Mishahara UDSM 'utata' mtupu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mishahara UDSM 'utata' mtupu...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by VUTA-NKUVUTE, Oct 5, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Kwanza wafanyakazi wa UDSM wameanza kupokea mishahara ya mwezi uliopita tangu jana tarehe 4/10/2012 saa sita mchana. Wameanza wafanyakazi wenye akaunti katika benki ya Makabwela yaani 'National Microfinance Bank-NMB'.

  Katika mishahara hiyo, wapo watumishi waliopata ongezeko la mishahara. Wapo pia pia wasiopata ongezeko.Hawa wamepata mshahara wao wa kawaida kabla ya ongezeko. Vilevile wapo walioshushwa mishahara.

  Hakuna sababu zilizotolewa na Serikali wala Chuo. Nyaraka za mishahara zinaonesha hivyo. Taarifa zinaonesha kuwa Utawala wa UDSM umeziba pengo la walishushwa mshahara ili kuzuia mgomo wa wafanyakazi wa aina hiyo.

  Hali ni tete. Lolote laweza kutokea pale...
   
 2. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hakuna chochote kitakachotokea maadam watu disign ya akina Dr bana,palamagambb etc ndo wapo pale
   
 3. Ufunuo

  Ufunuo JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  segwanga pokea like yangu manual natumia simu sioni kitufe cha like.
   
 4. s

  slufay JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,372
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Jaribuni kuchezea serikali; mulizeni Ulimboka yuko wapi? kama hamtaki kazi waache tu, kwanza wasomi hawa faida kazi yao kuzalisha mafisadi; angalieni Richmond mikataba feki yote huwezi kukosa msanii toka Udsm
   
 5. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Unataka kupendekeza kwamba shule na vyuo vifutwe? Naomba uthibitishe namna vyuo vikuu vinavyoshiriki kuzalisha mafisadi na ueleze wananchi wanaopambana na ufisadi wamesoma wapi.
   
 6. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wamejiweka kuwa mateka wa serikali ya CCM huwezi kuwa na mwendawazimu kama Dr.Bana au mapunga wengine wanasifia serikali ya majambazi ya CCM.Walifurahia CCM walivomnyima mkataba prof.wa tume ya katiba kwakuwa yupo chadema leo wanalialia nini watulie tu waendelee kuburuzwa na vilaza wajumbe wa nyumba kumikumi wa CCM,maprof na madr. utadhani hawakusoma kabisa kupigia magoti majambazi ya CCM.UDSM potelea kuzimu
   
 7. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kaazi kweli kweli!
   
 8. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  U r very right!
   
 9. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hakuna kugoma ni kufanya kazi lazima walinywe maana ndio amadili ya kazi
   
 10. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Wadau,
  Hili bandiko hapa chini nimetumiwa na jamaa yangu wa UDSM kuhusu yanayoendelea. Inaelekea mtoa mada amechungulia hapa JF kabla ya kwenda kutoa ya moyoni. Soma mwenyewe.

  Wana UDASA

  Nimeikuta hii kwenye moja ya mitandao ya kijamii
  Mishahara UDSM 'utata' mtupu...
  "Kwanza wafanyakazi wa UDSM wameanza kupokea mishahara ya mwezi
  uliopita tangu jana tarehe 4/10/2012 saa sita mchana. Wameanza
  wafanyakazi wenye akaunti katika benki ya Makabwela yaani 'National
  Microfinance Bank-NMB'.


  >Katika mishahara hiyo, wapo watumishi waliopata ongezeko la mishahara.
  Wapo pia pia wasiopata ongezeko.Hawa wamepata mshahara wao wa kawaida
  kabla ya ongezeko. Vilevile wapo walioshushwa mishahara.


  >Hakuna sababu zilizotolewa na Serikali wala Chuo. Nyaraka za mishahara
  zinaonesha hivyo. Taarifa zinaonesha kuwa Utawala wa UDSM umeziba pengo
  la walishushwa mshahara ili kuzuia mgomo wa wafanyakazi wa aina hiyo.
  >
  >Hali ni tete. Lolote laweza kutokea pale..."
  >
  >
  >Nianze kwa kueleza kuwa nimesikitishwa sana kusikia mmoja wa wanachama wa Udasaametishwa kutokana na yale aliyoyatolea maoni kwenye "forum" hii hii. Ifike wakatikoleo tuliite koleo> Mimi binafsi dini ninayoamini inaniambia kuwa "Iseme kweli nahiyo kweli itakuweka huru". Yanayotokea CKD kwa sasa hasa kuhusu mishahara yawafanyakazi inaonesha kuwepo kwa ombwe la uongozi. Nimefanya utafiti kuyasema hayanitakayoyasema hapa chini. Yaani matatizo yaliyopo CKD ni matatizo ya miaka nendarudi ambayo yamekuwa yakiikabili Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,mpakanajiuliza kunani CKD?


