Mitambo IPTL yazimwa, wakwama kufanya biashara ya umeme | Page 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mitambo IPTL yazimwa, wakwama kufanya biashara ya umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ghazwat, Jul 17, 2017.

 1. Ghazwat

  Ghazwat JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 4, 2015
  Messages: 16,525
  Likes Received: 48,893
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Ni wingu zito. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya maombi ya Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kukwama, huku wakilazimika kuzima rasmi mitambo yao ya uzalishaji umeme.

  Hatua hiyo imekuja baada ya kukwama kwa maombi ya kuongezewa muda wa miezi 55 ya leseni yake ya uzalishaji umeme kutokana na kusubiri uamuzi wa Ikulu.

  Hali hiyo inajitokeza wakati mmiliki wa Kampuni ya Pan Africa Power (PAP) Harbinder Singh Sethi na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira wakiwa tayari wamefikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya uhujumu uchumi, kutakatisha fedha na kusababisha hasara Serikali.

  Hali za uhakika zilizolifikia gazeti hili jana zilisema mitambo hiyo kwa sasa haizalishi umeme.

  MTANZANIA lilitembelea mitambo hiyo iliyoko Tegeta na kukuta wafanyakazi wachache ambao walikiri mitambo hiyo kutofanya kazi.

  "Mitambo ilizimwa tangu siku ile walipomkamata Sethi", alisema mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambaye hakuwa tayari kutajwa jina lake gazetini.

  Pamoja na hatua hiyo inaelezwa kuwa kuna hatari ya kuitaifishwa kwa mitambo hiyo hasa baada ya Serikali kuweka ngumu katika utoaji wa leseni mpya ya biashara ya kuzalisha umeme kwa kampuni hiyo.

  Licha ya hali hiyo leseni ya kampuni hiyo ilimalizika muda wake Julai 15, mwaka huu ambapo hadi sasa uamuzi wa kuitaifisha mitambo hiyo kurudi kuwa mali ya TANESCO ama laa ukisubiri uamuzi wa Ikulu.

  Kwa sababu hiyo, kama Serikali itaendelea na msimamo wake dhidi ya IPTL ndiyo utakuwa mwisho wa miaka 23 ya IPTL.

  Kampuni hiyo au IPTL iliingia nchini tangu mwaka 1994 na kila mwezi imekuwa ikilipwa Sh. bilioni 5.943 na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ikiwa ni gharama za uwekezaji mbali na gharama za umeme inaoliuzia shirika hilo.

  Novemba 2014, baada ya Bunge kujadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ilitoa maazimio manane ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO.

  Siku chache baada ya Bunge kupitisha uamuzi huo ambao ulifanyiwa kazi kwa haraka kwa Profesa Sospeter Muhongo kujiuzulu nafasi yake.
   
 2. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #41
  Jul 17, 2017
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 19,348
  Likes Received: 12,476
  Trophy Points: 280
  Mkuu tukiachana na Mkataba na leseni juu ya hii kampuni.....tukumbuke kuna maazimio ya Bunge ambayo mpaka sasa hayajatekelezwa.
   
 3. H

  Haruni George Vassardanis Member

  #42
  Jul 17, 2017
  Joined: Feb 16, 2017
  Messages: 13
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  H

  HAITUMIKI,JE CAPACITY CHARGE TUNAENDELEA KULIPA?
   
 4. H

  Halichachi JF-Expert Member

  #43
  Jul 17, 2017
  Joined: Feb 24, 2017
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1,565
  Trophy Points: 280
  Lakini Capacity Charge si inaingia kila siku hata wasipozalisha?
   
 5. k

  kindikwili JF-Expert Member

  #44
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 5, 2016
  Messages: 1,596
  Likes Received: 2,349
  Trophy Points: 280
  Jaly 15 mwaka gani mbona hueleweki mkuu? Leseni yao iliisha July 15 ila mkataba wao bado upo mpaka mwaka 2020 HV nadhani ndiyo maana waliomba kuongezewa uhai wa leseni kwa miezi 55 kutoka July 15 mwaka huu

  Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
   
 6. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #45
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 15,469
  Likes Received: 7,751
  Trophy Points: 280
  Mitambo ya IPTL imezimwa rasmi baada ya kukwama kwa maombi ya kuongezewa muda wa miezi 55 ya leseni yake ya uzalishaji umeme.

  NI wingu zito, ndivyo unavyoweza kusema baada ya maombi ya Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kukwama, huku wakilazimika kuzima rasmi mitambo yao ya uzalishaji umeme.

