Misomisondo wana mwanasheria wa kuwasaidia kutengeneza mikataba yenye tija kwa kazi wanazofanyishwa na makampuni ya kibiashara?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
888
4,136
Tanzania imekuwa eneo moja wapo la matajiri kuwatumia maskini kunufaika kibiashara

Vijana kutoka kijijini na makoti yao wameingia mjini; joto ni kali lakini muda wote wamevaa makoti wanacheza barabarani na kwenye kumbi kutangaza biashara za watu.

Kwa fedha makampuni wanazoigiza kupitia vijana hawa nilitegemea kusikia wamesaini mikataba kwa kazi wanazofanya.

Naamini hawa vijana wanahitaji kujisimamia na kukomboa familia zao. Naona dalili za umaarufu wao ukishuka bila wao kunufaika na mateso wanayopitia.

Nimeona Vodacom wanawatumia, nimeona eFM wanawatumia na makampuni mengine kibao; Je, wanawalipa sawa na ukubwa na mchango wao kwenye kutangaza business?

Wanalipwa as group au ndio analipwa mmoja awagawie? Au yupo mtu kawasainisha mikakataba ya kibepari wasiyonufaika nayo?

Hawa watu wasipochangamka sasa watakuja kwenye vyombo vya habari kulia lia wametumika na kutupwa.

Wapate japo nyumba na usafiri iwe motisha kwa wabunifu wengine. Naamini wakipata mwanasheria mzuri wanaagana na umaskini wao na familia zao
 
Majizo ndie kawaleta mjini na kujipa umeneja

Mikataba na hayo makampuni kama vodacom anaingia majizo.

Misondo yeye na wenzake wanalipwa na majizo mgao kidogo
Huyu hajawahi kuwa na nia njema na Wasanii. Ni Mwizimwizi.
 
Back
Top Bottom