Kwa tathmini ya haraka haraka mpaka sasa mikoa yenye watumiaji wengi wa JF ni Dar, mwanza , arusha, na mbeya,
Mikoa mingine bado inajikongoja kabisa tena kwa kuchechemea. Thibitisha hilo kwa kufatilia jinsi wachangiaji wanavyoitaja mitaa au vitongoji vya maeneo ya mikoa hiyo.
Tajeni koooote ila Ungalimited Arusha ni habari nyingine.....sijui siku hizi ......kuna chochoro ukipita hadi nywele zinasimama aina ya watu unaopishana nao ..........chochoro za ajabu utafikiri jehanam ..........wezi wa ungalimitedi ni wazawa wa pale ........wanafanya chochote bila woga kabisaaaaa.................
Inawezekana lakini mimi naona Arusha ni kiboko ya mikoa yote kwa uhuni wa mitaani na kuuana kwa visu, silaha, vibaka n.k. Ni mkoa ambao binafsi siupendi sababu wahuni ni wengi mno. Wala mirungi na bhangi
Siamini unachokisema wakati kuna jamaa yangu kaibiwa bodaboda wiki ya pili na hao askari kanzu hawakuonekana. Alipata mteja tokea Mwenge hadi Obey. Mteja kashuka ile kutoa wallet mfukoni wakati huohuo anaongea na simu kama dk 3 imekuja gari ndogo zile za mizigo wametoka wajomba wawili mmoja kashika bunduki mwingine ana panga. Jamaa kapigwa kitako cha bunduki na kuwekwa chini ya ulinzi. Wakabeba pikipiki na kuweka kwenye gari kisha wakatokomea. Jamaa kapiga kelele zote wala hakupata msaada, hatimaye mlinzi mmoja ndo anatoka ndani ya geiti na kumkuta jamaa kafungwa kamba pale kwa nje. Mlinzi akamfungua na kumwambia maeneo yale majambazi wanawaletaga bodaboda na kuwaibia pikipiki zao wala asijisumbue, aende nyumbani kwake akalale.... unajua ilikua saa ngapi hiyo??? Saa saba mchana kweupe... si unajua tena obey hata mchana utafikiri hawaishi watu. Sasa hao askari kanzu wanakuwaga wapi mpaka hiyo barabara ikose usalama???