  Hatua hiyo imekuja baada ya kukwama kwa maombi ya kuongezewa muda wa miezi 55 ya leseni yake ya uzalishaji umeme kutokana na kusubiri uamuzi wa Ikulu.

  Hali hiyo inajitokeza wakati mmiliki wa Kampuni ya Pan Afrika Power (PAP), Harbinder Singh Sethi na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira wakiwa tayari wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya uhujumu uchumi, kutakatisha fedha na kuisababishia hasara Serikali.

  Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili jana zilisema mitambo hiyo kwa sasa haizalishi umeme. MTANZANIA lilitembelea mitambo hiyo iliyoko Tegeta na kukuta wafanyakazi wachache ambao walikiri mitambo hiyo kutofanya kazi.

  “Mitambo ilizimwa tangu siku ile walipomkamata Sethi,” alisema mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambaye hakuwa tayari kutajwa jina lake gazetini.

  Pamoja na hatua hiyo inaelezwa kuwa kuna hatari ta kuitaifishwa kwa mitambo hiyo hasa baada ya Serikali kuweka ngumu katika utoaji wa leseni mpya ya biashara ya kuzalisha umeme kwa kampuni hiyo.

  Licha ya hali hiyo leseni ya kampuni hiyo ilimalizika muda wake Julai 15, mwaka huu ambapo hadi sasa uamuzi wa kuitafisha mitambo hiyo kurudi kuwa mali za Tanesco ama laa ukisubiri uamuzi wa Ikulu.

  Kwa sababu hiyo, kama Serikali itaendelea na msimamo wake dhidi ya IPTL ndiyo utakuwa mwisho wa miaka 23 ya IPTL. Kampuni hiyo ya IPTL iliingia chini tangu mwaka 1994 na kila mwezi imekuwa ikilipwa Sh. bilioni 5.943 na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ikiwa ni gharama za uwekezaji mbali na gharama za umeme inaoliuzia shirika hilo.

  Novemba 2014, baada ya Bunge kujadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ilitoa maazimio manane ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa Tanesco.

  Siku chache baada ya Bunge kupitisha uamuzi huo ambao ulifanyiwa kazi kwa haraka kwa Profesa Sospeter Muhongo kujiuzulu nafasi yake.

  Wengine ni Profesa Anna Tibaijuka ambaye pia alijiuzulu nafasi ya Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Jaji Frederick Werema aliyejiuzulu nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

  Eliachim Maswi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini alisimamishwa kazi pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanesco waliotakiwa kuwajibishwa, kukaa pembeni baada ya muda wa bodi yao kwisha na ikaundwa nyingine.

  Naye Spika wa Bunge wakati huo, Anne Makinda alitangaza kuwa wazi nafasi za wenyeviti wa kamati za Bunge ambao ni William Ngeleja, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, Andrew Chenge aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti na Victor Mwambalaswa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini.

  Azimio jingine lililotaka Harbinder Singh Seth ambaye ni Mwenyekiti wa PAP kufikishwa mahakamani, lilitekelezwa hivi karibuni ambako yeye na mwenzake James Rugemalira wa VIP Engineering, walifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka 12 yakiwamo ya uhujumu uchumi na kutakatisha fedha.

  Baadhi ya maazimio ambayo yalikuwa hayajafanyiwa kazi ni lile la pili lilolotaka Serikali iangalie uwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO.

  Mei 11, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, wakati wa maswali ya papo kwa papo bungeni, alimuhoji Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu kutokutekelezwa maazimio hayo ya Bunge kuhusu Escrow.

  Akijibu swali hilo, Majaliwa alimuhakikishia Mbowe kuwa Serikali inaheshimu muhimili wa Bunge na kuthamini uamuzi wake. Alisema kunahitajika uchunguzi wa kina na yapo mambo ambayo yana umuhimu wa kufikishwa bungeni hivyo uchunguzi wa Serikali utakapokamilika yatawasilishwa bungeni.

  Kwa sababu hiyo, inawezekana kuisha leseni hiyo ya IPTL sasa, kukachukuliwa kama moja ya njia ya kutekeleza azimio la lipi la Bunge.

  Pia Juni 20 mwaka huu, akiwa ziarani mkoani Pwani, Rais John Magufuli, alisema serikali itaendelea kuchukua hatua dhidi ya watu wanaolihujumu Taifa ikiwamo kujihusisha na vitendo vya wizi na rushwa na haitakatishwa tamaa na watu wanaolalamika na kubeza juhudi hizo.

  “Stiegler’s Gorge, mradi ambao ulifanyiwa utafiti tangu enzi ya Mwalimu Nyerere tukautelekeza. Nataka tujenge bwawa litakalozalisha umeme utakaotosheleza katika nchi yetu, nchi ya viwanda ili Watanzania wasilalamikie tena suala la umeme, nataka tuachane na umeme wa matapeli wanaokuja hapa wanawekeza kwa lengo la kutuibia.”

