Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 784
- 1,066
Baada ya kufanyika kwa mafanikio makubwa jijini Dar es Salaam, sherehe za maadimisho ya miaka miwili ya programu maalumu ya Darling Hair maarufu kama ‘Loyalty Program’ sasa zinahamia mikoani ili kuwafikia wasusi wengi zaidi.
Tayari wasusi zaidi ya elfu sita wameshafikiwa kufuatia hafla zilizofanyika katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam ambapo wasusi walijumuika pamoja na uongozi wa juu wa kampuni hiyo katika maadhimisho hayo ya miaka miwili.
Akizungumza maeneo ya Mbagala Zakiem ambapo takriban wasusi elfu moja walikusanyika, Meneja Saluni wa Darling Hair, Joyce Mwijage alisema hadi sasa program hiyo imekuwa na mafanikio makubwa na mwitikio wa wasusi umekuwa ni mkubwa.
“Haya ni maadhimisho ya mwaka wa pili wa program yetu hii ambayo inawalenga wasusi wadogo wadogo waweze kupata mitaji ya kufanya shughuli zao za ususi kwa ufanisi zaidi. Katika programu hii wanakusanya lebo za bidhaa zetu mbalimbali na kujikusanyia pointi ambazo zinawawezesha kushinda vifaa mbalimbali vya saluni kulingana na pointi husika,” alifafanua.
Aliendelea kusema walianza na wasusi takriban elfu tano mwaka wa kwanza na kwa mwaka huu wameshawasajili wasusi zaidi ya elfu kumi huku lengo likiwa ni kufikia wasusi elfu ishirini ifikapo mwakani.
“Baada ya kuhitimisha maadhimisho haya kwa Mkoa wa Dar se Salaam ambapo muitikio umekuwa mkubwa mno, sasa tunabisha hodi mikoani na baadhi ya mikoa ambayo tutapita ni pamoja na Arusha, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Morogoro,” alisema huku akitoa wito kwa wasusi wa mikoani wajitokeze kwa wingi.
Aliongeza kuwa katika sherehe hizo za maadhimisho ya miaka miwili, wasusi wa Dar es Salaam walipata fursa ya kushinda zawadi, kucheza mziki, mashindano mbalimbali, kupata mafunzo kutoka Darling na kufahamu bidhaa mpya za kampuni hiyo na matumizi yake.
Geogffrey Ahadi ambaye ni Msusi kutoka Kongowe aliishukuru Darling Hair kwa kuwaongezea uwezo wasusi nchini kwa kuwapa mitaji kwa kupitia zawadi wanazoshinda. “Pamoja na kula na kunywa kwa kweli tumenufaika sana kutokana na vifaa ambavyo tunashinda katika program hii ya Loyalty. Kwa ambao hamjajiunga mmechelewa sana milango iko wazi njooni tufaidi sote,” alisema.
Naye Latifa Athumani ambaye pia ni msusi kutoka Kizuiani, alisema anajivunia kuwa sehemu ya familia ya Darling kwani program hii ya Loyalty imekuwa na faida kubwa kwake na kwa wasusi wengine. “Kitendo tu cha kutukusanya pamoja na kutuweka sehemu moja ni jambo kubwa sana ambalo wengine hawafanyi tunaomba programu hili iwe endelevu ili tuendelee kukua,” ali
sisitiza.
Mariamu Joash kutoka Ferry Kigamboni alisema programu ya Loyalty imewasaidia wasusi kutoingia gharama za vifaa vya saluni hasa viti kwani karibu kila msusi sasa ana kiti cha Darling Hair. “Kama tunavyofahamu viti vinatumika sana katika saluni yoyote ile kwa hivyo ujio wa program hii umesaidi wasusi wengi kupata viti kwa urahisi na kuhudumia wateja kwa ubora zaidi,” aliongeza.
Alitoa wito kwa wasusi waendelee kutumia program hiyo kujitanua zaidi kwani ni mpango wa kudumu wa kampuni hiyo.