwama kufanya biashara ya umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ghazwat, Jul 17, 2017.

 1. Ghazwat

  Ghazwat JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 4, 2015
  Messages: 15,830
  Likes Received: 48,061
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Ni wingu zito. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya maombi ya Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kukwama, huku wakilazimika kuzima rasmi mitambo yao ya uzalishaji umeme.

  Hatua hiyo imekuja baada ya kukwama kwa maombi ya kuongezewa muda wa miezi 55 ya leseni yake ya uzalishaji umeme kutokana na kusubiri uamuzi wa Ikulu.

  Hali hiyo inajitokeza wakati mmiliki wa Kampuni ya Pan Africa Power (PAP) Harbinder Singh Sethi na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira wakiwa tayari wamefikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya uhujumu uchumi, kutakatisha fedha na kusababisha hasara Serikali.

  Hali za uhakika zilizolifikia gazeti hili jana zilisema mitambo hiyo kwa sasa haizalishi umeme.

  MTANZANIA lilitembelea mitambo hiyo iliyoko Tegeta na kukuta wafanyakazi wachache ambao walikiri mitambo hiyo kutofanya kazi.

  "Mitambo ilizimwa tangu siku ile walipomkamata Sethi", alisema mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambaye hakuwa tayari kutajwa jina lake gazetini.

  Pamoja na hatua hiyo inaelezwa kuwa kuna hatari ya kuitaifishwa kwa mitambo hiyo hasa baada ya Serikali kuweka ngumu katika utoaji wa leseni mpya ya biashara ya kuzalisha umeme kwa kampuni hiyo.

  Licha ya hali hiyo leseni ya kampuni hiyo ilimalizika muda wake Julai 15, mwaka huu ambapo hadi sasa uamuzi wa kuitaifisha mitambo hiyo kurudi kuwa mali ya TANESCO ama laa ukisubiri uamuzi wa Ikulu.

  Kwa sababu hiyo, kama Serikali itaendelea na msimamo wake dhidi ya IPTL ndiyo utakuwa mwisho wa miaka 23 ya IPTL.

  Kampuni hiyo au IPTL iliingia nchini tangu mwaka 1994 na kila mwezi imekuwa ikilipwa Sh. bilioni 5.943 na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ikiwa ni gharama za uwekezaji mbali na gharama za umeme inaoliuzia shirika hilo.

  Novemba 2014, baada ya Bunge kujadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ilitoa maazimio manane ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO.

  Siku chache baada ya Bunge kupitisha uamuzi huo ambao ulifanyiwa kazi kwa haraka kwa Profesa Sospeter Muhongo kujiuzulu nafasi yake.
   
 2. c

  chikundi JF-Expert Member

  #81
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 16, 2016
  Messages: 8,214
  Likes Received: 2,251
  Trophy Points: 280
  Tulivyokuwa hatuna bomberdier hata moja umeme ulikuwepo?

  Sent from my TECNO-C5 using JamiiForums mobile app
   
 3. c

  chikundi JF-Expert Member

  #82
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 16, 2016
  Messages: 8,214
  Likes Received: 2,251
  Trophy Points: 280
  Sio mingi yote. Kwa sab Tanzania haijawahi kutawaliwa na chama kingine.. Kila mtu anajua hivyo pamoja na magufuli.

  Sent from my TECNO-C5 using JamiiForums mobile app
   
 4. Yiyu Sheping

  Yiyu Sheping JF-Expert Member

  #83
  Jul 17, 2017
  Joined: Jun 21, 2016
  Messages: 1,714
  Likes Received: 803
  Trophy Points: 280
  Kishika uchumba 5.943 × 12 × 23 = nchi hii shamba la bibi. Mitambo imezimwa lakini wataendele kulipwa


  Na washawasha!
   
 5. c

  chegreyson JF-Expert Member

  #84
  Jul 17, 2017
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 821
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 80
  Mkataba imeisha watalipwaje capacity charge? Kilichokuwa kinawafanya walipwe capacity charge ni mkataba.
   
 6. G

  G4rpolitics JF-Expert Member

  #85
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 2,444
  Likes Received: 2,456
  Trophy Points: 280
  Hata mi nimemshangaa...wazee wa kupinga kils kitu..
   
 7. Wachovu

  Wachovu JF-Expert Member

  #86
  Jul 18, 2017
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 1,222
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Mambo kama ya Lowassa Kununua uongozi wa Chadema
   
 8. Ngumu kumeza

  Ngumu kumeza JF-Expert Member

  #87
  Jul 18, 2017
  Joined: Jun 19, 2012
  Messages: 503
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 60
  migao ya umeme kiukweli haipo tunayopambana nayo mtaani ni ya kutengenezwa.Hapo mahamani sijajua kwa kweli.
   
 9. ikipendaroho

  ikipendaroho JF-Expert Member

  #88
  Jul 18, 2017
  Joined: Jul 26, 2015
  Messages: 1,597
  Likes Received: 1,041
  Trophy Points: 280
  Hata gari, inafika wakati ukahisi kama huna haja ya kuwa na breki.
   
