Mitambo IPTL yazimwa, wakwama kufanya biashara ya umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mitambo IPTL yazimwa, wakwama kufanya biashara ya umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ghazwat, Jul 17, 2017.

 1. Ghazwat

  Ghazwat JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 4, 2015
  Messages: 15,755
  Likes Received: 47,974
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Ni wingu zito. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya maombi ya Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kukwama, huku wakilazimika kuzima rasmi mitambo yao ya uzalishaji umeme.

  Hatua hiyo imekuja baada ya kukwama kwa maombi ya kuongezewa muda wa miezi 55 ya leseni yake ya uzalishaji umeme kutokana na kusubiri uamuzi wa Ikulu.

  Hali hiyo inajitokeza wakati mmiliki wa Kampuni ya Pan Africa Power (PAP) Harbinder Singh Sethi na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira wakiwa tayari wamefikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya uhujumu uchumi, kutakatisha fedha na kusababisha hasara Serikali.

  Hali za uhakika zilizolifikia gazeti hili jana zilisema mitambo hiyo kwa sasa haizalishi umeme.

  MTANZANIA lilitembelea mitambo hiyo iliyoko Tegeta na kukuta wafanyakazi wachache ambao walikiri mitambo hiyo kutofanya kazi.

  "Mitambo ilizimwa tangu siku ile walipomkamata Sethi", alisema mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambaye hakuwa tayari kutajwa jina lake gazetini.

  Pamoja na hatua hiyo inaelezwa kuwa kuna hatari ya kuitaifishwa kwa mitambo hiyo hasa baada ya Serikali kuweka ngumu katika utoaji wa leseni mpya ya biashara ya kuzalisha umeme kwa kampuni hiyo.

  Licha ya hali hiyo leseni ya kampuni hiyo ilimalizika muda wake Julai 15, mwaka huu ambapo hadi sasa uamuzi wa kuitaifisha mitambo hiyo kurudi kuwa mali ya TANESCO ama laa ukisubiri uamuzi wa Ikulu.

  Kwa sababu hiyo, kama Serikali itaendelea na msimamo wake dhidi ya IPTL ndiyo utakuwa mwisho wa miaka 23 ya IPTL.

  Kampuni hiyo au IPTL iliingia nchini tangu mwaka 1994 na kila mwezi imekuwa ikilipwa Sh. bilioni 5.943 na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ikiwa ni gharama za uwekezaji mbali na gharama za umeme inaoliuzia shirika hilo.

  Novemba 2014, baada ya Bunge kujadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ilitoa maazimio manane ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO.

  Siku chache baada ya Bunge kupitisha uamuzi huo ambao ulifanyiwa kazi kwa haraka kwa Profesa Sospeter Muhongo kujiuzulu nafasi yake.
   
 2. MKWEPA KODI

  MKWEPA KODI JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2017
  Joined: Nov 28, 2015
  Messages: 19,915
  Likes Received: 42,185
  Trophy Points: 280
  Sawa wazime tu tumechoka na ufisadi, tena tunataka Serikali itaifishe mitambo hiyo
   
 3. wambura marwa

  wambura marwa JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 7, 2015
  Messages: 2,180
  Likes Received: 1,097
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo mkataba mpya vipi

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 4. Lukubigwa

  Lukubigwa Member

  #4
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 12, 2017
  Messages: 23
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 5
  Awamu ya 5 hii

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 5. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,967
  Likes Received: 683
  Trophy Points: 280
  Nombeni kujilishwa kama hizi ni Kampuni Mbili tofauti.

  1. PAN AFRICA POWER
  2. PAN AFRICA ENERGY
   
 6. m

  masaduku JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2017
  Joined: Feb 6, 2016
  Messages: 357
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  MUNGU MKUBWA NA IZIMWE ILI TUWEZE KUWEKA MKATABA MPYA NA WENYE MITAMBO HIYO? NA WATUMIE GESI NA BEI ISHUKE TENA CHINI YA WENZAO MAANA UNUNUZI WA MITAMBO TULISHALIPIA TAYARI SASA WAKO KWENYE FAIDA TU.
   
