Mishahara ya SUMATRA kufuru

Mishahara ya SUMATRA kufuru

cape town

Member
Joined
May 28, 2013
Posts
40
Reaction score
42
Wakuu, hii mamlaka ya serikali inayoendeshwa kwa kodi za wavuja jasho ina unyeti sana kiasi cha watumishi wake kuenjoy pepo duniani?

Cjajua Taasisi zingine kama TRA mishahara yao ikoje ila nimeijua mishahara ya SUMATRA hadi nimeshangaa. Huenda sijafahamu unyeti wa mamlaka hii ila wanaoijua watatueleza.

Rafiki yangu amemaliza pale IFM akichukua Accouting, amepata ajira mwanzoni mwa mwaka huu katka mamlaka ya SUMATRA na kwa macho yangu amenionyesha Salary Slip yake daah, ni Milioni 1.53 kwa mwezi.

Wakuu hii mishahara inapangwa na ofisi ya utumishi au wanajipangia wafanyakazi wenyewe wa Mamlaka?
 
Unashangaa nini sasa hapo? Huo si mshahara bali masikhara tu. Uliza watu huko kwingine wanaanzia kiasi gani? Sasa unataka ashushiwe mshahara wake? Badala ya kuomba na kumshinikiza mwajiri wako nawe uongezewe unaanza kuwangalia wenzio kwa kijicho na husda. Kwanza ujue katika nchi hii miongoni mwa watu ambao wanalipwa maskhara ni pamoja na hao wanaoitwa wahasibu.


 
Millioni 1.35 ni mshahara wa kufuru? Kweli tunatofautiana.watu wanalipwa dola 25000 ambayo ni kama millioni 40 kwa mwezi endelea kulalamika na vyeti vyako

Huenda hata vyeti hana. Kama naona ananyonywa si akatafute kazi kwingine. Kuna Kilimo kwanza na Gesi vinalipa vizuri.

 
Mbona ni mishahara ya kawaida sana hiyo au wewe ulifikiri ni mikubwa ?
 
Hahahahaaaa...bila shaka atakuwa ana njaa iliyopitiliza..huwez kushangaa kamshahara hako na kuja na uzi kabisaaaa
 
wakuu,

Hii mamlaka ya serikali inayoendeshwa kwa kodi za wavuja jasho ina unyeti sana kiasi cha watumishi wake kuenjoy pepo duniani? Sijajua Taasisi zingine kama TRA mishahara yao ikoje ila nimeijua mishahara ya SUMATRA hadi nimeshangaa.

Huenda sijafahamu unyeti wa mamlaka hii ila wanaoijua watatueleza. Rafiki yangu amemaliza pale IFM akichukua Accouting, amepata ajira mwanzoni mwa mwaka huu katka mamlaka ya SUMATRA na kwa macho yangu amenionyesha Salary Slip yake daah, ni Milioni 1.35 kwa mwezi.

Wakuu hii mishahara inapangwa na ofisi ya utumishi au wanajipangia wafanyakazi wenyewe wa Mamlaka?

Mbona mshahara mdogo sana huo.

Kuna watu nchi hii wanapokea milioni 40 kwa mwezi wameajiriwa.
 
Hahahahaaaa...bila shaka atakuwa ana njaa iliyopitiliza..huwez kushangaa kamshahara hako na kuja na uzi kabisaaaa
anathani aonea mada hii, lakini anashindwa tu, tatizo la kuwa na msimamo wa kulaumu kila jambo.
 
Mbona mshahara mdogo sana huo.

Kuna watu nchi hii wanapokea milioni 40 kwa mwezi wameajiriwa.

Huyu bwana siyo kosa lake, walishakubaliana katika vikao vyao kuwa lolote linalofanywa na Serikali wanapaswa kulaani. Sasa wenzake wanapochanganya akili zao na zile za kuambiwa yeye anatoka mzima mzima, teh teh teh.
 
Mimi napata 6m kwa mwezi wewe unasema 1m?

Mleta mada amekariri kuwa humu kila kitu ni kupingana na Serikali. AIBU iliyoje hii jamani ndo ma-great Thinkers tunaojivunia humu. Mimi nimekariri ID yake hii ili nianze kufuatilia michango yake kwa kwaribu labda nitajiridhisha kama anastahili kuendelea kuwemo humu au tumhamishie gumzo la jiji.
 
Back
Top Bottom