  >Nimepata kuongea na mtu wa karibu ambaye yupo ofisi ya mishahara, ameniambia,kwakuwa yeye amekuwepo hapo muda mrefu, matatizo wanayokumbana nayo wafanyakazi kwenyemishahara yao sasa hayakuwapo enzi za Prof. Mathew Luhanga (akiwa VC) na mtanguliziwake. Tena ameendelea kueleza kuwa ilifikia mahali huko nyuma
  mishahara ilikuwa ikiwahi kufikia tarehe 25 ya kila mwezi mishahara ya wafanyakazi
  inakuwa tayari imelipwa.


  >Utafiti wangu umenionesha kuwa kufikia mwezi July mwishoni mwaka huu, vyuo vinginena hata vyuo vishiriki vya CKD waliweza kulipwa mshahara wao wa Julai ambao ulikuwana ongezeko la kila mwaka (annual increament) lakini CKD haikuwa hivyo, tatizo ninini? Kuna wafanyakazi wamepandishwa madaraja zaidi ya miezi minne iliyopita lakinihadi sasa wanalipwa mishahara yao ya awali bila ongezeko la madarajawaliyopandishwa, tatizo ni nini? Kwa nini mliwapandisha madaraja kama hamkuwa napesa za kuwalipa? Kwa nini mnashindwa kufikisha taarifa zao kupanda kwao madarajakwenye mamlaka husika ili mishahara yao iletwe kwa wakati?


  >Usomi wetu uwapi kama tunashindwa kufanya kazi na kutatua changamotozinazotukabili? Kwa nini matatizo yale yale yajirudie kila mwaka na sababuzinazotolewa kila mwaka zinakuwa zilezile? Mishahara ya wafanyakazi
  inacheleweshwa halafu tangazo linawekwa likisomeka "Tunapenda
  kuwatangazia/kuwajulisha kuwa mishahara itachelewa...." Yaani umechelewa kuwalipa
  wafanyakazi wako halafu tena unasema "Ninapenda'? Kwa nini usiseme kuwa
  "Unasikitika kuwatangazia kuwa mshahara umecheleweshwa kwa....."?


  >Malimbikizo ya mwaka jana ya mishahara hadi sasa hayajalipwa, tatizo ni nini? Mimibinafsi tangu niajiriwe na nafikiri wapo wengi wa aina yangu, ni zaidi ya miakamitatu sasa sijalipwa pesa ya kujikimu iliyopaswa ilipwe (subsistence allowance).Hii ni pesa niliyopaswa kulipwa bila kujali nimeajiriwa toka wapi. Pesa ambayoingekuwa nisipewe ni ya mizigo kwa kuwa mimi niliajiriwa kutokea Dar es Salaam.Tulijaza fomu miaka kama miwili imepita sasa lakini kimya.


  >Tuache kufanya kazi kwa kutumia "vimemo". Tuammke na kuyafanyika kazi mahitaji yamsingi nya yakisheria ya walio chini yetu. This should be a waking call to Prof.Yunus Mgaya. Haya yote yanayotokea yako chini ya ofisi yako. Prof. Mukandala nawetunakuomba uyashughulikie masuala haya yanayokikabili chuo ambacho kwayo wewe ndiwekiongozi wake mkuu. Msipuuze hata kidogo na mkifanya hivyo mtkauwa mnafanya kwa
  hasara yenu wenyewe. Tuna tatizo kwenye utawala wa CKD. Kikubwa kabisa tuna tatizo
  sasa hadi kwenye uongozi wa UDASA, wote kimyaaa,utafikiri hawayaoni haya? Kuna
  faida gani sasa ya kukatwa pesa yangu kwenda kwenye chama kama Udasa au THTU
  ambacho hakina msaada kwangu? mambo yakiendelea hivi tutafanya ya Mheshimiwa Pinda,
  "Liwalo na Liwe" ili tujiondoe kwenye vyama kama hivi visivyo na tija kwa wanachama
  wake.


  >Kubwa zaidi ni kwamba wakati wakubwa pale wakisema hakuna pesa, wao wanajilipa helanyingi za wanachokiita "Responsibility Allowance". Aaaaaagh, kweli aliyeshibahamjui mwenye njaa!!! Mazingira ya kazi kwa sasa yanatushusha nguvu (demoralize)sana sisi "juniors" na tunashindwa kupata nguvu ya kutusemea kwa kuwa "seniors"ndiyo hivyo wako kwenye mikataba na wanaogopa kutusemea kwa kuwa kwa kufanya hivyomikataba yao itakuwa hatarini!!!


  >Siku zote tuiseme kweli ili kweli ituweke huru!! Tuna tatizo la kiuongozi CKD.
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  CKD ndio nini wakuu?
   
 12. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  CKD= Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
   
 13. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,721
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Mlimani aka Chuo Kikuu Dar es Salaam
   
 14. A

  Ame JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Umenifurahisha sana aise..Siku zote nasema hakuna wanafiki kama wanataaluma wa TZ wako out of touch na jamii inayowazunguka baada ya kupewa just enough for life na kuwazidi kwa mbali waajiriwa wakawaida....I hate their character kuliko kawaida...Ni watu ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa hii hali ya nchi yetu..Wamepewa nafasi za kisiasa na za kiuongozi kwa kiasi kikubwa katika hii serikali lakini wengi wamebakia kuwa vibaraka badala ya kutumia taaluma zao kukomboa nchii hii na kujenga uchumi imara...Wakose mishahara kabisa nitampongeza JK kwakugundua unafiki wa hawa ndugu zetu...
   
