Mishahara Tanzania ni midogo mno

Mishahara Tanzania ni midogo mno

Ni kweli usemayo, ila maisha yetu ya kila siku huendeshwa kwa takwimu yaani namba halisi kilama
Nafikiri hawezi kupata takwimu za kila idara, si kazi nyepesi sana ingawa upo sahihi kujiridhisha kitakwimu ili kuondoa porojo za mtaani. Hahahaha japo yupo sahihi kwa ground.
 
Sio midogo mkuu;

Hiyo inaendana na hali ya uchumi wetu kabisa.

Watu wanasomesha, wanapatia matibabu familia, wanajenga, wanafungua biashara na kununua usafiri kwa mishahara hii hii.

Wewe ni na vipaumbele vyako.
 
Hautoshi hats kula nyama wiki mbili mfululizo.
Nyama kilo sh 14000
Michele kilo 3000 ule el classical
Mkaa 2000
Viungo 4000
Jumla 23000
Ukizidisha Mara 14 days hutoboi kwa mishahara ya bongo
23000*14=322000
Bado chai,
Kodi za nyumba
Nauli ya kazini
Hela ya watoto skuli
Matibabu
Umeme
Maji
Ushuru wa taka,kifupi watz wengi tuna unga unga mwana tu.
Duh
 
Hapo watu wa serikali ungewatoa kwanza hao mishahara midogo posho mlima..

Shida ipo sekta binafsi yaani kama nchi tumefeli sana kuwategemea wahindi na wachina ndio washikilie secta binafsi yaani wao wenyewe kwao maisha magumu eti ndio waje watukomboe sisi huku uwongo labda kama tuweke sheria kali sana za usimamizi..
Nchi za Wenzetu wote waliohakikisha European na American ndio wawekezaji wakuu wananemeka wale jamaa wana mbingu yao wale ni watu haswa..

Ila hawa wawekezaji jamii za asia ni vitoto vya shetani kabisa.
Wa asia kukulipa 5000 kwa siku wanaona sawa.
 
Kampuni nyingi mishahara yao ni laki tatu mpaka tano.
Unaweza ona kajamaa kaafisa mikopo kamenyuka pamba swafi, kinge kingi na plus unyamwezi kumbe mshahara 230k baada ya makato yao lukuki.
 
Chanzo mojawapo cha ukosefu wa mzunguko wa hela Tanzania, ni mishahara ni midogo mno.

Wafanyakazi wengi ambao wapo humu wapo kwenye wigo huo.
1. Mishahara ya serikali
2. Mishahara ya sekta binafsi.
3. Mishahara ya deiwaka
4. Mishahara ya wafanyakazi wa sehemu mbalimbali
5. Mishahara ya madeiwaka kwenye viwanda vya mabilionea wakubwa na wawekezaji wa ndani na nje wafanyakazi wanalipwa 5000 kwa siku hadi 10,000 kwa siku. Tajiri/mwekezaji/mkandarasi akilipa hela nyingi Haizidi 15,000.
6. Mishahara ya wafanyakazi kwenye miradi mikubwa ya ujenzi ni midogo.

Mzunguko wa hela unakuwa mgumu.
Mshahara hautokuja kutosha. Biashara japo kuwa ni ngumu ndio njia pekee ya kufanikiwa na kuchangia kuongeza mzunguko wa fedha.
 
Gentleman,
ni muhimu kujifunza na kuchukua hatua muafaka my friends, ladies and gentlemen,

wewe mtu alikua mbunge kwa miaka 10 na kwa mshahara wa zaidi ya milioni 10 kila mwezi, lakini ameshindwa kujenga hata kanyumba kamaana tu ka milioni 20 kwao, sembuse wewe mwalimu wa shule ya msingi, eti unategemea mshahara kuendesha maisha yako na ya familia yako?

Gentleman,
unafikiri na kuwaza sawasawa kweli? :pedroP:
Hakuna Mbunge mwenye mshahara wa 10M,mara ya mwisho nijuavyo mie mshahara wa Mbunge ulikuwa 4.5M au ww unahesabu na posho?
 
Hautoshi hats kula nyama wiki mbili mfululizo.
Nyama kilo sh 14000
Michele kilo 3000 ule el classical
Mkaa 2000
Viungo 4000
Jumla 23000
Ukizidisha Mara 14 days hutoboi kwa mishahara ya bongo
23000*14=322000
Bado chai,
Kodi za nyumba
Nauli ya kazini
Hela ya watoto skuli
Matibabu
Umeme
Maji
Ushuru wa taka,kifupi watz wengi tuna unga unga mwana tu.
Yan nyama iliwe siku 14 mfululizo?
 
Kampuni nyingi mishahara yao ni laki tatu mpaka tano.
Unaweza ona kajamaa kaafisa mikopo kamenyuka pamba swafi, kinge kingi na plus unyamwezi kumbe mshahara 230k baada ya makato yao lukuki.
😄 bongo ukipata sehemu wanalipa vzr ni kushukuru Mungu.
 
Chanzo mojawapo cha ukosefu wa mzunguko wa hela Tanzania, ni mishahara ni midogo mno.

Wafanyakazi wengi ambao wapo humu wapo kwenye wigo huo.
1. Mishahara ya serikali
2. Mishahara ya sekta binafsi.
3. Mishahara ya deiwaka
4. Mishahara ya wafanyakazi wa sehemu mbalimbali
5. Mishahara ya madeiwaka kwenye viwanda vya mabilionea wakubwa na wawekezaji wa ndani na nje wafanyakazi wanalipwa 5000 kwa siku hadi 10,000 kwa siku. Tajiri/mwekezaji/mkandarasi akilipa hela nyingi Haizidi 15,000.
6. Mishahara ya wafanyakazi kwenye miradi mikubwa ya ujenzi ni midogo.

Mzunguko wa hela unakuwa mgumu.
Tupo pamoja mond
 
Back
Top Bottom