Mitaala ya somo la Historia iliyositishwa ilijaa propaganda za kumsifu Magufuli kuwa ni kinara wa mabadiliko nchini

Status
Not open for further replies.
Sawa hakuna shida.
Acha tuendelee na historia hii hii ya kuwadanganya watoto wetu kuwa tuligunduliwa nawazungu. Huku tukiwasifu kina Carl peters na Vasco da gama.
 
Katiba zinajengwa na kulindwa na watu.

Usitegemee katiba ndio itaandamana badala yako pale haki zako zitakapokiukwa.

Kama watu hawajawa tayari kwa hilo hakuna namna ya kulifanya.

Siku watu wakihitaji katiba mpya, itapatikana ndani ya muda mfupi tu. Sasa hivi wananchi wa kawaida bado wanaona katiba mpya hakuna namna itawasaidia kuwaletea tonge mezani.
Ni kwa sababu wengi hawaelewi mantiki ya katiba inaamzia kwenye familia ambapo baba ni kila kitu hakuna mpango au makubaliano au mwongozo maalumu.
Ndo maana wengi humwangalia rais kama bab/mama.
 
Angalia kariakoo ilivyoungua magari ya zimamoto yakawa yanapata shida kupita. Aliwaruhusu machinga kujazana kule kwa sifa tu. Hili kundi lilipandikizwa imani mpya juu ya huyu mtu wangeweza hata kumsahau Mungu.
Wako wanaotaka lijengwe lisanamu lake sijui watakuwa wanaenda kusujudu pale!

kkoo imeungua usiku nungu nungu,uliishawahi kufika kkoo???
 
Bila hata kuona kitabu, namna amri ya kuanzishwa hili somo ilivyotolewa inaonyesha utaalam haukuzingatiwa. Mitaala ya masomo haianzishwi na kutayarishwa kwa gahafla namna hiyo. Inatakiwa kwanza ifanyike research na wataalam wa kuandaa mitaala wapewe muda ili kuandaa. Tulikuwa na rais kichaa.
Ulikuwa ujinga. Kwa muda mfupi unawekaje content katika levels mbalimbali. Wanaelimu wanaelewa..
 
My take, huyu mzee alikuwa amejipanga kubrainwash watu ili apewe muhula mrefu wa kutawala nchi
Meko alikuwa ni shetani kabisa yule mzee.
Aliiharibu sana nchi, afadhali Mwenyezi Mungu alimchukua mapema maana kama angekuwepo tu mpaka leo sijui tungekuwaa wapi, tulikuwa tunaelekea kuwa kama Cuba au Korea Kaskazini kabisa.
Kujiongezea kinga ya kutoshtakiwa yeye na wahuni wenzake, kujilimbikizia matrillion ya fedha za umma, kujambazi fedha za wafanyabiashara, kujiandalia somo la kumsifia mashuleni, yani huyu mzee kama kuna uwezekano akafufuliwe auawe kwa aibu kwa mara ya pili
 
VITABU vipya vya “Historia ya Tanzania” vilivyokuwa vimechapwa kwa agizo la Rais John Magufuli havitatumika tena. Badala yake, vitaandaliwa vingine – endapo kutakuwa na umuhimu huo, SAUTI KUBWA imeelezwa.

Somo hilo lilipangwa lifundishwe kwa wanafunzi wa shule za awali hadi sekondari za juu kuanzia Julai Mosi mwaka huu. Kwa taarifa zilizopo, sasa itabidi somo hilo lisubiri au halitakuwepo kabisa kutokana na udhaifu uliogundulika.

Taarifa ambazo zimeifikia SAUTI KUBWA zinaeleza kwamba kusitishwa kwa somo hilo kunatokana na kile kinachoelezwa kuwa ni mkanganyiko wa “usahihi wa historia” iliyokuwa imelengwa na imechapishwa kwenye vitabu hivyo vya kiada.

Sehemu kubwa ya historia hiyo ilikuwa imeandikwa kama propaganda za kusifu watawala na kubeba taarifa nyingine zisizokuwa sahihi, hasa katika kuelezea mwenendo wa kuimarika kwa uchumi na maendeleo ya siasa nchini Tanzania.

Chanzo chetu kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) kimeiambia SAUTI KUBWA: “Sehemu kubwa ya vitabu vilivyochapishwa imebeba historia potofu; inasifia mmoja wa marais wa Tanzania kuwa ndiye kinara wa mabadiliko ya maendeleo yanayoonekana sasa, hatua ambayo haina usahihi.” TEA ndiyo waandaaji wa mitaala ya elimu nchini Tanzania.

Alisema vitabu hivyo vilisheheni sifa kwa Rais Magufuli, huku viongozi wengine waliomtangulia wakitajwa kwa mbali kama sehemu ndogo au “wakibebeshwa lawama” kwa baadhi ya madhila yaliyoonekaa kushamiri Tanzania.

Miezi michache kabla ya kifo chake, Rais Magufuli ndiye alitamka hadharani, na kaagiza waziri wa elimu, kwamba kuna ulazima wa kubadili mitaala na kuandika upya vitabu vya somo la Historia na kwamba lianze kufundishwa haraka tangu madarasa ya awali. Magufuli aliaga dunia Machi 17, 2021.

Ofisa mwandamizi wa TEA ambaye hakupenda kutajwa jina lake alisema kuwa uamuzi wa kusitisha vitabu hivyo umefikiwa baada ya serikali kubaini kwamba somo hilo litakuwa limejaa hadaa za kisiasa, jambo ambalo ni upotoshaji wa historia halisi ya Tanzania.

Rais Magufuli alitaka somo hilo liwe maalumu, akidai kwamba Watanzania wengi hawajui historia ya nchi yao. Hata hivyo, historia ya Tanzania, miaka nenda rudi, imekuwa ikifundishwa shuleni katika somo la historia na kama sehemu ya somo la Uraia.

