Mitambo IPTL yazimwa, wakwama kufanya biashara ya umeme | Page 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mitambo IPTL yazimwa, wakwama kufanya biashara ya umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ghazwat, Jul 17, 2017.

 1. Ghazwat

  Ghazwat JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 4, 2015
  Messages: 15,830
  Likes Received: 48,061
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Ni wingu zito. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya maombi ya Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kukwama, huku wakilazimika kuzima rasmi mitambo yao ya uzalishaji umeme.

  Hatua hiyo imekuja baada ya kukwama kwa maombi ya kuongezewa muda wa miezi 55 ya leseni yake ya uzalishaji umeme kutokana na kusubiri uamuzi wa Ikulu.

  Hali hiyo inajitokeza wakati mmiliki wa Kampuni ya Pan Africa Power (PAP) Harbinder Singh Sethi na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira wakiwa tayari wamefikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya uhujumu uchumi, kutakatisha fedha na kusababisha hasara Serikali.

  Hali za uhakika zilizolifikia gazeti hili jana zilisema mitambo hiyo kwa sasa haizalishi umeme.

  MTANZANIA lilitembelea mitambo hiyo iliyoko Tegeta na kukuta wafanyakazi wachache ambao walikiri mitambo hiyo kutofanya kazi.

  "Mitambo ilizimwa tangu siku ile walipomkamata Sethi", alisema mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambaye hakuwa tayari kutajwa jina lake gazetini.

  Pamoja na hatua hiyo inaelezwa kuwa kuna hatari ya kuitaifishwa kwa mitambo hiyo hasa baada ya Serikali kuweka ngumu katika utoaji wa leseni mpya ya biashara ya kuzalisha umeme kwa kampuni hiyo.

  Licha ya hali hiyo leseni ya kampuni hiyo ilimalizika muda wake Julai 15, mwaka huu ambapo hadi sasa uamuzi wa kuitaifisha mitambo hiyo kurudi kuwa mali ya TANESCO ama laa ukisubiri uamuzi wa Ikulu.

  Kwa sababu hiyo, kama Serikali itaendelea na msimamo wake dhidi ya IPTL ndiyo utakuwa mwisho wa miaka 23 ya IPTL.

  Kampuni hiyo au IPTL iliingia nchini tangu mwaka 1994 na kila mwezi imekuwa ikilipwa Sh. bilioni 5.943 na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ikiwa ni gharama za uwekezaji mbali na gharama za umeme inaoliuzia shirika hilo.

  Novemba 2014, baada ya Bunge kujadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ilitoa maazimio manane ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO.

  Siku chache baada ya Bunge kupitisha uamuzi huo ambao ulifanyiwa kazi kwa haraka kwa Profesa Sospeter Muhongo kujiuzulu nafasi yake.
   
 2. Mr Miller

  Mr Miller JF-Expert Member

  #61
  Jul 17, 2017
  Joined: Jan 24, 2017
  Messages: 6,368
  Likes Received: 11,879
  Trophy Points: 280
  Nyerere nae alikuwepo!!
   
 3. Nolasc

  Nolasc Member

  #62
  Jul 17, 2017
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 25
  Kwan IPTL ilikuwa ikizalisha megawat ngapi ambazo zinamezwa na kinyelezi 1 na 2 ikikamilika hivyo hatuna shida na Umeme wao Wa kitapeli.

  Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
   
 4. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #63
  Jul 17, 2017
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 44,483
  Likes Received: 14,132
  Trophy Points: 280
  Hahahahah pamoja IPTL kujulikana madudu yake hakika haitapita siku 6 wale wakubadili gear angani wataanza kuwatetea kwa hofu ya mgao..watu wanataka mabadiliko lakini wanaogopa mgao wa umeme na wengine wanajaribu kuonesha hatuwezi kwenda bila IPTL...
   
 5. Mkendo

  Mkendo JF-Expert Member

  #64
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 14, 2013
  Messages: 2,014
  Likes Received: 753
  Trophy Points: 280
  CCM ndio walipitisha hii mikataba kwa mbwembwe nyingi....

  Mikataba mingi ya kitapeli mepitishwa na Serikali ya CCM.....

  Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
   
 6. fundi25

  fundi25 JF-Expert Member

  #65
  Jul 17, 2017
  Joined: Apr 16, 2013
  Messages: 5,645
  Likes Received: 2,613
  Trophy Points: 280
  Wauze chuma chakavu kwa mhindi mwenzake shubashi pateli
  Maana kiatu cha baniani dawa !!!
   
