Mitambo IPTL yazimwa, wakwama kufanya biashara ya umeme

Ni hela zenu hivyo anajua anatoa 0.5 tu ya pato lake.!
ndio maana nimekwambia yy alijitahidi kwenye kulipa wafanyakazi hayo makosa mengine ni yake mbona mafisadi wengine wanakimbiza pesa tu nje hata duka hafungui bongo
 
Migao mikali ilikuwa inasababishwa na ukame na wapiga dili wenye plants binafsi za kuzaliwa Umeme(hawa wako wengi sana, japo iptl ndo maarufu). Kumekuwa na mvua za kutosha na kinyerezi imejengwa plant nyingine, hivyo hata kama kutakuwa na mgao basi utakuwa ule tuliouzoea.

Ikumbukwe iptl ilikuwa inatumika kunapokuwa na mahitaji makubwa, mfano jioni au wakati wa sikukuu.
Mgawo mkali unakuwaje na usiokuwa mkali unakuwaje?
 
d7012b6a8fcb7940569328e3e746878c.jpg
Ni wingu zito. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya maombi ya Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kukwama, huku wakilazimika kuzima rasmi mitambo yao ya uzalishaji umeme.

Hatua hiyo imekuja baada ya kukwama kwa maombi ya kuongezewa muda wa miezi 55 ya leseni yake ya uzalishaji umeme kutokana na kusubiri uamuzi wa Ikulu.

Hali hiyo inajitokeza wakati mmiliki wa Kampuni ya Pan Africa Power (PAP) Harbinder Singh Sethi na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira wakiwa tayari wamefikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya uhujumu uchumi, kutakatisha fedha na kusababisha hasara Serikali.

Hali za uhakika zilizolifikia gazeti hili jana zilisema mitambo hiyo kwa sasa haizalishi umeme.

MTANZANIA lilitembelea mitambo hiyo iliyoko Tegeta na kukuta wafanyakazi wachache ambao walikiri mitambo hiyo kutofanya kazi.

"Mitambo ilizimwa tangu siku ile walipomkamata Sethi", alisema mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambaye hakuwa tayari kutajwa jina lake gazetini.

Pamoja na hatua hiyo inaelezwa kuwa kuna hatari ya kuitaifishwa kwa mitambo hiyo hasa baada ya Serikali kuweka ngumu katika utoaji wa leseni mpya ya biashara ya kuzalisha umeme kwa kampuni hiyo.

Licha ya hali hiyo leseni ya kampuni hiyo ilimalizika muda wake Julai 15, mwaka huu ambapo hadi sasa uamuzi wa kuitaifisha mitambo hiyo kurudi kuwa mali ya TANESCO ama laa ukisubiri uamuzi wa Ikulu.

Kwa sababu hiyo, kama Serikali itaendelea na msimamo wake dhidi ya IPTL ndiyo utakuwa mwisho wa miaka 23 ya IPTL.

Kampuni hiyo au IPTL iliingia nchini tangu mwaka 1994 na kila mwezi imekuwa ikilipwa Sh. bilioni 5.943 na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ikiwa ni gharama za uwekezaji mbali na gharama za umeme inaoliuzia shirika hilo.

Novemba 2014, baada ya Bunge kujadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ilitoa maazimio manane ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO.

Siku chache baada ya Bunge kupitisha uamuzi huo ambao ulifanyiwa kazi kwa haraka kwa Profesa Sospeter Muhongo kujiuzulu nafasi yake.
waswshili wanasema ukimchunguza kuku utumbo huwezi kumla..mi nasema ukiichunguza iptl utumbo waweza zimia..
 
Ngoja niweke blah blah pembeni na kujifanya mzalendo linapokuja suala la Capacity Charge under normal condition. I am talking from business point of view na sio from (fake) nationalism point of view.

Hapa kuna mambo mawili... Power Purchase Agreement (PPA) na Leseni ya Uuzaji umeme!!!