Kauli ya Rais Magufuli ilitolewa Desemba 9 mwaka jana wakati akiapisha mawaziri wapya Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma, akamwagiza Prof. Joyce Ndalichako kuhakikisha somo la Historia ya Tanzania linaanza kufundishwa upya na haraka – na kwamba liwe ni somo la lazima kwa kila mwanafunzi.

Februari 12, 2021 Prof. Ndalichako alisema wizara hiyo ilikuwa imeanza utekelezaji wa maagizo ya Rais Magufuli mara moja kwa kuandaa muhtasari ambao ungewezesha somo hilo kuanza kufundishwa kutoka madarasa ya chini hadi kidato cha sita.

Alisema kwamba somo hilo lingesaidia “kujenga moyo wa uzalendo” kwa kuwafanya Watanzania kuifahamu nchi yao, kuithamini na kuipenda na kujenga moyo wa kulinda rasilimali; akasema maandalizi – ikiwa ni pamoja na kuandika vitabu hivyo – yalikuwa yanaendelea vema.

SAUTI KUBWA inazo taarifa kuwa kazi ya kuandaa na hatimaye kuchapishwa vitabu vya somo hilo ilikamilika mwezi Aprili, 2021 na zilikuwa zikisubiriwa fedha za kuanza kuvisambaza shuleni.

Wadau wengi wa elimu walilaumu serikali kwa kuanzisha somo hilo kana kwamba ni jipya huku wanafunzi wamekuwa wakilisoma miaka yote kuanzia madarasa ya chini.

Akitoa maoni yake, mhadhiri mstaafu wa vyuo vikuu, Dk. Lenny Kasoga, amesema kuwepo kwa “somo la Historia linalojitegemea” ni mzigo mwingine kwa serikali na matumizi mabaya ya raslimali fedha.

“Wanafunzi wamekuwa wakisoma historia ya nchi yetu. Sasa kuwaongezea somo jingine ni kuwapa shida watoto wetu. Kwanza tayari wana masomo mengi sana,” aliongeza msomi huyo wa siasa ya uchumi.

Akiwa mjini Morogoro Februari 12, 2021, Rais Magufuli alikumbusha tena umuhimu wa somo hilo na kutishia kumfukuza kazi Prof. Ndalichako kwa kuendelea kuchelewa kulianzisha.

Juni 26, 2021, Prof. Ndalichako alitangaza kusitishwa kwa mchakato wa kuanza kufundishwa Historia ya Tanzania, akiueleza umma kwamba kuna “mambo yanaboreshwa kwanza.”

Wachambuzi wa siasa na wanazuoni walitoa maoni na kutoona mantiki ya kuanzishwa kwa somo jipya, na sasa wanabashiri kwamba huenda somo hilo halitakuwepo tena kwa kuwa si kipaumbele cha Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alirithi madaraka kutoka kwa Magufuli.

Mwalimu Phoebe Makelemo, ambaye sasa ni mshauri wa masuala ya elimu katika balozi kadhaa nchini ni mmoja wa wataalamu wa elimu ambaye alipinga kuanzishwa kwa somo hilo, alihoji umuhimu wa somo hilo sasa na uharaka wake huku akitahadharisha kupotoshwa au kuandaliwa kwa mtaala ambao hauna vigezo ili tu kukidhi matakwa ya rais.

Mwalimu huyo alisema katika kuandaa mitaala yapo mambo ya msingi kuzingatia, na kwamba ana shaka endapo yalifuatwa.

Mambo hayo ni pamoja na kufanya maandalizi ya ufundishaji ni kuchambua muhtasari wa somo na vitabu vya kiada kwa somo husika ili kubaini mada kuu na mada ndogo zilizopo na kuzipangilia kimantiki kufuatana na mazingira ya ufundishaji unaoukusudia, uandaaji wa azimio la kazi, uandaaji wa somo na zana pamoja na mbinu za kufundishia.

“Shaka ni kwamba mambo haya hayakuzingatiwa kwa kuwa kulikuwa tu na msukumo wa rais, na kwamba muda haukuweza kutosha kuwa na mitaala yenye maana pana na kubeba dhana iliyokusudiwa,” alisema na kuongeza: “Hawa walichofanya ni kazi ya zima moto.”

Source: Sauti Kubwa
Mataga vitabu vipo vichukueni mkafundishie watoto wenu..

Ila watoto wa maskini wanalishwa kila uchafu wa kila dekio
 
kkoo imeungua usiku nungu nungu,uliishawahi kufika kkoo???
Umefurahi kutamka nungunungu unajuaje kama niko kariakoo. Usiku ndo nini vibanda vimelizunguka soko. Na je, kariako watu wanakaa hadi saa ngapi? Tukana, jitukane
 
Ndalichako bado ni waziri.

Serikali yote ni batili
 
Unataka kumuelewa Mungu utaweza? Mungu huyo huyo kamchukua Magufuli ila kamuacha Ibilisi hadi leo.
Tusipangiane kuhusu kumuelewa Mungu, we muelewe hivyo na mimi nimemuelewa nilivyo elewa, mi najua Mungu nae ni mwana demokrasia, hakulazimishi kuchagua UPANDE kaka.
 
Nani kakwambia Mungu ni mwanademokrasia? Mungu anaamua kufanya lolote alitakalo pasina kupangiwa wala kumhofia yeyote, wewe ushawahi kusikia Mungu kutaka hata ushauri wa mawazo kwa kiumbe yeyote?

Au wewe kabla ya Mungu kukuumba alikushirikisha akuumbaje? huyo Mungu unayemuelewa wewe na mwenyedemokrasia sijui ni Mungu gani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom