Mishakaki ya Paka

Cha msingi nadhani ni je anawaambia wateja wake kuwa ni mishikaki ya paka kabla hawajanunua? Kama hilo lipo wazi kwa mteja na kwa utashi wao wananunua na kula then sion tatizo kwa muuzaji.

Nyama, nyama, nyama!....Nyama!
Ya paka?...
.........siyo nyama!!
 
nimemsikia hajaniconvince...
huyo anataka airtime tu.... eti namwita nyau nyau wanakuja kisha nawafunga mikono na miguu... nawakanyaga tumboni na kuwachinja... jamani paka ni jamii ya chui na simba... akisense hatari habari yake utaiona... huyo jamaa hana lolote, hao hawako serious

Hata kwa babu Loliondo mwanzoni ilikuwa hivyohivyo

:coffee:
KIKOMBE CHA UZIMA
 
Nakumbuka kuna jamaa flani kibaha alikuwa anauza mahindi.
kuna siku mbwa aligongwa na gari akafa, ghafla jioni yake yule bwana akabadili biashara badala ya kuuza mahindi akauza mishikaki.
Wananchi hawakumwelewa.
 
Hata kwa babu Loliondo mwanzoni ilikuwa hivyohivyo

:coffee:
KIKOMBE CHA UZIMA

huwezi kufananisha hivyo vitu viwili
yule ni mwongo kwa sababu aliulizwa familia yako inajua kwamba unafanya shuguli hizo ie unachinja na kupika mishkaki ya paka akasema ndio.. nasomesha watoto wanne shule kwa kazi hiyo

akaulizwa; je wewe na familia yako mnakula hiyo nyama... akazunguka mwisho akasema hapana, hata hawajui kwamba nafanya kazi hiyo....
why contradict yourself???

mtu wa wapi eti mpogolo ukimsikiklliza anaonekana mmakonde
 
nimemsikia hajaniconvince...
huyo anataka airtime tu.... eti namwita nyau nyau wanakuja kisha nawafunga mikono na miguu... nawakanyaga tumboni na kuwachinja... jamani paka ni jamii ya chui na simba... akisense hatari habari yake utaiona... huyo jamaa hana lolote, hao hawako serious

Kila kitu mnabisha ok, ya kwababu watu wanatoa shughuda mnabisha, ya nyau jamaa katoa shuhuda na bonge kamkuta mnabisha ! Haya kale mishkaki ya manzese
 
Siku hizi Wachina wengi sana Dar, angefanyia biashara yake maeneo ya Kariokoo ingelipa sana.
 
Mlio sikiliza power breakfast Leo najua Mmeipata vizuri.
Jamaa mburahati kauza mishkak ya paka for the last four years!
Amekiri kwa siku anauza paka wanne na kuendelea.
Hivi huyu jamaa hawezi chukuliwa hatua zozote za kisheria?
Jamni hii inasikitisha!!

Binafsi nina maswali zaidi kuliko majibu,hii kipengele cha kazi ni kazi lengo lake hasa ni nini?na Clouds wanapofikia kurusha kitu kama kile lengo ni nini?kuwajuza watu,kuwatahadharisha watu au?maana wanajua (kama kweli) basi anachofanya ni kosa;huwezi kuwalisha watu paka bila ya ridhaa yao.Sasa Clouds kama wanalijua hilo wamefanya nini baada ya kugundua hilo?
 
Cha msingi nadhani ni je anawaambia wateja wake kuwa ni mishikaki ya paka kabla hawajanunua? Kama hilo lipo wazi kwa mteja na kwa utashi wao wananunua na kula then sion tatizo kwa muuzaji.

Nyama, nyama, nyama!....Nyama!
Ya paka?...

si nyama
 
Mlio sikiliza power breakfast Leo najua Mmeipata vizuri.
Jamaa mburahati kauza mishkak ya paka for the last four years!
Amekiri kwa siku anauza paka wanne na kuendelea.
Hivi huyu jamaa hawezi chukuliwa hatua zozote za kisheria?
Jamni hii inasikitisha!!
Mimi nilishindwa kumuelewa kama walaji wanakifahamu wanachokula..
 
paka kama hajawadhuru watu,muuzaji hana hatia.hakuna sheria inayokataza kuuza nyama ya paka.aliyedhurika anaweza kudai fidia.muuzaji alikuwa anafanya biashara haramu lakini halali
 
huwezi kufananisha hivyo vitu viwili
yule ni mwongo kwa sababu aliulizwa familia yako inajua kwamba unafanya shuguli hizo ie unachinja na kupika mishkaki ya paka akasema ndio.. nasomesha watoto wanne shule kwa kazi hiyo

akaulizwa; je wewe na familia yako mnakula hiyo nyama... akazunguka mwisho akasema hapana, hata hawajui kwamba nafanya kazi hiyo....
why contradict yourself???

mtu wa wapi eti mpogolo ukimsikiklliza anaonekana mmakonde

Kaka hapo kwenye red nilikuwa siko-sure kama nilisikia hivyo na mimi,uko sahihi kabisa....jamaa ni muongo alijichanganya hapo na hiyo ni base ya kudanganya...swali sasa CLOUDS wanataka kutuambia nini??
 
Binafsi nina maswali zaidi kuliko majibu,hii kipengele cha kazi ni kazi lengo lake hasa ni nini?na Clouds wanapofikia kurusha kitu kama kile lengo ni nini?kuwajuza watu,kuwatahadharisha watu au?maana wanajua (kama kweli) basi anachofanya ni kosa;huwezi kuwalisha watu paka bila ya ridhaa yao.Sasa Clouds kama wanalijua hilo wamefanya nini baada ya kugundua hilo?

Swali lako la mwisho Limenivutia!!
 
anapata shilingi 20,000 to 25,000 per day ifikapo saa 3 mishikaki kwisha duuuuuuuuuuuuuu
 
sio mbaya sana, cha msing ni kwamba hakuna ambaye ameshawahi kula nyama ya nyau na akapata matatizo ya kiafya, mshkaj aendelee kupeta tu kwa kujiingizia kipato.
 
Huyo jamaa kweli mjasiliamali, haangalii hata athali kwa raia wengine!
...Lakini kwa nyie mliosikiliza maelezo ya huyo jamaa kuna madhara yoyote waliopata wateja wake?? Kama hakuna sioni tatizo na may be huo ukawa uvumbuzi mpya wa kitoweo na hasa kipindi hiki cha ukata mkali nyama za ng'ombe kwenye mabucha bei juu na pia itapunguza hata paka wanaozagaa hovyo kama pale Rose garden kuna paka wakiona unakula wanakugusa kama binadam kuomba msosi....:lol:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom