Waziri wa Kazi: Kwanini tusiandae mazingira ili makampuni ya simu yasiweke viwanda vyao nchini

Right3

Senior Member
Aug 16, 2015
193
233
Nimejaribu kuwaza gharama za uzalishaji Marekani na Ulaya ziko juu kutokana na vyama vya wafanyakazi kusimamia kisawasawa maslahi ya wafanyakazi na gharama za maisha za nchi hizo.

Makampuni mengi yakikimbilia uchina kwa kuwa kuna mazingira yanayoruhusi wao kwenda huko ikiwemo watu wenye ujuzi, umeme wa uhakika,mishahara midogo, usafirishaji wa bidhaa na malighafi nk.

Nikawaza hii nchi tuna maelfu ya vijana wasio na kazi ambalo ni bomu (mwanasiasa mmoja aliwahi kusema).

Kwa nini tusiainishe skills (ujuzi) unaohitajika na makampuni haya kwa kuzungumza nao na ikibidi hata kuomba kuwa na mikataba nao tukipeana muda hata wa miaka kumi au mitano tukachagua vyuo kadhaa vya VETA tukapeleka walimu wetu uchina kwenye plants za hawa jamaa hata Marekani ili wakapate ujuzi hitajika.

Km si hivyo tunaweza hata kuhire walimu kutoka nje tukaanzisha kozi za ujuzi hitajika ili tuandae wafanyakazi bora ili baadae tupate viwanda vya simu, computer na mambo mengine.

Soon
1. tutakua na umeme wa uhakika JNHPP itakuwa imeanza kuzalisha umeme.
2. Tunalidege la mizigo litapeleka bidhaa hizo popote duniani na bahari tunayo.
3. Tutaweka sera nzuri zitakazowafanya waone mazingira yetu ya uwekezaji ni wezeshi.
4. Tuna amani hivyo hakutakuwa na interruptions za uzalishaji.
5. Geographically tuko positioned vizuri kuliko Rwanda.
6. Tuko na watu walio tayari kupata ujuzi.

Nilitamani kuona mkienda mbele zaidi kwenye kukabiliana na tatizo la ajira na sio kufanya yale yaliozoeleka.
Yawezekana mna mipango ongezeni bidii mtaani kubaya vijana hawana pakushika pamoja na jitihada za BASHE na wengine bado hazitoshi tatizo ni kubwa.
 
Amini nakwambia siku ambayo utaona bongo movie wanatengeneza movies nzuri za kimataifa na kuacha mambo ya jambazi kuvua viatu basi ndipo na serikali itakuwa na mitazamo ya kimaendeleo.
 
Back
Top Bottom