PPA ni makubaliano kati ya serikali na IPTL kuuziana umeme pale kunapokuwa na hayo mahitaji! Mkataba huu ilikuwa ni IPTL kutuuzia umeme pale tu tunapokuwa na mahitaji ya ziada ya umeme... hususani pale tunapokuwa na upungufu wa uzalishaji umeme kutoka vyanzo vingine, hususan vyanzo vya maji!

Kwavile mkataba haukuwa kununua umeme wa IPTL wakati wote, hapo Capacity Charge haikwepeki hata kama ingekuwa ni wakati wa Nyerere! Hii ni kwa sababu, endapo mabwawa yetu yanakuwa na maji mwaka mzima, ina maana mitambo ya IPTL nayo ingezimwa mwaka mzima! Kama tusingekuwa na uhaba kwa miaka 5, ina maana mitambo ya IPTL nayo ingezimwa kwa miaka 5!!!!

Sasa sijui ni Mwekezaji gani angekubali aje kuwekeza mitambo kisha iwe inakaa hata mwaka mzima na zaidi bila kuingiza hata senti tano wakati kuna cost of wear and tear!!!

Hivyo kabla hatujaenda mbali, Capacity Charge haikuwa dhuluma bali tulipaswa kulipa kutokana na nature ya mkataba tulioingia!!!

Ki-Tanzania ukisema hivyo unaambiwa sio Mzalendo as if Uzalendo ni kuwa Mjinga na Mbumbumbu!!!

Je, kwa sasa bado tunapaswa kulipa Capacity Charge?!

REMEMBER... kuna Mkataba wa Kuuziana Umeme na Leseni ya Kuuza Umeme! Hivyo ni vitu viwili tofauti!!! Jambo la kuhoji, Capacity Charge inatokana na nini? Inatokana na Mkataba wa Kununua Umeme au Leseni ya Kuuza Umeme?

Kwa maoni yangu, kwavile sifahamu mkataba upo vipi, Capacity Charge inatokana na Mkataba wa Kuuziana Umeme na sio Leseni ya Kuuza Umeme!!!

Capacity Charge inatokana na Mkataba wa Kununua Umeme kwa sababu, kama mkataba ungekuwa ni kuuziana umeme bila conditional ya mahitaji, yaani kuuziana continuously, basi Capacity Charge kuna uwezekano isingekuwapo! As we speak, Mkataba wa Kununua Umeme unaisha mwaka 2022.

So, unless Mkataba wa Kununua Umeme unavunjwa mapema iwezekanavyo, kuna hatari tutaendelea kulipa Capacity Charge hata kama kupitia mahakamani!!! Au, tutaendelea kulipa CC hadi pale mkataba utaakapovunjwa rasmi kama kuna hiyo room ya kuvunja!!!!

Hapo juu tena, kwa mujibu wa Tanzania yangu, nina sifa ya kuitwa sio Mzalendo kwa sababu wanadhani Uzalendo ni kuwa Mjinga au kufumbia macho FACTS!

REMEMBER, Haki na Sheria ni mambo mawili tofauti!!!!
As usual Mkuu Chige at your own best! Asante kwa darasa! Je haiwezekani kukubaliana viwango wa tofauti vya capacity charge kulingana na mahitaji yetu ya nishati?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nombeni kujilishwa kama hizi ni Kampuni Mbili tofauti.

1. PAN AFRICA POWER
2. PAN AFRICA ENERGY

Usifukue Makaburi!
Hawa wameshika mpaka vitalu vya Gesi na Mafuta. Ule wimbo wa sio fedha za serikali waliimba watu wengi na haikuwa bure. Kumbuka maneno ya Waziri Mkuu Pinda ukiwagusa mafisadi nchi itatetemeka habari ndio hizo. Nalaani mkataba wa Zanzibar uliofuta Azimio la Arusha !
 
