Misri yamwachia mwandishi wa habari wa Al Jazeera baada ya miaka minne

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Baada ya kukaa kizuizini kwa zaidi ya miaka minne, mwandishi wa habari wa Al Jazeera, Mahmoud Hussein ameachiwa siku ya Ijumaa.

Hussein, raia wa Misri, alikamatwa mwezi Disemba mwaka 2016 kwa tuhuma za kuandika habari za uwongo. Shirika la Habari la Al Jazeera lilifanya kampeni kila siku kutaka kuachiwa kwake, likidai kuwa mfanyakazi wake alishikiliwa kinyume cha sheria bila kufunguliwa mashtaka.

Shirika hilo halijatoa taarifa kuthibitishwa kuachiwa kwake, lakini ripoti ya Shirika la Habari la AFP imesema kuwa taarifa ya mwandishi huyo kuachiwa imethibitishwa na Mtandao wa Kiarabu wa Taarifa za Haki za Binadamu, ikiongeza kuwa mwandishi huyo hajarejea nyumbani.

Shirika la habari la Al Jazeera lilijikuta katikati ya mzozo wa kisiasa kati ya Cairo na Doha baada ya kuondolewa madarakani kwa Rais wa zamani na kiongozi wa vuguvugu la Udugu wa Kiislamu anayeungwa mkono na Qatar, Mohammed Morsi, huku tovuti ya Al Jazeera ikizuiwa nchini Misri tangu mwaka 2017.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameulaumu utawala wa Rais Abdel Fattah al-Sisi kwa ukandamizaji wa haki za binadamu, ukijihusisha na kuwakamata maelfu ya wafuasi wa Morsi, wakiwamo waandishi wa habari, wanasiasa na wanamuziki.
 
Tatizo moja kubwa la third world ni kutothaminiana sisi kwa sisi.

Egypt wana bifu na Al Jazeera, wakaogopa kumkamata mtu wa Al Jazeera foreigner, wakamkwida mwandishi raia wao wenyewe.

Formula hii hii ndio ilitumika bifu la Tanzania, The Economist na Kabendera.
 
Kuna kutofahamiana kati ya Qatar na UAE but pia Misri anawafata UAE sera zake ila sasaivi ndio wamepatana kidogo kidiplomasia ndio maana nahisi kaachiwa huyo muandishi
 
Tatizo moja kubwa la third world ni kutothaminiana sisi kwa sisi.

Egypt wana bifu na Al Jazeera, wakaogopa kumkamata mu Al Jazeera foreigner wakamkwida mwandishi raia wao wenyewe.

Formula hii ndio ilitumika bifu la Tanzania, The Economist na Kabendera.
Mkuu upo vizuri
 
Mkuu, Peter Greste mwandishi wa Al Jazeera raia wa Australia alikamatwa mwaka 2013 na kukaa kizuizini kwa zaidi ya siku 400 kabla ya kuachiwa
 
Duh nadhani ni baada ya Amnesty International kupitisha azimio juzi la kuwasaidia wanahabari na wanasheria wanaoteswa/kushikiliwa na serikali kandamizi.

Huwa nilikuwa kila nikiw naangalia Al Jazeera naona lazima hiyo headline ipite chini pale

"Aljazeera journalist Mahmoud Hussein jailed in Egypt without trial for 1400+ days".
 
Ila Al Jazeera na wao wamezidi kuna habari za uongo walitangaza last year kuhusu Misri mpk nikashangaa yaani isingekuwa niko Cairo hiyo time ningeamini hiyo news. Baada ya kuona wako biased kwa news zao ndio nilielewa kwa nini Sisi anawafunga. Wawe wana report ukweli sio kumchukia mtu kisa anaelewana na wazungu
 
Mkuu, Peter Greste mwandishi wa Al Jazeera raia wa Australia alikamatwa mwaka 2013 na kukaa kizuizini kwa zaidi ya siku 400 kabla ya kuachiwa
Okay, walijitutumua kumkamata mu Australia. Wakamfungulia mwaka mmoja baadae.

Mwenzao mu Egypt wamempa mvua nne!

Yani mu Afrika huna thamani mbele ya serikali yako, mbele ya raia wenzako.

Historia inasema zama, enzi na dahili ndivyo tulivyo, tulikuwa tunawauza wenzetu wakatupwe baharini wakielekea utumwani kwa Waarabu na Waamerika.
 
Ww unailaumu serikali kwa kumkamata ila waandishi wa habari was ndani huwa ndo silaha ya wenye chuki na taifa lenu mfano kipindi Cha uchaguzi 2015 chombo Fulani kikubwaaa dunian kilitangaza mwanza Jeshi la polisi limeua watu kadhaa ktk kuzuia maandamano wkt in reality kitu km hcho hakikuwepo , na mwandishi wa habari ni mzawa kbsa analipwa ili kuvuluga usalama was taifa lake , akishikwa nyinyi msioelewa chochote mnakuja kuilaumu serikali , jmn dunia ya leo mabeberu na mataifa mengine makubwa duniani yanatumia media km silaha zao ktk kuteteresha siasa na kuchochea fujo kwa nchi masikini mf China wanna TV zao hawana muda na BBC , aljazeera , cnn , VOA Wala France 24 na hvyohvyo kwa mataifa ya ulaya hayapi sikio kubwa channel km RT , Aljazeera , kwasababu wanaelewa athari ya hv vyombo coz vpo kueneza propaganda na si hbr km unavyoelewa ww
 
Back
Top Bottom