Mitambo IPTL yazimwa, wakwama kufanya biashara ya umeme

Mitambo IPTL yazimwa, wakwama kufanya biashara ya umeme

Kampuni ya IPTL iliingia mkataba na Serikali mnamo 26 May, 1995; Kampuni hii ilikuwa na jukumu la kuuza umeme kwa TANESCO ktk kipindi cha dharura ya umeme kwa muda wa miaka 20. Mitambo ya IPTL ina capacity ya kuzalisha Megga Watt 100 (100Mw). Hivyo basi Mkataba ulikuwa ufikie mwisho wake rasmi mwaka 2015. Lakini inaelekea kulikuwa na figisu figisu zilizowezesha IPTL kuendelea kutafuna fedha za TANESCO hadi majuzi hawa vibaka ( Harbinder Seth & Ruge) waliposhtukiwa. IPTL ni muunganiko wa kampuni mbili yaani Kampuni ya MECHMAR ya Malaysia ikisimamiwa na Seth (70% ya share) na VIP Engineering ya Ruge (30% ya share).
Ni kweli hawawezi kuendelea kuungurumisha mitambo yao ya kuzalisha umeme bila ya kupewa go ahead (mkataba).
hao wa Malaysia walisepa long time baada tu ya mitambo kusimama wakapewa zengwe la ajabu.
 
Sasa hayo maelezo yana uhusiano gani na nilichoandika?!
Wewe umesema capacity charge haina uhusiano na kuisha kwa leseni kwakuwa mkataba bado uko hai, nami nikakuonyesha kuwa kutokuwa na leseni kutasababisha washindwe kuzalisha umeme na hivyo kukiuka masharti ya mkataba, na mkataba ukikiukwa unaweza kuvunjwa, na ukivunjwa capacity charge nayo inavunjwa, get it?
 
Sasa kama mliwapa wa kumkataba wa kununua umeme pale tu mnapohitaji ulitarajia nini?! Ingekuwa wewe ungekubali uwekeze mitambo lakini kuuza umeme ni hadi watakapotaka wao?!

Narudia, hata kama ingekuwa ni wakati wa Nyerere, so long as mkataba ulikuwa ni kununua umeme pale tu kunapokuwa na mahitaji basi katika mazingira kama hayo capacity charge ni LAZIMA!!! Kwahiyo hawakuwa wanakula pesa za bure... nature ya mkataba ndiyo iliyowapa haki ya capacity charge! Na suala la capacity charge lipo dunia mzima!!!
Sawa, ila duration ya miaka 23, probaly 28 years (2022) ni sahihi? Capacity charge ya bilioni 6 per month for 28yrs ni sahihi? 6bn x 12 = 72 bn per annum, 72bn x 28yrs = 2,016bn shs, yaani wavune shs. Trillion 2 bila kuzalisha hata unit 1 ya umeme??! Hiyo mitambo waliyowekeza inauzwa trillion ngapi?
 
Sawa wazime tu tumechoka na ufisadi, tena tunataka Serikali itaifishe mitambo hiyo

Sifa za maraisi walopita ni dhipi ikiwa nchi imetafunwa vyakutosha na itachukua karne kama si kizazi cha karne nyingine ili ijirudi hali.

Tunapoambiwa maraisi wana kinga inabidi wawe moto wakuwotea mbali ?maana kinga hii inawafanya wacharukwe kwavile untouchbly .

Maendeleo kwa Tanzania yatachukua muda kuja ikiwa kama kinga hii haikuondoshwa criminal is criminal tusivishane vilemba vya ukoka.
 
d7012b6a8fcb7940569328e3e746878c.jpg
Ni wingu zito. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya maombi ya Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kukwama, huku wakilazimika kuzima rasmi mitambo yao ya uzalishaji umeme.

Hatua hiyo imekuja baada ya kukwama kwa maombi ya kuongezewa muda wa miezi 55 ya leseni yake ya uzalishaji umeme kutokana na kusubiri uamuzi wa Ikulu.

Hali hiyo inajitokeza wakati mmiliki wa Kampuni ya Pan Africa Power (PAP) Harbinder Singh Sethi na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira wakiwa tayari wamefikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya uhujumu uchumi, kutakatisha fedha na kusababisha hasara Serikali.

Hali za uhakika zilizolifikia gazeti hili jana zilisema mitambo hiyo kwa sasa haizalishi umeme.

MTANZANIA lilitembelea mitambo hiyo iliyoko Tegeta na kukuta wafanyakazi wachache ambao walikiri mitambo hiyo kutofanya kazi.

"Mitambo ilizimwa tangu siku ile walipomkamata Sethi", alisema mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambaye hakuwa tayari kutajwa jina lake gazetini.

Pamoja na hatua hiyo inaelezwa kuwa kuna hatari ya kuitaifishwa kwa mitambo hiyo hasa baada ya Serikali kuweka ngumu katika utoaji wa leseni mpya ya biashara ya kuzalisha umeme kwa kampuni hiyo.

Licha ya hali hiyo leseni ya kampuni hiyo ilimalizika muda wake Julai 15, mwaka huu ambapo hadi sasa uamuzi wa kuitaifisha mitambo hiyo kurudi kuwa mali ya TANESCO ama laa ukisubiri uamuzi wa Ikulu.

Kwa sababu hiyo, kama Serikali itaendelea na msimamo wake dhidi ya IPTL ndiyo utakuwa mwisho wa miaka 23 ya IPTL.

Kampuni hiyo au IPTL iliingia nchini tangu mwaka 1994 na kila mwezi imekuwa ikilipwa Sh. bilioni 5.943 na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ikiwa ni gharama za uwekezaji mbali na gharama za umeme inaoliuzia shirika hilo.

Novemba 2014, baada ya Bunge kujadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ilitoa maazimio manane ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO.

Siku chache baada ya Bunge kupitisha uamuzi huo ambao ulifanyiwa kazi kwa haraka kwa Profesa Sospeter Muhongo kujiuzulu nafasi yake.
Hivi makanikia imeishia wapi!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa, ila duration ya miaka 23, probaly 28 years (2022) ni sahihi? Capacity charge ya bilioni 6 per month for 28yrs ni sahihi? 6bn x 12 = 72 bn per annum, 72bn x 28yrs = 2,016bn shs, yaani wavune shs. Trillion 2 bila kuzalisha hata unit 1 ya umeme??! Hiyo mitambo waliyowekeza inauzwa trillion ngapi?
Nilichosema kwa mazingira ya mkataba ulivyokuwa Capacity Charge ilikuwa haikwepeki, sijazungumzia suala la kiwango, kwa sababu, kufahamu ni kiwango gani kinastahili mtu unapaswa kufahamu mambo mengi. Kwa uchache... thamani ya uwekezaji (Fixed investment), investment operations costs (hizi, wawe wanauza umeme au hawauzi, wataendelea kuingia hizi gharama), anticipated annual turnover kutokana na makadirio ya umeme ambao wangeuza... hapo, at least, unaweza kukisia ni kiwango gani kilistahili!

Kwavile nafahamu no one, (including serikalini wenyewe) wanaweza kuwa na best estimation, ndo maana sijazungumzia suala la kiasi kama ni kingi, kidogo au ni sawa! Nasema hata serikali wenyewe hawawezi kuwa na best estimates kwa sababu, mkataba ni kununua umeme inapotokea dharula... no one knows dharula inaweza kutokea wakati gani!

Btw, kwanini umeweka miaka 28 wakat mkataba ulikuwa wa miaka 20 ?!

IPTL na serikali waliingia mkataba mara 3. Mara ya kwanza ilikuwa 1995; mara ya pili mwaka 1997 na mara ya tatu ni mwaka 2002. Mkataba wa kuuziana umeme uliingiwa mwaka 2002 kwa sababu ndipo walianza kuzalisha umeme rasmi. Mkataba ambao waliingia ulikuwa ni wa miaka 20 hadi mwaka 2022.