Hakuna athari yeyote ila wana mkataba hai....hilo ni pigo sio kwao tu wakitaifisha wawekezaji hawatakuja inabidi watumie akili sanaa nini cha kufanya!! Mwekezaji akija anakuw haelewi kama akikosea lolote halindwi na mkataba!! Ni tishio kwa wawekezaji!! Tuone busara kama ipo au hakuna kabisa!! Yeye ataondoka next 8yrs unaachaje nchi umevuruga miaka 100 mingine?? Sera za uwekezaji Zipo ila zinavunjwa nani atajenga viwanda?? Labda wajenge serikali.......maana wengine wataogopa!!! Makampuni mengi ya exploration yameamua kuondoka!!! Nani atakuja kwa hali ilivyo?? Sio rahisi kuwekeza kwenye risk!!!!
Risk ipi? Ile risk ya kula billion 6 kila mwezi kiulaini kabisa, ufanye kazi au usifanye kazi ni uamuzi wako, 6B yako iko pale pale, au risk ipi unazungumzia?
 
Ngoja niweke blah blah pembeni na kujifanya mzalendo linapokuja suala la Capacity Charge under normal condition. I am talking from business point of view na sio from (fake) nationalism point of view.

Hapa kuna mambo mawili... Power Purchase Agreement (PPA) na Leseni ya Uuzaji umeme!!!

PPA ni makubaliano kati ya serikali na IPTL kuuziana umeme pale kunapokuwa na hayo mahitaji! Mkataba huu ilikuwa ni IPTL kutuuzia umeme pale tu tunapokuwa na mahitaji ya ziada ya umeme... hususani pale tunapokuwa na upungufu wa uzalishaji umeme kutoka vyanzo vingine, hususan vyanzo vya maji!

Kwavile mkataba haukuwa kununua umeme wa IPTL wakati wote, hapo Capacity Charge haikwepeki hata kama ingekuwa ni wakati wa Nyerere! Hii ni kwa sababu, endapo mabwawa yetu yanakuwa na maji mwaka mzima, ina maana mitambo ya IPTL nayo ingezimwa mwaka mzima! Kama tusingekuwa na uhaba kwa miaka 5, ina maana mitambo ya IPTL nayo ingezimwa kwa miaka 5!!!!

Sasa sijui ni Mwekezaji gani angekubali aje kuwekeza mitambo kisha iwe inakaa hata mwaka mzima na zaidi bila kuingiza hata senti tano wakati kuna cost of wear and tear!!!

Hivyo kabla hatujaenda mbali, Capacity Charge haikuwa dhuluma bali tulipaswa kulipa kutokana na nature ya mkataba tulioingia!!!

Ki-Tanzania ukisema hivyo unaambiwa sio Mzalendo as if Uzalendo ni kuwa Mjinga na Mbumbumbu!!!

Je, kwa sasa bado tunapaswa kulipa Capacity Charge?!

REMEMBER... kuna Mkataba wa Kuuziana Umeme na Leseni ya Kuuza Umeme! Hivyo ni vitu viwili tofauti!!! Jambo la kuhoji, Capacity Charge inatokana na nini? Inatokana na Mkataba wa Kununua Umeme au Leseni ya Kuuza Umeme?

Kwa maoni yangu, kwavile sifahamu mkataba upo vipi, Capacity Charge inatokana na Mkataba wa Kuuziana Umeme na sio Leseni ya Kuuza Umeme!!!

Capacity Charge inatokana na Mkataba wa Kununua Umeme kwa sababu, kama mkataba ungekuwa ni kuuziana umeme bila conditional ya mahitaji, yaani kuuziana continuously, basi Capacity Charge kuna uwezekano isingekuwapo! As we speak, Mkataba wa Kununua Umeme unaisha mwaka 2022.

So, unless Mkataba wa Kununua Umeme unavunjwa mapema iwezekanavyo, kuna hatari tutaendelea kulipa Capacity Charge hata kama kupitia mahakamani!!! Au, tutaendelea kulipa CC hadi pale mkataba utaakapovunjwa rasmi kama kuna hiyo room ya kuvunja!!!!

Hapo juu tena, kwa mujibu wa Tanzania yangu, nina sifa ya kuitwa sio Mzalendo kwa sababu wanadhani Uzalendo ni kuwa Mjinga au kufumbia macho FACTS!