 15. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Thanx mkuu kwa ufafanuzi!
   
 16. A

  Ame JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Huko nilipo mm hao seniors kila tukikaribia ngazi ya kupata mafao mazuri wanapandisha ngazi juu ili wao waendelee kujilipa mafao makubwa maana tukiongezeka kwakua uchumi wa nchi haukuwi serikali itakataa kulipa hayo mafao wanayojilipa wao...Ole wao niwe mkuu wa idara hakuna cha mkataba wala nini...lol!

  Mi niliaacha hata kuangalia mshahara wangu kama napanda ama vipi maana nilikuwa busy kupata uhakika wa kuzalisha na si kula tu nisicho zalisha....Nimekuja gundua sijawahi ongezewa mshahara for about four years!

  I wonder what kind of people they are; badala ya kuwaza kuzalisha kilicho bora ili kujenga uchumi wa nchi kazi yao kuwaza how much benefit they can get as individuals nakujipendekeza pendekeza kwa wanasiasa....Nadhani siasa ya ujamaa (chama kushika hatamu) iliwa affect mno hawa watu mpaka hawaamini kama they can work ku-strengthen institution badala ya individuals....Kwaku jenga taasisi hata wao kama individuals watajikuta wanapata benefit kuliko wanavyofanya sasa...

  Mi natamani mishahara yote serikalini ingekuwa sawa then hawa ndugu watapata akili ya kusaidia nchi badala ya kuishi kinafiki kama wanavyofanya sasa...
   
 17. m

  mwamola Senior Member

  #17
  Oct 5, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tukubaliane wanataaluma kuwa tumelala mno. Kenya walimu wameweza, Tanzania kuna nini?

  UDOM hali ni mbaya zaidi kwani kuna walimu walipandishwa (promoted) november 2010 walikaa pasipokulipwa mshahara wao wa promotion miezi 13, walipokuja kulipwa walilipwa ule wa mwaka jana yaani bila increment. Kibaya zaidi wameendelea kulipwa mshahara kwa daraja (norch) la kwanza wakati tayari wana miaka mitatu kwenye daraja hilohilo. Mtu akiajiriwa leo kama mhadhiri msaidizi atalingana na mhadhiri msaidizi alieko na daraja hilo kea zaidi ya miaka 3. Ukiuliza kwa nini tofauti ya mishahara ipo kati ya UDOM na other public Universities unaambiwa hizo university zingine zinavunja sheria ya kuwalipa watumishi wao mishahara mikubwa kuliko UDOM. Nimekubali kuwa kweli UDSM wanavunja sheria kama wanapunguza mishahara ya watu kama vile UDOM inavyoweza kumlipa mhadhiri msaidizi mshahara sawa na tutorial assistant.

  Watumishi hao wa UDOM waliokuwa promoted 2010 hawajalipwa ARREAS zao kwa maelezo kuwa UDOM management hawajapeleka madai ya wafanyakazi wao tangu wawapromote 2010. Imefuatiliwa kuanzia hazina hadi utumishi hakuna maombi ya watumishi hao, swali HRM, PFA's wanafanya kazi zipi kwa UDSM na UDOM?
   
 18. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Duu haya madaraja ndo nini wajameni, nauliza tu wajameni msinishambulie, ukipandishwa daraja by default mshahara umepanda?
  Ningekuwa mimi serikali ningefutilia mbali kitu madaraja, kitu inakuwa hivi, mwanzo mwa mwaka unajiwekea/wekea malengo mwisho mwa mwaka unakaa na mwajiri wako anafanya annual assessment ya malengo uliyowekewa na kunegoatiate mshahara kulingana na maendeleo yako.
   
 19. m

  mwamola Senior Member

  #19
  Oct 5, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo la kukaa na mwajiri lipo kwani idara hujadili sifa za kila mtumishi. Hili la madaraja ni utaratibu usiokuwa na mpindo kuwa mtumishi akijiendeleza kusoma kozi tena inayozidi mwaka mmoja, anapashwa apandishwe daraja UDSM hapa wanafanya vizuri, UDOM wao wanadai wanafuata sheria. SWALI, hivi ni sheria gani inamweka mtumishi palepale miaka 3 bila kupata kinachoitwa annual increment? Na kama serikali ndo iliweka taratibu hizi, kwa nini UDOM wanavunja waziwazi na hawachukuliwi hatua kama si kukanywa?
  Timu ya ukaguzi ilikuja UDOM watumishi walilieleza hili na timu ile ilishangazwa kwa watumishi kukaa bila annual increment, kutopewa salary arreas, na kulipwa mishahara pungufu ya stahili zao kwa kivuli kuwa vyuo vingine vinavunja sheria
   
 20. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  wamekaa kisiasa badala ya kuzalisha elimu bora,wamepata stahili yao
   
Loading...