 7. Poise

  Poise JF-Expert Member

  #66
  Jul 17, 2017
  Joined: May 31, 2016
  Messages: 7,492
  Likes Received: 7,436
  Trophy Points: 280
  Siku moja niliandika hapa JF hivi "serikali ina mkono mrefu sana na jicho ang'avu Sana, utafanya madudu ila wakati ukifika, Bwana Pepsi atakukuta utaenda na maji.
   
 8. o

  olyanu JF-Expert Member

  #67
  Jul 17, 2017
  Joined: May 30, 2017
  Messages: 1,746
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Mtafika wapi?

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 9. o

  olyanu JF-Expert Member

  #68
  Jul 17, 2017
  Joined: May 30, 2017
  Messages: 1,746
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Sijui ndo maana ninauliza

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 10. o

  olyanu JF-Expert Member

  #69
  Jul 17, 2017
  Joined: May 30, 2017
  Messages: 1,746
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Swala Siyo kuzimwa au kung'olewa. Swala ni kwenda kwenye original agreement ambapo baada ya muda wa mkataba kuisha ilikuwa mitambo imikishwe kwa tanesco. What happened thereafter? MSG knows

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 11. o

  olyanu JF-Expert Member

  #70
  Jul 17, 2017
  Joined: May 30, 2017
  Messages: 1,746
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Wewe mchochezi. Muuze nini eti? Ngoja noah hiyoooooo

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 12. boyfriendy

  boyfriendy JF-Expert Member

  #71
  Jul 17, 2017
  Joined: Sep 9, 2012
  Messages: 1,954
  Likes Received: 658
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo kwa sasa wananufaika na capacity charge au na hiyo pia imefungwa?
  Alafu hiyo mitambo imezimwa yote wakati katika operation ili ibaki salama ilitakiwa mmoja utembee kufanya warmup vinginevyo baada ya muda hapo ni bonge la scraper hizo yaani zikilala down miezi kadhaa itabidi ipigwe major overall
   
 13. Pancras Suday

  Pancras Suday Verified User

  #72
  Jul 17, 2017
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,293
  Likes Received: 1,374
  Trophy Points: 280
  Ni bora mgao urudi lakini si kuwa na mafisadi kama hawa

  Sent from my iPhone 6s
   
 14. Ghosryder

  Ghosryder JF-Expert Member

  #73
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 6, 2014
  Messages: 9,310
  Likes Received: 2,270
  Trophy Points: 280
  Ndio ulivyoambiwa na Lissu or?
   
 15. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #74
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,350
  Likes Received: 1,907
  Trophy Points: 280
  Iptl haina mkataba halali na tanesco au serikali. The cost of forgery.
   
 16. Ghosryder

  Ghosryder JF-Expert Member

  #75
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 6, 2014
  Messages: 9,310
  Likes Received: 2,270
  Trophy Points: 280
  Amejitambua
   
 17. kmbwembwe

  kmbwembwe JF-Expert Member

  #76
  Jul 17, 2017
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 6,434
  Likes Received: 1,402
  Trophy Points: 280
  hiyo mitambo ya iptl kufuatana na mkataba wa awali ilitakiwa kua mali ya tanesco baada ya mkataba wa awali kumalizika. ila inaelekea wajanja walipoona mkataba unamalizika wakapora mitambo na kujipa mkataba mwingine..ndio bongo..
   
 18. c

  chidwadwa T New Member

  #77
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 17, 2017
  Messages: 2
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
 19. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #78
  Jul 17, 2017
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,695
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Ndio ndugu
  1. Inahusika na uzalishaji wa umeme wa mafuta mazito
  2. Inahusika na biashara ya gas ... ya lile bomba la mwanzo ... sio hili kubwa la TPDC
   
 20. Wonderful

  Wonderful JF-Expert Member

  #79
  Jul 17, 2017
  Joined: Apr 8, 2015
  Messages: 7,500
  Likes Received: 5,197
  Trophy Points: 280
  Hakuna kabisaaaaa!huku kwetu ni full taa kuanzia asbh hadi kuchwee!sasa sijui huo wao ulikua unapelekwa wapi!!
   
 21. c

  chikundi JF-Expert Member

  #80
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 16, 2016
  Messages: 8,214
  Likes Received: 2,251
  Trophy Points: 280
  Gesi ipulizwe hewani kutoa umeme bila miundo mbinu?

  Sent from my TECNO-C5 using JamiiForums mobile app
   
Loading...