 7. Al-Watan

  Al-Watan JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2017
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,981
  Likes Received: 14,078
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo mgawo (wa umeme) unarudi au vipi?

  Sent from my Kimulimuli
   
 8. mbalizi1

  mbalizi1 JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2017
  Joined: Dec 16, 2015
  Messages: 7,557
  Likes Received: 8,502
  Trophy Points: 280
  Taarabu inapigwa
   
 9. Root

  Root JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2017
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,955
  Likes Received: 13,784
  Trophy Points: 280
  Sawa ila tusipate mgao wa umeme au baadae tusijepelekwa mahakamani kudaiwa
   
 10. kipara kipya

  kipara kipya JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2017
  Joined: May 2, 2016
  Messages: 4,061
  Likes Received: 3,662
  Trophy Points: 280
  Tangu ilipozimwa je kuna upungufu wa umeme mtujuze sisi wa vijijini!
   
 11. Perfectz

  Perfectz JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2017
  Joined: May 17, 2017
  Messages: 4,987
  Likes Received: 9,891
  Trophy Points: 280
  KAMA WAMEIZIMA BASI WATUAMBIE TUKAPIME VYUMA CHAKAVU.HATUTAKI UCHAFU SISI

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 12. tameer

  tameer JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 508
  Likes Received: 751
  Trophy Points: 180
  Kurudisha ulichodhulumiwa ni haki,iwe kwa busara au kwa nguvu
   
 13. barafuyamoto

  barafuyamoto JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 26, 2014
  Messages: 23,586
  Likes Received: 15,691
  Trophy Points: 280
  Id yako imevamiwa au??
   
 14. barafuyamoto

  barafuyamoto JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 26, 2014
  Messages: 23,586
  Likes Received: 15,691
  Trophy Points: 280
  Mkataba umeisha, wanatupelekaje mahakamani??
   
 15. MKWEPA KODI

  MKWEPA KODI JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2017
  Joined: Nov 28, 2015
  Messages: 19,915
  Likes Received: 42,185
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwenye ukweli ni lazima tuseme ukweli, msema Kweli ni mpenzi wa Mungu tetetetetetete
   
 16. Ghazwat

  Ghazwat JF-Expert Member

  #16
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 4, 2015
  Messages: 15,755
  Likes Received: 47,974
  Trophy Points: 280
  Yah.. Hatupingi kila kitu ila tupinga mambo mengine namna yanavyofanyika.
   
 17. barafuyamoto

  barafuyamoto JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 26, 2014
  Messages: 23,586
  Likes Received: 15,691
  Trophy Points: 280
  Nakuunga mkono kabisa kwenye hili!!
   
 18. A

  Abdallah M. Nassor Verified User

  #18
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 20, 2008
  Messages: 592
  Likes Received: 594
  Trophy Points: 180
  Kama imezimwa tokea alipokamatwa, Je kuna athari zozote zilizojitokeza za upungufu wa Umeme/ Maana sijaona kama kuna kukatika katika au mgao wa umeme hapa mjini, inaonesha kuwa wale walikuwa wezi tu na hakuna msaada mkubwa waliokuwa wakiutoa TANESCO
   
 19. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2017
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,835
  Likes Received: 1,017
  Trophy Points: 280
  Ruge sio mmiliki tena wa IPTL...aliuza share zake kwa Singa.
  Na hii mitambo haifanyi kazi kwa sasa. Haijazimwa kwa maana ya hoja.
  Mitambo hii huwashwa pale tu tunapokuwa na upungufu wa umeme unaozalishwa na Tanesco...sasa hivi hakuna upungufu hivyo hautumiki.
   
 20. robert sendabishaka

  robert sendabishaka JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2017
  Joined: Dec 11, 2015
  Messages: 1,369
  Likes Received: 1,058
  Trophy Points: 280
  looh! '...... vipofu wanaona, viziwi wanasikia na mabubu wanaongea. lakini usimwambie mtu yeyote habari hizi'
   
Loading...