  “Mimi nachukia wezi na kwa kweli wezi watakoma tu, awe mwizi wa Tanzania, awe mwizi wa Ulaya, awe anatoka magharibi, mashariki, kaskazini au kusini, mwizi ni mwizi tu,” alisema Rais Magufuli.

  IPTL imekuwa ikilalamikiwa kuwa ni miongoni mwa miradi inayoiumiza Tanesco, hivyo kauli hiyo ya mkuu wa nchi inaweza kuwa siyo ishara njema kwa kampuni hiyo.

  Chanzo: MTANZANIA
   
 7. o

  olyanu JF-Expert Member

  #46
  Jul 17, 2017
  Joined: May 30, 2017
  Messages: 1,843
  Likes Received: 1,058
  Trophy Points: 280
  Lakini capacity charge si bado inalipwa as per contract?

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 8. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #47
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 23,464
  Likes Received: 14,541
  Trophy Points: 280
  Tuvumiliane...tutafika tu!
   
 9. n

  ndayilagije JF-Expert Member

  #48
  Jul 17, 2017
  Joined: Nov 7, 2016
  Messages: 5,883
  Likes Received: 5,988
  Trophy Points: 280
  Lazima tuheshimiane mjini.

  Sent from my TECNO 7C using JamiiForums mobile app
   
 10. Joseverest

  Joseverest Verified User

  #49
  Jul 17, 2017
  Joined: Sep 25, 2013
  Messages: 38,889
  Likes Received: 45,588
  Trophy Points: 280
  Kabisa mkuu
   
 11. balimar

  balimar JF-Expert Member

  #50
  Jul 17, 2017
  Joined: Sep 18, 2015
  Messages: 2,850
  Likes Received: 3,379
  Trophy Points: 280
  Kinyerezi's si zipo?
   
 12. Ban2Ban

  Ban2Ban Senior Member

  #51
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 7, 2015
  Messages: 133
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Una uhakika?
   
 13. B

  Bayyo JF-Expert Member

  #52
  Jul 17, 2017
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,254
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Hiyo mitambo bora ing'olewe kabisa, kuzimwa tu haiyoshi... Wameshatuibia sana watanzania
   
 14. m

  mtanzania1989 JF-Expert Member

  #53
  Jul 17, 2017
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 2,383
  Likes Received: 2,172
  Trophy Points: 280
  Hawana leseni, kwa lugha nyepesi IPTL haina mamlaka ya kuendelea na shughuli zake wala kulipwa chochote tangu July 15 leseni yao ilipoisha muda.
   
 15. K

  K tea shop Member

  #54
  Jul 17, 2017
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 25
  GESI YA MTWARA SI IPO?

  KWA NINI MSITUMIE GESI KUWASHA UMEME NCHI NZIMA?
   
 16. darubin

  darubin JF-Expert Member

  #55
  Jul 17, 2017
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,069
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  sasa wafanya kazi vipi, daaa kuajiriwa huku mateso mpaka unazikwa
   
 17. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #56
  Jul 17, 2017
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,921
  Trophy Points: 280
  Hii makala ya wakala wa IPTL. Kwamba nchi hii haina jeuri ya kuwa na umeme bila IPTL si bora tuuze bombadear moja tuongeze uzalishaji umeme
   
 18. FRANCIS DA DON

  FRANCIS DA DON JF-Expert Member

  #57
  Jul 17, 2017
  Joined: Sep 4, 2013
  Messages: 11,703
  Likes Received: 5,905
  Trophy Points: 280
  For 23 years wamekua wakila monthly pension ya billion 6 bila kufanya kazi yeyote ile.., bure kabisa
   
 19. s

  singojr JF-Expert Member

  #58
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 28, 2014
  Messages: 3,480
  Likes Received: 3,552
  Trophy Points: 280
  Toka 1994 sijaanza hata chekechea jamaa wamekula hela sanaaa
   
 20. chengbi

  chengbi Senior Member

  #59
  Jul 17, 2017
  Joined: May 5, 2017
  Messages: 111
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  hongera japo siyo sana ila kweli kuna Nazi inafanyika

  iPhone 6
   
 21. MOTOCHINI

  MOTOCHINI JF-Expert Member

  #60
  Jul 17, 2017
  Joined: Jan 20, 2014
  Messages: 24,132
  Likes Received: 12,680
  Trophy Points: 280
  Sikuzingine unajitoa ufahamu
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...