 10. misasa

  misasa JF-Expert Member

  #89
  Jul 18, 2017
  Joined: Feb 5, 2014
  Messages: 6,581
  Likes Received: 3,303
  Trophy Points: 280
 11. mrangi

  mrangi JF-Expert Member

  #90
  Jul 18, 2017
  Joined: Feb 19, 2014
  Messages: 23,839
  Likes Received: 10,426
  Trophy Points: 280
  Kamulize mzee wa msga,si alizibariki hela za escrow,mbn mnamgwayagwaya

  Ova
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #91
  Jul 18, 2017
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 79,067
  Likes Received: 111,651
  Trophy Points: 280
  Una uhai hadi 2022.

   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #92
  Jul 18, 2017
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 79,067
  Likes Received: 111,651
  Trophy Points: 280
  Mkuu mkataba wao na Tanesco uko hai kwa miaka mingine mitano hadi 2022, leseni yao ya kufanya kazi/biashara nchini ndiyo iliyoisha muda wake July 15, 2017.

   
 14. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #93
  Jul 18, 2017
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,388
  Likes Received: 5,741
  Trophy Points: 280
  PAE ni Songas.... wanauza umeme wa gas pale Ubungo!! Hao wengine ndio IPTL wamo
   
 15. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #94
  Jul 18, 2017
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,388
  Likes Received: 5,741
  Trophy Points: 280
  Hakuna athari yeyote ila wana mkataba hai....hilo ni pigo sio kwao tu wakitaifisha wawekezaji hawatakuja inabidi watumie akili sanaa nini cha kufanya!! Mwekezaji akija anakuw haelewi kama akikosea lolote halindwi na mkataba!! Ni tishio kwa wawekezaji!! Tuone busara kama ipo au hakuna kabisa!! Yeye ataondoka next 8yrs unaachaje nchi umevuruga miaka 100 mingine?? Sera za uwekezaji Zipo ila zinavunjwa nani atajenga viwanda?? Labda wajenge serikali.......maana wengine wataogopa!!! Makampuni mengi ya exploration yameamua kuondoka!!! Nani atakuja kwa hali ilivyo?? Sio rahisi kuwekeza kwenye risk!!!!
   
 16. d

  demulikuy JF-Expert Member

  #95
  Jul 18, 2017
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 741
  Likes Received: 416
  Trophy Points: 80
  Mkuu Bak hebu tuwekane sawa! Mitambo imezimwa sawa, je "CAPACITY CHARGES" zinalipwa au hazilipwi? Na kama zinalipwa, je zinalipwa na nani na ni kiasi gani?

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #96
  Jul 18, 2017
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 79,067
  Likes Received: 111,651
  Trophy Points: 280
  Mkuu swali lako ni zuri sana. Jibu langu linaweza kabisa kuwa si sahihi. Hawa jamaa hizo capacity charges walikuwa wanalipwa mitambo yao iwe imewashwa au la. Kutokana na leseni ya kufanya shughuli waliyokuwa wanaifanya tangu waingie nchini zaidi ya miaka 20 iliyopita kwisha muda wake hawastahili kuendelea kulipwa hata senti moja.

   
 18. n

  ng'adi lawi JF-Expert Member

  #97
  Jul 18, 2017
  Joined: Sep 27, 2014
  Messages: 2,847
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  H
  Hakuna mkataba mpya na matapeli.
   
 19. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #98
  Jul 18, 2017
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,772
  Likes Received: 4,515
  Trophy Points: 280
  Mkuu ukiyajua majibu ya maswali haya, basi utapata majibu ya maswali yako:
  1. Nani aliitafuta gesi ya Mtwara?
  2. Nan aliichimba gesi?
  3. Nan aligharamia kujenga miundombinu ya usafirishaji?
  4. Tanesco wanapewa bure gesi au wananunua kutoka TPDC?
   
 20. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #99
  Jul 18, 2017
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,772
  Likes Received: 4,515
  Trophy Points: 280
  Migao mikali ilikuwa inasababishwa na ukame na wapiga dili wenye plants binafsi za kuzaliwa Umeme(hawa wako wengi sana, japo iptl ndo maarufu). Kumekuwa na mvua za kutosha na kinyerezi imejengwa plant nyingine, hivyo hata kama kutakuwa na mgao basi utakuwa ule tuliouzoea.

  Ikumbukwe iptl ilikuwa inatumika kunapokuwa na mahitaji makubwa, mfano jioni au wakati wa sikukuu.
   
 21. c

  chige JF-Expert Member

  #100
  Jul 18, 2017
  Joined: Jul 11, 2016
  Messages: 6,974
  Likes Received: 12,415
  Trophy Points: 280
  Hakuna but it's a matter of time! Kwavile mvua zimekata majuzi tu, sina shaka mabwawa bado yana maji ya kutosha!!!
   
Loading...