Sasa hiyo miaka 28 sijui umeitoa wapi!!!
 
Wewe umesema capacity charge haina uhusiano na kuisha kwa leseni kwakuwa mkataba bado uko hai, nami nikakuonyesha kuwa kutokuwa na leseni kutasababisha washindwe kuzalisha umeme na hivyo kukiuka masharti ya mkataba, na mkataba ukikiukwa unaweza kuvunjwa, na ukivunjwa capacity charge nayo inavunjwa, get it?
Kwanza, nilisema wazi mkataba sifahamu unasemaje lakini pili, attachment uliyoweka sio mkataba bali ni proposal ya Rugemalila kwenda serikalini!

Sijaona popote proposal ilipozungumzia suala la automatic contract termination inapotokea IPTL wanashindwa kuzalisha umeme! Sijaona popote walipozungumzia suala la leseni isipokuwa, Ruge anawashauri serikali kwamba waiambie IPTL ipunguze Capacity Charge at the expense of TANESCO's Right to end PPA!

Wametaja vifungu vinavyoipa (au vilivyokuwa vinaipa TANESCO) uwezo wa kuvunja PPA. Unless hizo clauses ungeziweka hapa, kinyume chake huwezi ku-conlude kwamba vinahusiana na suala la kushindwa kuzalisha umeme!

But on top of that, hizo clauses zenyewe hazielekei kama zinahusiana na suala la kushindwa kuzalisha umeme kwa sababu wameandika "...in order for the GOT to waive its right of allowing TANESCO to terminate the PPA for IPTL's continuing defaults under clauses....!"

Ikumbukwe, tangu IPTL inazaliwa hadi hii leo, ni full matatizo kiasi cha TANESCO kuwapeleka IPTL mahakamani (ICSID) hata kabla umeme hawajaanza kuzalisha. Na ukifuatilia kumbukumbu za IPTL, mwaka 1997 Mkapa aliagiza kabla ya chochote ufanyike uchunguzi kuhusu IPTL lakini cha ajabu, mwezi mmoja baadae serikali hiyo hiyo ambayo iliagiza IPTL ichunguzwe ikasaini mkataba na IPTL; mkataba ambao ulikuwa ndio msingi wa TANESCO kwenda ICSID ingawaje TANESCO walishindwa kesi!

Kwahiyo kuna kila dalili, Ruge alikuwa anazungumzia masuala ya sintofahamu yaliyokuwa yameingia IPTL na ndio maana katumia neno "...continuing default" kwa sababu, by the time, hata Ruge mwenyewe tayari walishaanza kutofautiana na mbia mwenzake!

Lakini hata kama nikitaka kukubaliana na maelezo yako, hapo IPTL/PAP hawajashindwa kuzalisha bali wameshindwa kuuza! IPTL sio wapumbavu wakubali kupewa haki kwa mkono wa kulia halafu hapo hapo waone wananyang'anywa hiyo haki kwa mkono wa kushoto!!

Kwamba, kama mkataba ulikuwa unasema under PPA lifetime, IPTL watakuwa na haki ya kulipwa Capacity Charge wauze umeme au wasiuze halafu hapo hapo kuwe na kipengele kinachosema, wasipouza umeme hawalipwi Capacity Charge wakati wanafahamu uuzaji wao umeme unategemea leseni toka kwa yule yule anayewapa haki ya Capacity Charge...!!!

Kama ndivyo, the whole PPA stuff ingekuwa meaningless kwa sababu, serikali ingenunua umeme mwaka mmoja tu wakati ule wana shida na baada ya hapo, wanagoma kutoa leseni kama ilivyo sasa na hivyo hawalipi capacity charge!!!!
 
Nilichosema kwa mazingira ya mkataba ulivyokuwa Capacity Charge ilikuwa haikwepeki, sijazungumzia suala la kiwango, kwa sababu, kufahamu ni kiwango gani kinastahili mtu unapaswa kufahamu mambo mengi. Kwa uchache... thamani ya uwekezaji (Fixed investment), investment operations costs (hizi, wawe wanauza umeme au hawauzi, wataendelea kuingia hizi gharama), anticipated annual turnover kutokana na makadirio ya umeme ambao wangeuza... hapo, at least, unaweza kukisia ni kiwango gani kilistahili!

Kwavile nafahamu no one, (including serikalini wenyewe) wanaweza kuwa na best estimation, ndo maana sijazungumzia suala la kiasi kama ni kingi, kidogo au ni sawa! Nasema hata serikali wenyewe hawawezi kuwa na best estimates kwa sababu, mkataba ni kununua umeme inapotokea dharula... no one knows dharula inaweza kutokea wakati gani!

Btw, kwanini umeweka miaka 28 wakat mkataba ulikuwa wa miaka 20 ?!

IPTL na serikali waliingia mkataba mara 3. Mara ya kwanza ilikuwa 1995; mara ya pili mwaka 1997 na mara ya tatu ni mwaka 2002. Mkataba wa kuuziana umeme uliingiwa mwaka 2002 kwa sababu ndipo walianza kuzalisha umeme rasmi. Mkataba ambao waliingia ulikuwa ni wa miaka 20 hadi mwaka 2022.

Sasa hiyo miaka 28 sijui umeitoa wapi!!!
Usilete porojo nyingi, jifunze kwenda straight to the point when needed. Capacity charge haikwepeki, kweli. Ila capacity charge mara 100 ya capacity charge 'range' inakwepeka. Hayo maelezo mengine ni sawa na kujaribu kujustify pipi ya kijiti kuuzwa shs. 10,000/ = badala yakuuzwa kati ya 200/= hadi 500/=. " ooh.., unajua hii pipi ina bluetooth na whatsapp, pia imeongezewa facebook yenye chocolate flavour..", come on man....! By the way 2022 - 1994 = 28.
 
Kutoa conclusion kwa vitu usivyo na facts wakati issue inahitaji fact ndizo porojo zenyewe hizo!!!

Na ndio maana suala lililohitaji kuweka mkataba wewe ukaweka barua ya Ruge kama defending doc halafu unataka ku-draw conclusion kutoka kwenye invalid doc... that's not my style!!

Lingine nililokuuliza 28 years umetoa wapi! Jibu lako ni 2022-1994 wakati hapa tunazungumzia PPA ambayo ilisainiwa 2002 na sio 1994!!

Hii unaonesha unaongea mambo usiyoyajua au una-conclude kupitiana hoja usizo na uhakika nazo!

Kuongea usoyoyajua na kuyafanyia conclusion ndiyo porojo zenyewe hizo!

Lakini hata kama ulikuwa unachanganya mikataba still the original contract haikuwa 1994 bali May 1995 !! Again, unaonesha unaongea vitu ambavyo hauna taarifa nazo za kutosha! Na kuongea mambo usiyo na taarifa nazo za kutosha na kufanya conclusion kupitia invalid info ndo porojo zenyewe hizo!!

Na kama unaona nilichoongea ni kuhalalisha capacity charge inayolipwa wakati nimeshakuambia siwezi kusema sahihi au hapana then unaonesha hutakaa ukaweza kunielewa kamwe manake sio staili yangu ku-conclude kwa kutumia my own assumptions!

Hoja yangu from the beginning imekuwa kwamba kutokana na mkataba walioingia, Capacity Charge ilikuwa haikwepeki! Sijaongea popote kuonesha kama CC ni kubwa, ndogo au kiwango kinachotozwa ni sahihi!

Uwe unaelewa msingi wa hoja!!
 
Since your way of thinking is different from mine, then lets agree to disagree.Maana naona hapo ndipo tatizo lilipo. In the mean time, endelea tu kusubiri huo udhibitisho wa pipi ya kijiti kuuzwa shs.10,000/=.(Ushauri: Don't behave like a programmable robot, ease up a lil')

When Does a Theory Become a Law? | The Happy Scientist
 
Back
Top Bottom