REMEMBER, Haki na Sheria ni mambo mawili tofauti!!!!
Rejea hiyo barua ya mwaka 2004, hiyo barua inaonyesha kwamba endapo IPTL itashindwa kuzalisha umeme pale watakapohitajika, kwa sababu zozote zile, iwe ubovu wa mitambo au ukosefu wa vibali, basi Tanesco ina haki ya kimkataba kuvunja mkataba huo.
 
Attachments

  • IPTL Phase 1.zip
    852.9 KB · Views: 32
Mgawo mkali unakuwaje na usiokuwa mkali unakuwaje?
Kipindi cha Mkwere kulikuwa na mgao wa masaa 12 kila siku kwa mwaka mzima, hasa ktk mkoa wa Arusha. Huo ndo mgao mkali kwangu mimi. Mgao wa masaa 1-3 naweza kusema tumeshauzoea, ni kawaida.
 
Rejea hiyo barua ya mwaka 2004, hiyo barua inaonyesha kwamba endapo IPTL itashindwa kuzalisha umeme pale watakapohitajika, kwa sababu zozote zile, iwe ubovu wa mitambo au ukosefu wa vibali, basi Tanesco ina haki ya kimkataba kuvunja mkataba huo.
Sasa hayo maelezo yana uhusiano gani na nilichoandika?!
 
For 23 years wamekua wakila monthly pension ya billion 6 bila kufanya kazi yeyote ile.., bure kabisa
Sasa kama mliwapa wa kumkataba wa kununua umeme pale tu mnapohitaji ulitarajia nini?! Ingekuwa wewe ungekubali uwekeze mitambo lakini kuuza umeme ni hadi watakapotaka wao?!

Narudia, hata kama ingekuwa ni wakati wa Nyerere, so long as mkataba ulikuwa ni kununua umeme pale tu kunapokuwa na mahitaji basi katika mazingira kama hayo capacity charge ni LAZIMA!!! Kwahiyo hawakuwa wanakula pesa za bure... nature ya mkataba ndiyo iliyowapa haki ya capacity charge! Na suala la capacity charge lipo dunia mzima!!!
 
As usual Mkuu Chige at your own best! Asante kwa darasa! Je haiwezekani kukubaliana viwango wa tofauti vya capacity charge kulingana na mahitaji yetu ya nishati?

Sent using Jamii Forums mobile app
Of course, negotiation ni LAZIMA kwa watu wanaoweka mbele maslahi mapana ya taifa! Kwa mfano, Investor ata-propose capacity charge lakini upande wa serikali nao watatakiwa kwenda mezani na maximum proposed capacity charge kwamba, above that, no business!!!!

But all in all, isn't about huyu anakuja na propose hii na yule anakuja na hii bila kuonesha kwanini umefikia hiyo proposed amount. Kwa upande wa mwekezaji, obvious estimation zake zita-base kwenye cost of wear and tear.

Hii mitambo inaponunuliwa tayari inakuwa na depreciation value kwa kila mwaka! Which means, assume depreciation value kwa mwaka ni $100, na expected sales ya umeme kwa mwaka (kutokana na mkataba wenu) ni $30, hapo mwekezaji lazima ata-demand capacity charge ya $70 ili ku-offset hiyo annual depreciation cost.

Na isipokuwa hivyo, so who's to bear that cost?!

REMEMBER, hayo hapo juu yatatokana kwenye mazingira ya win-win situation lakini kama hutaki kujifanya mzalendo fake unatakiwa kukubali kwa nature ya mkataba wa IPTL, capacity charge ilikuwa haikwepeki!!!

Na hata sisi raia hizi capacity charge tunalipa sana!!! DAWASCO wakija kukufungia tu ile mita yao ya maji... maji utumie au usitumie; lazima ulipe capacity charge in the name of service charge!!!! TANESCO nadhani ni Muhongo ndie aliitoa hiyo service charge!!!

Ukiwa na account bank hata usipoenda kutumia zile stationeries zao kwa mwaka mzima, bado maintenance fee lazima wakuchape and they're right!!! Wamenunua yale madubwasha ili wateja wayatumie... kwahiyo hata usipoyatumia, wao haiwahusu lazima uyalipie kwa sababu tayari wameshaingia gharama!!!

FACT From Business Point of View against FAKE Nationalism Point of View
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom